Mtoto aliyezaliwa 2004 mwaka huu anamaliza la saba, Mbowe na CHADEMA mnaujua ukweli huo?

CDM ni 13 yrs old, CCM ni zaidi ya 50 na nusu yake ilitumika na hayati Mwalimu Nyerere, mmekuwa mnabadili watu na sio sera, chama ni kile kile na sera ni zile zile hata mngekuwa mnaachiana asubuhi na jioni bado atakayekuja ataendesha chama kwa sera hizo hizo kwa hiyo usituzuge kwa mtindo wa kubadilishana mashati ndio utuambie mna demokrasia ndani yenu mngekuwa mnataka demokrasia mngeachia madaraka kwa vyama vingine ili muweze kujifunza mnapokosea! Kama ilivyo America na ulaya au nchi zilizoendelea kwa demokrasi!
Mkuu CDM imeshindwa hata kufanya hilo zoezi la kubadilishana watu. Mwalimu alipoondoka akaja mzee Mwinyi, alipoondoka akaja Mkapa, alipoondoka akaja Kikwete na sasa JPM kakabidhiwa kijiti.
CDM ili iweze kuwa taasisi ni lazima yenyewe iwe juu na sio mtu kuwa juu. Chama kikubwa cha siasa siku zote hufanana na imani katika kitu fulani, ndio maana hata kama mwenye mamlaka anapendwa kupita maelezo ipo siku yake ya kuachia nafasi kwa wengine.
 
Afya ya kisiasa wewe ndio docta unataka kuitibu au? Mbona Luna ugonjwa uko wazi sana, si ungeanza kuutibu huo wa kuzui mikutano ya siasa? Au una makengeza!! Kwako wewe demokrasia ni uenyekiti wa Mbowe tu, au? Kwa taarifa yako ukiona watu wanakuzungimzia kwa chuki za bila sababu ujue wanakukubali.
Povu linakutoka mpaka unanichafulia shati langu. Mkuu huu ni wakati wa damu mpya kufikiriwa kupewa nafasi CDM. Maana ya ukomavu wa kisiasa ni kuwa tayari kuendana na dunia kadri inavyobadilika.
 
Uliona wapi adui yako anakuchagulia mpiganaji wa kupigana naye?

Mbowe ataendelea kuwepo sana, ilimradi hajavunja katiba ya Chadema.

MaCCM Mbowe ndio kiboko yenu.
Huyo aliyebadilishia gia angani hawezi kuwa kiboko ya mtu yoyote. Leo hii mzee wa Rada akiamua kujiunga na CDM atapewa utakaso wa kipekee, ambao hata Papa wa Roma hajawahi kuusikia.
 
Zanzibar jahazi linasonga kama kawa, mtu akisusa wengine wanakula.

Mkuu Aikaeli ananyima nafasi ya kuchipuka kwa kizazi kipya cha uongozi. Vinginevyo ondoeni neno Demokrasia kwenye jina la chama.

Nakubaliana Na hoja yako mkuu,Chadema wanapaswa kuidhihirisha demokrasia inayobeba jina la chama chao kama vile CCM walivyoidhihirisha dhana ya MAPINDUZI kwa kupindua matokeo ya urais ya 2015,heko ccm huo diyo ukomavu.
 
Nchi. ipo chini ya CCM miaka zaidi ya hamsini dawa za chanjo tuu ni shida na tuna kila kitu unazungumzia Ghana vyama vya upinzani kweli!!!
 
Mwaka 2004 ndipo Mkuu Freeman Mbowe alipochaguliwa kuwa mwenyekiti wa taifa wa CDM.

Mtoto aliyezaliwa mwaka huo, mwaka huu anafanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi.

Kwa maneno mengine huu mwaka 2017 ni wa 13 wa uongozi wa Kaka Mbowe.

Taratibu siku zinasogea, ikifika January 2018 utakuwa ni mwaka wa 14 kwenye uongozi.

Unaposema JPM ni one man show inabidi pia uwe na ujasiri wa kusema CDM ni one man party.

CDM inahitaji damu mpya, akili mpya, fikra mpya, na yote hayo kutoka kwa uongozi mpya.

Achana na habari kwamba siasa zimepigwa marufuku, maishani binadamu ili afanikiwe ni lazima awe na sifa ya kubadilika kutokana na wakati usiomsubiri mtu.

Wazungu husema adaptability, uwezo wa kufanana na mazingira yanayokuzunguka haswa jinsi yanavyobadilika.

Ifike mahali mwana CDM mwenye kupenda mabadiliko awe tayari kujenga hoja kwenye mikutano ya ndani, juu ya umuhimu wa chama kupata visions mpya.

Uhai wa CDM ndio uhai wa CUF na ndio uhai wa CCM, twende mbele turudi nyuma.

2017 uwe ni mwaka ambao mwenye kupenda afya ya siasa ya Tanzania na awe wa kwanza kuanzisha vuguvugu la mabadiliko ya kweli ndani ya CDM.

Mkuu kwani Kuna sehemu umesikia Kuna mwanachadema yoyote anataka uenyekiti au kataka kugombea kakatazwa?

Katiba ya Cdm unaijua vizuri? Mbona Jk kawa mwenyekiti wa Ccm ten years,tatizo liko wapi mkuu
 
Mkuu kwani Kuna sehemu umesikia Kuna mwanachadema yoyote anataka uenyekiti au kataka kugombea kakatazwa?

