Mungu nisaidie nisifikie hatua hii!!

Baadhi ya wanaume ni makatili na wana roho mbaya kupita kiasi. Inasikitisha sana.

Jamani kuna watu wanaishi maisha ya ndoa kwa kuvumilia sana!Hakika mwanamke kapewa moyo wa uvumilivu sana. Mwanamke anaweza fanyiwa ubandidu na madharau na mumewe lakini akaendelea kukomaa tu kama vile aliokotwa porini na hana kwao

Asubuhi nimeshuhudia tukio la kusikitisha sana jamaa akimfanyia mkewe. Jamaa walikuwa bank akionekana kumuacha mkewe nje...baada ya kumaliza na kutoka alisogea alipokuwa mwanamke mmoja mpole aliyekuwa kapakatia kitoto cha miaka kama minne hivi cha kiume kilichofanana na jamaa!

Jamaa akasogea akiwa umbali kama hatua 20 akamwambia yule dada(naamini ni mkewe)....."weeeee" kwa sauti ya ukali..... yule dada alivyostuka akamwonyesha ishara(kibabe) waondoke

Nikavutiwa sana na tukio.Wakasogea kituo cha daladala na mimi nikowafuata karibu. Binti akamzunguka jamaa akaenda kusimama nyuma yake akiwa hana raha. Jamaa akaita bodaboda akapanda bila kumsemesha yule binti na kuondoka. Yule binti naye akaita yake na kumfuata

Kwa kweli imenifikirisha sana wanandoa tena wa umri huu(kwa muonekano ni chini ya miaka 35) wanawezaje kuishi maisha haya kama wanyama?
Naomba Mungu asinifikishe hapa
 
Huyo Dada aonyeshe msimamo bado mapema otherwise huyo mwanaume anaeza kukuchamba mbele ya mama ako.

Hakuna kitu kinaumiza nafsi kama kudharauliwa hususan mbele za watu.
 
Ndo maana upo muda wa uchumba... Na kwa ushauri zaidi mnaambiwa msiowane kama hamjajuana vizuri... Naweza ni kasema hathari kama hizi zinaletwa na zile tabia zetu za kuingiza tu ndani bila hata kusomana kitabia
Inatia huruma! Wanaume wengine ni wakatili sana!
Hapo mdada itakua anaishi kwa woga.
 
15625362_822367394570468_138304690029854720_n.jpg
 

Attachments

  • 15625362_822367394570468_138304690029854720_n.jpg
    15625362_822367394570468_138304690029854720_n.jpg
    26 KB · Views: 45
Unanikumbusha tabia ya wengi wetu, akiona tukio ataacha hata shughuli zake, akafuatilie na kupoteza mda wake mwingi tu kufuatilia mambo yasiyomhusu.

Imagine ulikuwa unaenda sehemu muhimu, lakini ukaacha kabisa na kwenda hadi kituoni kumfuatilia jamaa.
 
Unanikumbusha tabia ya wengi wetu, akiona tukio ataacha hata shughuli zake, akafuatilie na kupoteza mda wake mwingi tu kufuatilia mambo yasiyomhusu.

Imagine ulikuwa unaenda sehemu muhimu, lakini ukaacha kabisa na kwenda hadi kituoni kumfuatilia jamaa.

SHILAWADU katika ubora wake
 
Ni ngumu kuchukulia kwa asilimia zote kwamba huyo dada anadharauliwa kwa sababu pia inatakiwa tujiulize kwa nini alivyoitwa kwa ishara alienda nadhani ndio maisha aliyoyachagua hivyo hakuna wa kumlaumu hapo.
 
Back
Top Bottom