Muhimu: Chukua mwenza wako mkapime UKIMWI

Kamwe sitofunga safari kwenda hospital kupimwa ukimwi. Na nilisha mwambia mwenza wangu akipata ukimwi Ni wa kwake, atajua Kwa kuupeleka
 
  • Thanks
Reactions: TBO
Pamoja na kwamba ukimwi unaonekana kama vile ni ugonjwa wa kawaida, lakini, Ah wapi, ukimwi bado ni noma sana, ukiupata ndio utanielewa. Kuna jamaa zangu fulani walishawahi kunipigia simu kila mtu kwa wakati wake tofauti, kueleza masahibu ya ukimwi yalivyowapata. Ajabu ni kwamba walikuwa bado hawajawaeleza wenza. Niliwaambia acheni ujinga, waambieni wenza wenu kuwa mmeathirika ili kuwanusuru. Nimegundua kuwa wote wanaume kwa wanawake wana tabia ya kuwaficha wenzi wao pindi wanapokumbana na hilo janga. TAFADHALI ACHA KUISHI KWA MAZOEA, MCHUKUE MWENZI WAKO, AKIKATAA, TUMIA NGUVU ZA ZIADA MKAPIME ILI KUBAINI KAMA MNA MAAMBUKIZI AU LAH, MKIJIKUTA MNAO AU MMOJAWAPO ANAO, MTAJUA NAMNA YA KUISHI. Nawaambia baadhi yenu hamtaamini, matokeo, na kwa kweli kama utazingatia ujumbe wangu, nitakuwa nimekunusuru!
Ukimwi upo tena kwa kasi kubwa zaidi, hasa Dar.
we mwenyewe umeshapimaaa?? MAJIBU JE?
 
unapima kila mara.. unaonyesha unajishughulisha sana kwenye mchiriku etiee.. bila kinga.
weka ushahidi hapa usituzuge na mipasho yako

Ngono na mimi wapi na wapi mkuu, ni kama magharibi na mashariki.
 
Ukweli ukimwi bado ni jinamizi linalotisha sana.
Tumebaki masikini wa kutupwa ndg zangu wote wanne wamekufa kwa ngoma ktk umri ambao tulikuwa tunawatadhamia sana.

Hakuna furaha tena ktk familia yetu.

Familia zao zote ziliishia kutengana.
Watoto wamekuwa wa kulushwalushwa hakuna hata wa kuwasaidia.

Jamani umakini unahtajika sana.
Haitupasi kuendekeza starehe za ngono na kuzani tutabaki salama.
Oh, nimeshikwa na simanzi. Huu ugonjwa umesababisha umasikini na upweke kwa baadhi ya familia.

Take courage brother. Abstinence ndio njia pekee ya kuepuka kupata hili gonjwa, tukioa/tukiolewa, tuacha kurukaruka, wala hatutapata chochote zaidi ya kuzisononesha familia zetu.
 
Back
Top Bottom