SaulGoodman
JF-Expert Member
- Nov 12, 2020
- 416
- 904
Habari za wakati huu, naomba ku declare interest kua muhusika mkuu wa kisa hiki sio Mimi lakini baada ya kusimuliwa nimeona ipo haja ya ku share na wewe tiririka nayo.
Mwaka 2016 nikiwa nimetoka mzigoni baada ya kuunganisha night mbili na day moja (hii ni ratiba ya kawaida kabisa kwa intern doctor hasa wale wenye njaa ya pesa😁. Unaingia night yako ukitoka jamaa anakulipa uingie ya kwake..
Na kesho yake unapaswa kuwa kazini kama kawaida, hivyo unaweza kujikuta ghetto hujapapita hata siku 😊.
Jioni hiyo nikijiandaa kutoka jamaa yangu Sana toka O-level akanipigia simu na kuniomba japo nikipata muda tutafutane.
Jamaa ni mtu wangu wa karibu Sana ambaye tuliishi wote ktk jua na mvua, Raha na shida na kiukweli sababu life kipindi fulani lilikuwa pangu pakavu tia mchuzi huyu jamaa ndiye alikuwa ananiweka mjini kwa sehemu kubwa enzi hizo za shule ya sekondari. Ukiongelea habari ya best friend Basi ni huyu jamaa.
Basi nikaona jioni ile badala ya kwenda ghetto niende nikaonane naye, nikapanda daladala m/mbusho-mbezi nikashukia mitaa ya makabe.
Kipindi hicho jamaa naye kamaliza chuo anasikilizia mishe mishe Basi akawa anasimamia hardware ya ndugu yake mitaa hiyo.
Tuliongea na kukumbushana mengi Sana baada ya kupotezana kwa kipindi, giza likaingia nikawa najiandaa kurudi maskani, jamaa akaniulizia ratiba yangu kesho yake nkamwambia mchana ntakuwepo free nataka nilale kidogo maana usiku nitarudi night hospitali.
Jamaa akanisihi tulale kule, baada ya kuchekecha nw kuona hakuna cha kuwahi ghetto nikakubaliana naye, Basi ndio ikawa kama story zimeanza mwanzo kabisa.
Jamaa naye akaamua badala ya kwenda kulala nyumbani anapoishi (Mbezi Luis) akaona Bora tulale pale pale hardware.
Sababu nyumbani kule kulikuwa geti Kali na too much protocol (wa ushuani wananielewa😅😅) hivyo tungeenda kule hata Uhuru wa kupiga story usingekuwepo kivile, lkn pia pale hardware kulikuwa na room za kuishi wafanyakazi na mlinzi, hivyo nafasi ya kulala ilikuwepo pia.
Story ziliendelea mpaka usiku wa manane baadae watu tukapotelea usingizini. Jamaa yangu aliamka mapema sana ili kukimbizana na order za wateja asbh asbh, kumbuka miaka hiyo gomba ndio inaanza kujengwa kwa sana na bado uchumi haujabana sana hivyo order zilikuwa nyingi sana.
Mbulula Mimi bado nilikuwa kwenye usingizi wa pono baada ya ile mikesha hospitali na shida ikaanzia hapo😂😂😂.
Ratiba ya pale saa 11 gari zimeanza kutoa mzigo so wengi wanaamka kabla ya hapo.
Mishale ya saa moja na nusu Mimi bado nikiwa ndani ya shuka akaja mlinzi wa pale😁.
Ukiachana na sifa ya mlinzi kupaswa kuwa serious na mkakamavu huyu jamaa yeye alikuwa ni mnoko kwa maana halisi na vibarua wote pale walimjua, ukija Kama humjui unaweza ukadhani Ni mwenye Mali kumbe kapuku mwenzangu tu🤣🤣.
Basi jamaa aliniamsha kwa fujo saaaana.
Mwizi si mwizi kibaka si kibaka😁😁, maneno machafu ya kila aina yalimtoka, nadhani alifahamu nimekuja kuomba kibarua pale.
"Wewe umelala Hadi saizi ndio umekuja kukuta godoro mjini umezoea kulalia ngozi ya ng'ombe 😂😂, changamka hapa n mjini wewe usidhani utabebwa kila siku.
Jamaa yako kakuthamini pa kulala humuoni kaamka mapema, wewe ndio umelala hadi saizi".
Kiukweli jamaa alishambulia kutoka kila kona kitu ambacho sikuwahi kukiona hapo kabla😂😂😂
Basi nikajikongoja nikaamka na kukung'uta mavumbi ya cement (si unaelewa wanakolala mafundi)
Nikatoka nikaenda kwa jamaa yangu akaniuliza kulikoni niamke mapema vile na sijalala siku 2 na si Kwamba nna kazi yoyote ya kumsaidia pale.
