Muongozo wa kozi ya kuchagua kwa undergraduate mwaka wa masomo (2017/2018)

hizi thread huwa zinanichanganya sana wengine wanasema CBG hawezi soma kozi ya afya hata moja ukweli ni upi na kama anaweza ni kwa vyuo vipi?
 
hizi thread huwa zinanichanganya sana wengine wanasema CBG hawezi soma kozi ya afya hata moja ukweli ni upi na kama anaweza ni kwa vyuo vipi?
Unasoma Mkuu
 

Attachments

  • Undergraduate+Admission+Guidebook+2014-2015_04_24.pdf
    0 bytes · Views: 109
Mwenye diploma ya computer engineering. Na anataka kuendelea Bachelor degree..
Degree ipinitamfaa na ambayo iko marketable kwa sasa?
 
Iko poa Sana tu due to mabadiliko ya Hali ya hewa inapelekea uhitaji wa wataalam wake kuwa kubwa muhimu sana
Watch out... Kama unataka kusoma diploma ya irrigation pale chuo cha maji ni bora ukasoma kozi ya water supply and sanitation eng iko wide sana compare to irrigation
 
NAWAKUMBUSHA TUU COURSE AMBAZO ZIPO NATIONAL INSTITUTE OF TRANSPORT - NIT

1. BLTM- Bachelor's degree in logistics and transport management

2. BATF - Bachelor's degree in accounts and transport finance

3. Kuna bachelor's education ya Mathematics and information technology

4. Pia kuna bachelor's degree in Automobile engineering. BAE. Hawa jamaa ni mainjinia wa Magarii

5. Pia kuna bachelor's degree in Aircraft engineering and maintanance
Hawa ni ma injinia wa ndege

Ada yake sasa
Mil. 10 na laki 5 jipangeeeeeeeee

Pia kuna bachelor degree zingine za kawaida kama vyuo vingine kama Procurement & logistics, BA, HRM, Marketing,

Bila kusahau kuna Diploma ya Freight clearing and Forwarding

Pia mashort course kibao. Kama professional driving. Fork lift. Ukaguzi wa magari. Automechanics

Pia unaweza tembelea site
Www.nit.ac.tz
 
Ivi kozi gani ya engineering ukisom ina urahis katik kupata nafasi za kwebda kusoma nje.. Schorlaship
 
Mimi nna diploma ya civil engineering, nataka kuhamia afya course gani ambayo haitanichelewesha kwenye upatikanaji wa ajira?
 
Mimi nna diploma ya civil engineering, nataka kuhamia afya course gani ambayo haitanichelewesha kwenye upatikanaji wa ajira?

Unamaanisha kuhamia afya kwa level ya digrii ilhali una diploma ya civil engineering ?

Mmmh mkuu, hiyo ngumu sana, ngumu kweli kweli and nearly impossible. Labda kama ulimaanisha kuhamia afya kwa maana ya kutaka kusoma diploma nyingine inayohusiana na afya. Hebu fafanua kidogo kabla sijaongea mengi.
 
Mwenye diploma ya computer engineering. Na anataka kuendelea Bachelor degree..
Degree ipinitamfaa na ambayo iko marketable kwa sasa?

Binafsi huwa napenda kushauri mtu asome kitu kulingana na interest zake zaidi kuliko kuliangalia soko la ajira zaidi. Na hii inatokana na kubadilika badilika kwa soko la ajira kulingana na wakati. (Ya leo sio ya jana, kesho si ndugu wa leo).

Tukiweka kando hayo, napendekeza asome kati ya kozi zifuatazo, ama aendelee na hiyo hiyo computer engineering, au asome telecommunications engineering, electronics au information technology (IT). Sharti ni moja tu, akajitume ili awe MAHIRI (competent).

Dunia ya sasa inazidi kuwa ya kisasa, tunashuhudia mabadiliko ya kiteknolojia kila kukicha, karibia kila kitu sasa kinafanywa kwa mifumo ya computer, bado kidogo hata sisi wakulima tutakua tunalima kwa matrekta yanayoendeshwa kwa computer, shamba linakua kwenye mfumo wa GPS, wewe uko control room unalima kama unacheza game la truck simulator. Hizi ni fursa kubwa za kupiga hela kwa wataalam wetu. Hizi teknolojia zinahitaji wataalam kwa ajili ya matengenezo na mambo mengine kibao.

Mara zote hua naamini kwamba
Competence + Interest = Success bila kujali ugumu wa mazingira yaliyopo.

NB: Japokua sio lazima uufuate, tafadhali ushauri huu uupe kipaumbele.

Kila la heri.
 
HGL naeza soma Bach, of science in land management and valuation japo mathematic Nina f

Frankly and honestly speaking, jibu ni NO.
Hesabu ni muhimu sana kwa kozi hiyo uliyoitaja, na ndio maana mara nyingi huwa wanachukua watu wa EGM, sasa kwa wewe ambaye mathematics una F itakua ngumu mno kuchaguliwa. Kumbuka kwamba hiyo kozi inatolewa na chuo kimoja tu kwa sasa (kama sikosei) ambacho ni ARDHI UNIVERSITY, hii itapelekea wewe kushindwa kufurukuta mbele ya waombaji wengine hasa wa EGM, PCM na wengineo mtakapokua mkiwania nafasi chache kwenye chuo hicho kimoja tu.

Anza kufikiria maisha bila LAND MANAGEMENT AND EVALUATION kama hautojali.
 
hizi thread huwa zinanichanganya sana wengine wanasema CBG hawezi soma kozi ya afya hata moja ukweli ni upi na kama anaweza ni kwa vyuo vipi?

Neno KOZI ZA AFYA ni pana sana na linajumuisha kozi nyingi humo ndani. Kwa hiyo CBG yako, kuna kozi za afya hauwezi kusoma mfano MD, Pharmacy nk lakini pia kuna kozi za afya unaweza ukasoma mfano Nursing, Midwifery, kozi kadhaa za maabara nk.

Kwa msaada zaidi tafuta kitabu elekezi (Guidebook) cha TCU utakutana na dozi nzima ya maelezo na maelekezo yatakayokata kiu ya dukuduku lako.
 
Back
Top Bottom