Katiba ya Cdm unaijua vizuri? Mbona Jk kawa mwenyekiti wa Ccm ten years,tatizo liko wapi mkuu
Unafika wakati kwenye maisha ya kisiasa, kunakuwa na uhitaji wa damu changa. Naamini CDM wanao uhitaji huo, mtu atakayekuwa na mtazamo mpya wa kisiasa.
Unaweza kusema hakuna mwanacdm aliyekatazwa lakini chini kwa chini kuna ile hali ya aliyepo juu kutotaka waibuke vijana wapya.
 
Mkuu hapa mm sikuungi mkono, sijaona Kosa la Mbowe. Pili ,chama lazima kiwe na mtu mwenye uwezo mkubwa wa kuhimili mikiki ya CCM ,awe na pesa pia. Sasa unampa John Mnyika uenyekiti Si chama kitakufa??

Tufikirieni kiukubwa jamani. Zito anadaiwa sh ngapi sasahv na lichama lake?
 
Kumng'oa Mbowe ni kazi kubwa sana haswa kwa wakati huu anapoelekea kufilisika kibiashara,Mbowe hana kipato chochote zaidi ya kuwa mwenyekiti ili aendelee kuiibia chadema.
Msifanye mchezo atakufa mtu.
 
CDM ni mabingwa wa kujadili demokrasia kinadharia lakini wameshindwa kabisa kuonyesha kwa vitendo, mwenyekiti wa chama hawezi kukaa zaidi ya miaka 10 afu muendelee kuwa na ujasiri wa kuongelea demokrasia, shame on you!!
Pole sana inaonyesha bado mdogo sana. Nyerere alikuwapo tangu 1954 - 1990 akiwa M/kiti wa TANU-CCM. ili kukijenga chama. Na hata alipoachia hakuwa mbali na CCM na alikuwa remote ya CCM.
 
Mwaka 2004 ndipo Mkuu Freeman Mbowe alipochaguliwa kuwa mwenyekiti wa taifa wa CHADEMA.
Mtoto aliyezaliwa mwaka huo, mwaka huu anafanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi.

Kwa maneno mengine huu mwaka 2017 ni wa 13 wa uongozi wa Kaka Mbowe.
Taratibu siku zinasogea, ikifika January 2018 utakuwa ni mwaka wa 14 kwenye uongozi.

Unaposema JPM ni one man show inabidi pia uwe na ujasiri wa kusema CHADEMA ni one man party. CHADEMA inahitaji damu mpya, akili mpya, fikra mpya, na yote hayo kutoka kwa uongozi mpya.

Achana na habari kwamba siasa zimepigwa marufuku, maishani binadamu ili afanikiwe ni lazima awe na sifa ya kubadilika kutokana na wakati usiomsubiri mtu.

Wazungu husema adaptability, uwezo wa kufanana na mazingira yanayokuzunguka haswa jinsi yanavyobadilika.

Ifike mahali mwana CHADEMA mwenye kupenda mabadiliko awe tayari kujenga hoja kwenye mikutano ya ndani, juu ya umuhimu wa chama kupata visions mpya.
Uhai wa CHADEMA ndio uhai wa CUF na ndio uhai wa CCM, twende mbele turudi nyuma.

2017 uwe ni mwaka ambao mwenye kupenda afya ya siasa ya Tanzania na awe wa kwanza kuanzisha vuguvugu la mabadiliko ya kweli ndani ya CHADEMA.
Rais John Pombe Magufuli alizaliwa mwaka 1958, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa tayari ni Kiongozi wa TANU/CCM, nafasi aliyoishikilia hadi mwaka 1990 Magufuli akiwa na miaka 32, akikaribia umri wa mtu mzima maana ujana mwisho miaka 35. Tunajifunza nini katika hili kutoka CCM?

Cc MsemajiUkweli
 
Mkuu hapa mm sikuungi mkono, sijaona Kosa la Mbowe. Pili ,chama lazima kiwe na mtu mwenye uwezo mkubwa wa kuhimili mikiki ya CCM ,awe na pesa pia. Sasa unampa John Mnyika uenyekiti Si chama kitakufa??

Tufikirieni kiukubwa jamani. Zito anadaiwa sh ngapi sasahv na lichama lake?
Mkuu accused hiyo tabia ya kumtwisha mzigo mwenye pesa ndio sawa na mambo yale Yanga na Manji.

Manji akikohowa Yanga yote inaugua mafua. CDM inapoteza hadhi kwa kumtegemea mtu mmoja.
 
Rais John Pombe Magufuli alizaliwa mwaka 1958, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa tayari ni Kiongozi wa TANU/CCM, nafasi aliyoishikilia hadi mwaka 1990 Magufuli akiwa na miaka 32, akikaribia umri wa mtu mzima maana ujana mwisho miaka 35. Tunajifunza nini katika hili kutoka CCM?

Cc MsemajiUkweli
Mkuu CCM waliachana na taratibu hizo ndio maana kuanzia sasa mwenyekiti hata akiwa na kipaji cha kisiasa cha hali ya juu, ni lazima apishe akili mpya zije na mbinu mpya za kisiasa.
Mkuu Mchambuzi, unataka kuniambia kuwa Mbowe ndio Nyerere wa CHADEMA?.
 
Back
Top Bottom