Jephta2003
JF-Expert Member
- Feb 27, 2008
- 6,575
- 6,328
Unaposema Mungu aliyehusika na uumbaji anaitwa ELIOH,ukimanima kuna Mungu zaudi ya mmoja,mbona tunafundishwa kua Mungu ni mmoja tu?,uko hapa kutopotosha kwa madhumuni yepi?Kwanza punguza ukali wa maneno,pili hakuna sehemu ambayo nimejinasibu kuwa naijua biblia.Kimsingi mawazo hayo yakiyoandikwa ni yakwangu ila kama kuna mtu umemsoma naye akasema nilivyosema na jambo la kawaida tu,mana ufanano wa kimtazamo si jambo geni.
Iko hivi,
Neno EL ni neno la kiebrania ambalo kwa kiswahili maana yake ni Mungu.
Neno hilo huweza kukaa mwanzo wa neno au mwisho wa neno ili kumaanisha kitu flani pia.
Mfano
ELia( El- ia)
ELisha( El_isha)
ELohim(EL_ohim)
EmanuEL( ema-nu-EL)
GabriEL( gabri-EL)
MikaEL(mika-EL)
kimsingi mifano iko mingi sana.sasa neno EL likikaa mwanzo wa neno huonyesha uwezo wa Mungu katika kufanya jambo flani,lakini likikaa mwisho humaanisha sifa ya Mungu katika jambo flani.
Sasa kwenye biblia ya kiebrania Mungu aliyehusika na uumbaji,anatambulika kwa jina la ELOHIM.
Rejea mwanzo 1:1 kwa kiebrania ( Bara shit baraad ELohim) hapo nimeandika kama inavyosomeka,mstari huu humaanisha Hapo mwanzo Mungu aliumba.
Sasa katika baadhi ya lugha za wenzetu majina ya vitu huwa na jinsia.
Mfano kwa waspanyora,neno likiishia na A huwakilisha jinsia ya kike na likiishia na O huwakilisha jinsia ya kiume.( Chika bonita/ msichana mrembo,chiko bonito/ mvulana anayevutia)
Hivyo neno ELOHIM ni jina la Mungu ambaye alihusika na uumbaji na lipo kwenye mfumo wa uwingi.( Mungu katika uwingi)"na tuumbe mtu kwa mfano wetu"
Neno hilo ELOHIM hubeba jinsia zote kwani kama lingebeba jinsia ya kiume tu lingetamkwa ELOO na kama lingebeba jinsia ya kike lingetamkwa ELOA ila kwa kuwa linabeba jinsia zote ndo mana hutamkwa ELOHIM.
Sasa katika lugha ya kiswahili tunamapungufu ya kimsamiati mana hatuna neno la kiswahili ambalo humaanisha uwingi wa neno Mungu.
Hivyo basi kwenye uwingi tunaweka Mungu na umoja tunaweka Mungu tu.
Sasa kwakuwa tunaumbwa na Mungu ambaye ndo ELOHIM na yeye anabeba jinsia zote mbili ni wazi hata wakati anaumba hakuumba jinsia moja tu,bali aliumba zote mbili kwa wakati mmoja.
Sasa ukinibishia na kusema kuwa adamu ni mwanaume basi ntakuomba ufafanue mwanzo 5:1_3
Pia naomba usichanganye kati ya uumbaji na hatua za ukuaji.
Mana unapozungumzia utengano kamili wa jinsia,hapo sio uumbaji bali ni hatua za ukuaji tu.
Naomba utumie lugha za staha na wala si za kudhalilisha mana mimi na wewe wote hatujui biblia,ila tunasoma na kujifunza tu.