Mtoto wa Kike wa Tanga aliyesifiwa kujua Lugha ya Kiingereza kwakuwa kasoma Shule za 'Kata CCM' amewaumbua Wanaomsifia na aliye Ziarani

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
60,833
121,788
Nimemsikia mwenyewe (tena kupitia TBC1 Taarifa ya Habari ya Saa Mbili usiku huu) huyo Msichana akisema kuwa kwa 95% hicho Kiingereza ambacho CCM na Mwenyekiti wake Taifa pamoja na Chawa Gegedu wake wanamsifia na kusema kuwa ni Faida ya Shule za Kata CCM hakujifunzia Shuleni hapo japo alikiri kuwa kwa hapa na pale Walimu walimsaidia Kumuelekeza tena pale ambapo walijua kuwa Kaandaliwa kuonana na Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa.

"Namshukuru sana Kaka yangu ambaye ni Msomi mzuri na katembea nchi nyingi kwa Kunifundisha hii Lugha na pia kuniwekea App Maalum katika Simu na Laptop yake ya Kujifunza vyema Kiingereza na nilikuwa kila nikijifunza huko naenda Kuongea (Kuwaonyesha) Wazazi wangu na hata nikienda Shuleni nilikuwa sioni Aibu kuzungumza mbele ya Wanafunzi wenzangu" amesema Msichana wa Tanga aliyesifiwa Leo na aliye Ziarani huko katika Ziara yake.

Na GENTAMYCINE namalizia kwa kusema kuwa tusidanganyane Shule zote za Kata Tanzania ni ICU ya Kitaaluma sawa?
 
Kiingereza ni lugha tu.
Issue ni maarifa, wengi hawana maarifa licha ya kujua lugha, lugha ni nyenzo ya kuwasiliana tu na wala haihusiani na maarifa nikadhani wamemsifu kwa kuwa na taaluma ya hali ya juu, ubunifu na ugunduzi wa mbinu za kutatua changamoto za nchi hii.
Kumbe ni lugha😂 hii nchi inaufala mwingi.
 
Nimemsikia mwenyewe (tena kupitia TBC1 Taarifa ya Habari ya Saa Mbili usiku huu) huyo Msichana akisema kuwa kwa 95% hicho Kiingereza ambacho CCM na Mwenyekiti wake Taifa pamoja na Chawa Gegedu wake wanamsifia na kusema kuwa ni Faida ya Shule za Kata CCM hakujifunzia Shuleni hapo japo alikiri kuwa kwa hapa na pale Walimu walimsaidia Kumuelekeza tena pale ambapo walijua kuwa Kaandaliwa kuonana na Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa.

"Namshukuru sana Kaka yangu ambaye ni Msomi mzuri na katembea nchi nyingi kwa Kunifundisha hii Lugha na pia kuniwekea App Maalum katika Simu na Laptop yake ya Kujifunza vyema Kiingereza na nilikuwa kila nikijifunza huko naenda Kuongea (Kuwaonyesha) Wazazi wangu na hata nikienda Shuleni nilikuwa sioni Aibu kuzungumza mbele ya Wanafunzi wenzangu" amesema Msichana wa Tanga aliyesifiwa Leo na aliye Ziarani huko katika Ziara yake.

Na GENTAMYCINE namalizia kwa kusema kuwa tusidanganyane Shule zote za Kata Tanzania ni ICU ya Kitaaluma sawa?
Kingereza kumbe ni kipimo cha elimu ah aha ha aa aha aaa hovyo kabisa nchi ya matahira hii
 
Shule anayosoma no ya kata na anajua kiingereza huo ndio mjadala. Sio bidii ipi na msaada upi kapata muhimu msingi wa kuingiza elimu kichwani ni shule ya kata ndio imemuwezesha.
 
Mbona wengine tupo mitaani hata hizo kata hatujasoma lakini tunajua kiingereza vema tu, tena British english na American english, tunatema slang kama tupo Marekani kumbe tupo bongo kwa mtogole. Ongeza na Irish english tunaongea kama maji. Wahindi, waarabu na waafrika wenzetu wa south afrika, nigeria, kenya na uganda na kule zambia na zimbabwe tunaona kama wanaongea kiingereza cha kishamba kama watoto wa english medium za bongo
 
Back
Top Bottom