Mugabe alionya baraza la usalama la UN, asema Kikwete aliambiwa akabidhi madaraka chama kingine

Wadhungu ni wanani kwa tanzania??
Wahuni fulani hivi. Alafu ajabu hivi kwa mfano marekani kwenyewe mbona demokrasia inanyongwa hivyo? Kwanini hawataki kuruhusu na wao vyama vingine viongoze badala ya kila siku kubebana wao wenyewe democratic na republican, hiyo ndo demokrasia?
 
Kila mtu mwenye akili anajua nchi za magharibi hazikufurahia ccm kurudi madarakani.

Kawaida wao hawataki nchi wanazozinyonya ziwe stable
 
Kwahiyo na mwl Jk tumuweke ktk kundi moja?


Tofauti ni kwamba Nyerere alikuwa anajitambua na alikuwa anapenda kucheza bao to gather information za watanzania ila kwa JK yeye alikuwa anapenda kupiga porojo na kuteta watu na alikuwa hajitambui mpaka hivi sasa sidhani kama anajitambua.
 
africa ina kila mifano ya tawala zisizozingatia demokrasia zinazonuka rushwa na ukandamizaji na ufisadi unaofanywa na ama viongozi wenyewe au wapambe wao bila wasiwasi tuna serikali dhaifu sana ambazo zinashndwa kukusanya kodi hivyo kushndwa kutoa huduma kwa wananchi wake viongozi wa afrika ni mahodari sana wa kuimarisha majeshi kwa gharama yoyote ili yawasaidie kubakia madarakani kinachoshangaza ni kwamba wamekazana kutuaminisha kua wachawi wa maendeleo yetu ni wazungu wanaacha kuambiana ukweli wanalishana ujinga hivi ni mzungu gani aliiambia tz inunue washawasha 700 wakati kilombero hakuna daraja,shule hazina madawati,wakulima hawana mbolea,dawa hakuna, viongozi wetu waache ujinga wabadili mtazamo wakumbuke kua ili kuimarisha uchumi huitaji propaganda unaitaji kufanya kazi
 
Kwa hali ya kawaida tu, mugabe kishazeeka hana uwezo wa kufikiria tena
 
mbaya zaidi waafrika mbumbumbu wanaamini mugabe anapambana na wazungu na shujaa kumbe ni nyenzo yake ya kisiasa. bora ukoloni urudi. bibi yangu hunisimulia jinsi serikali ya mkoloni ilivyokuwa efficiency.
 
Kama alivyosema mdau mmoja,Mugabe ameshachoka na ni Dictator.Statement aliyoitoa Addis Ababa juzi kuhusu wazungu ni kwamba anatafuta sympathy.Hana lolote.
 
Zimbabwe ya sasa umsifie Mugabe ? Wakina mama na watoto wanakufa pori la messina kwenda kutafuta chakula South Africa..maisha sio Zimbabwe na hili janga la njaa ndio linamuumbua zaidi maana aliokua anawaponda ndio wamekua mstari wa Mbele kumwaga chakula..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…