Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,147
- 21,165
Kuna tukio la hivi karibuni la Kibaha, ambapo wazazi wa mtoto wa kike wa miaka 8, Angel, mwanafunzi wa darasa la 2, walienda Polisi kuripoti kupotelewa mtoto, wakaambiwa Polisi hawawezi kupokea taarifa yao ya kupotelewa mtoto na inabidi wasubiri kwanza masaa 24 ndio wakaripoti kupotelewa mtoto.
Kesho yake huyu mtoto alipatikana akiwa ametupwa kwenye shimo la choo na akiwa amekufa. Ninashawishika kwamba kama Polisi wangeanza kufanyia kazi taarifa za kupotea mtoto pale zilipotolewa mara ya kwanza, huenda mtoto angepatikana akiwa hai.
Katika nchi nyingi, kama sio zote, suala la kusubiri masaa 24 kabla ya kutoa taarifa ya kupotea mtu, linahusu watu wazima, sio mtoto. Sasa najiuliza, hapa Tanzania tuna utaratibu tofauti wa kuripoti kupotelewa mtoto na polisi kuipokea hiyo taarifa rasmi, kwamba hawawezi kuifanyia kazi kabla masaa 24 hayajapita?
Kama ni kweli kwamba uratatibu wa Polisi hapa nchini kuhusu mtoto anaeripotiwa kupotea unahitaji yapite masaa 24, basi natoa wito kwa Raisi Samia na Waziri wa Mambo ya Ndani, kwamba itolewe amri ya DHARULA MARA MOJA, utaratibu huu ubadilishwe sasa hivi. Mtoto chini ya miaka 16 (au hata 18) akiripotiwa kupotea kituo cha polisi, Polisi wanatakiwa wapokee hiyo taarifa rasmi na kuanza kuifanyia kazi mara moja. Masaa 24 iwe ni kwa mtu mzima tu.
Na kama Polisi Kibaha waliwapotosha hawa wazazi wa huyu mtoto kuhusu kusubiri masaa 24, basi hatua kali za kisheria zichukiliwe dhidi ya Polisi wote waliohusika na wanaowajibika na hao waliohusika.
Nyumbani kwako kuna mtoto mdogo wa chini ya miaka 10? Sasa fumba macho, fikiria kwamba amepotea, hujui alipo, hujui kama amekula au la, hujui kama analia kwa uoga hapo alipo au la, hujui kama ana maumivu, analia kukuita umsaidie, hujui kama kuna mtu anamtesa, anamuumiza, anamfanyia vitendo vibaya kama ubakaji au ulawiti, anamchapa fimbo au ngumi kumlazimisha. Damu zinamtiririka sehemu sehemu, na amevimba viungo kadhaa vya mwili. Halafu unaenda polisi kuomba msaada waanze kuchunguza yuko wapi, alionekana na nani mara ya mwisho, wanakuambia subiri masaa 24 yapite!
Habari kamili iko Mwananchi

Uamuzi wa Polisi wasubiriwa maziko ya mwanafunzi aliyepotea, mwili kukutwa shimoni
Mwanafunzi Angel alipotea Mei 6, 2024 baada ya kuondoka nyumbani kwao akimfuata dada yake aliyekuwa amekwenda kusuka mtaa wa jirani na makazi ya familia yao
www.mwananchi.co.tz