Nikamzuga tu kutoyafanya kuwa makubwa tukaendelea na story nyingine.
Dk 2 nyingi mkulungwa kaja kalianzisha mwanzo kabisa pale pale Tena😂😂
"We mfundishe maisha jamaa yako atakuja kuolewa mjini hapa"😁😁
Na usidhani chai nnayochemsha jikoni ntamhesabu, (Kumbe moja ya jukumu lake ilikuwa n kuwaandalia mafundi na vibarua chai asbh, Basi nkatolewa kwenye list hata kabla ya moto kuwashwa😂😂. Jamaa yangu kuona vile..
Akaniomba msamaha kwa niaba na baadae kunielezea kumbe jamaa pale kaja hata mwezi hajamaliza ndio walimuombea kazi ya ulinzi kwa boss ila pale saizo anakaribia kumpanda kila mtu kichwani.😄😃
Basi baadhi ya vibarua pale wakaniomba nipotezee tu na nimzoee jamaa coz hajastaarabika
Mara mama lishe akaja kuchukua order ya chapati pale kwa vibarua nkamwambia atuletee chapati zinazotutosha na pesa yake nikampa, jamaa wakanishukuru kwa chapati mara jamaa akaja na chai yake wadau wakanywa.
Baada ya kusikia zile chapati nmenunua mm akapiga bango Tena😂😂😂😂
Hizi fujo tuu za hela ya chenji kwa konda akija mjini, acha ziishe anye mavi yake😂😂😂
Uzuri hatufahamiani mm nkawa naendelea na story na wajamaa.
Jamaa wakamsihi pia asiwe mtu wa kutukana kila mtu maana kumbe hata wanaokuja kutafuta kibarua pale wanaipataga fresh🤣🤣🤣.
Kama lisaa hivi naaga niondoke jamaa wanapakiza mzigo (nayeye alikuwa anaomba apakize japo apate za maji) ikatokea sijui ameshikaje bati wakati wa kuifunga ikafyatuka ikamkata vibaya mno mkononi.
Ghafla damu zikaanza kuruka Kama bomba lililopasuka😭😭
Mtafutano ukaanza
Hospital ya karibu ni Bochi ambayo hata nauli ya kukodi bajaji haikuwepo achilia mbali hiyo hela ya matibabu.
Boss amepigiwa simu anasema mm nilimuajiri kulinda, sababu kazi aliyokuwa anafanya malipo yake Ni nje ya mshahara wangu na sikumuajiri kwa Hilo Basi sihusiki.
Mpaka muda huo hatujafahamiana nani ni nani zaidi ya masimango ya kuelekea upande wangu mwanzo mwisho😁
Uzuri ni Kwamba nilikuwa natembea full mkoba, rasket Ina nyuzi, lignocaine, packed sterile gauze, drips na vikorokoro vingine vyotee, kifupi n portable minor theatre 😁.
Na hii ilikuwa maalumu kwa zile circumcision za ushuani ambao hawana time ya kupeleka watoto hospital + home wound dressing.
Basi nikaondoka eneo la tukio na kurudi ndani nilikofurushwa asbh na kuchukua mkoba wangu na kuja nao pale. Kwa yote yaliyotokea jamaa yangu akanizuia.
Kabisa kumsaidia yule jamaa akidai inabd apambane mwenyewe akili zimrudi na aheshimu asiowajua😊😊.
Kimaadili daktari hata ukiwa vitani akitokea adui anataka kuwaua ukamuwahi na kumjeruhi unapaswa ukishamuweka chini ya ulinzi umtibie tena kiroho safii😁😁😁
Baada ya kukumbuka hilo nkamwambia jamaa yangu hutanizuia kumsaidia huyu jamaa, Kwanza nikimlipa anavyofanyia wengine hatajifunza lolote. Nikamsogelea hali akiwa yuko hoi watu washafunga kidonda hakifungiki nikamuuliza Kama Yuko tayari nimsaidie kumtibia akawa hajui asemeje😁😁
Vibarua wengine wakawa kama wameduwaaa na kujiuliza huyu mtu ni Nani Hadi pale walipoona mikasi inatolewa na gloves zinavaliwa.
Nilimtibia jamaa vizuri kabisa kwa kumsafisha na kumshona nkamaliza nikatoa karatasi nikaandika dawa, nikampa kibarua fulani pamoja na pesa akalete dawa.
Nikamuelekeza jamaa namna atakavyotumia dawa nikaweka vifaa vyangu mkobani nikasimamisha bajaji na kutoweka..Sikutaka kuendelea kusikia kinachoendela huko nyuma ila jamaa yangu anadai kila mtu siku hiyo alikuwa na story yake na funzo lake.
Jamaa alipona na kuendela na majukumu.