Mtindo anaoondoka nayo Chongolo ni utamaduni mpya ndani ya CCM

1. Ni kwa mara ya kwanza nafasi ya Katibu mkuu wa chama inapiganiwa (Scramble) na makundi mbalimbali. Hapo kabla utamaduni huu haukuwepo, tulizoea mabadiliko yasiyo ya kimapambano jambo ambalo limeendelea kukipa chama chetu heshima na afya ya muunganiko kwa muda mrefu.
Mkuu Song of Solomon , kwanza asante sana kwa bandiko hili, ni muda mrefu humu sijawahi kukutana na bandiko very objective kihivi, asante sana for your objectivity kukisaidia CCM ni kulisaidia taifa
P
 
2. Kwa sasa Siri za Chama huenda zinaanza kuvuja. Kabla ya uteuzi wa Makonda kuwa mwenezi taarifa zilivuja siku mbili kabla na jambo hilo likaja kutokea kweli. Kama hili la katibu mkuu nalo litatokea ni dhahiri hatuko salama sana kwenye chama. Nani anavujisha hizi siri na kwa manufaa ya nani? Kesho zitavuja nyingine nzito zaidi na zitathibitika…. Tunakiua chama. Chama kinachounda Serikali lazima taarifa zake ziwe confidential kwa kuwa taarifa zake ni nyeti na ni taarifa ambazo huathiri hadi utendaji wa Serikali.
Naunga mkono hoja, hawa wavujisha siri ni kikulacho!, hili niliwahi kulizungumzia nakulilaani
View: https://youtu.be/-sr2_3bIHSo?si=3iwRwNFtW1nyylvn japo nilishutumiwa humu Pasco unaijua nguvu ya Twitter? hivyo naungana na wewe hawa kikulacho waliomo ndani ya chama, watafutwe!. Mtu wa kwanza kutafutwa awe ni mtu aliyevujisha barua ya Chongolo kujiuzulu!, hata kama ikitokea, ni hili ingizo jipya la Mama la huyu mtoto pendwa, chukua, weka pembeni, tupa kule!, hatufai!.

P
 
3. Zamani CCM ilikuwa si rahisi kupasuka kwa kuwa kulikuwa na chombo kilichoitwa baraza la wazee ambao kimsingi walikuwa wanaaminika na wanachama wote kwa kuwa walikuwa watenda haki na wasiokuwa na makundi ndani ya chama. Kwa sasa chombo hiki hakiaminiki tena na hakina kauli mbele ya vijana machachari waliopo ndani ya CCM. Katika mazingira kama haya Chama konakosa kundi muhimu sana la kutuliza mawimbi yayoweza kukipasua chama.
Kwanini hakiaminiki na hakina kauli?. Ina maana hao vijana machachari wana nguvu kuliko Baraza la Wazee?!, hizo nguvu wanapata wapi?. Juzi kati tumeshuhudia Waziri Mkuu wa JMT anakaripiwa na Dogo Janja!, anapewa ultimatum!, kuna Mzee yoyote wa chama umemsikia akikaripia?.
Kinyago tuchonge wenyewe halafu kinakuja kututisha wenyewe!, kosa ni la nani?, ni la vijana wanakimbiza chama mchaka mchaka au wazee walioshindwa kuonyesha relevance na kuwaleo vibaya vijana na sasa wamewaachia chama in their full control?.

P
 
4.Niliwahi kusema kuwa CCM haipo sayari nyingine. Magonjwa yaliyoviuua vyama vingine ambayo vina rika sawa nacho yanaweza kukiua CCM

Ukichunguza kwa makini kwa nn vyama hivi vilifurushwa madarakani utagundua ni mipasuko ya ndani.
Hapa natofautiana na wewe, CCM is still strong!. Wale ni wale na sisi ni sisi!. Kwa mahesabu yangu, CCM itaanza kutikisika 2030!. Uchaguzi mkuu wa mwaka 2030, ndio mwanzo wa mwisho wa CCM! Wajinga karibu wote watakuwa wamemalizika!
P
 
5.Historia Rasmi ya Rais Samia kuja kuliongoza taifa hili ilianzia mwaka 2015 pale ambapo aliyeteuliwa kugombea Urais Dr. Magufuli alipomchagua kuwa Mgombea Mwenza. Hata yeye binafsi nadhani alikuwa hajui kama muda mfupi ujao atakuwa Rais watanzania wote pia hawakujua kwamba ipo Siku ndani ya Muda Mfupi ujao Taifa hili litaongozwa na Mwanamke. Katika hili ni Mungu pekee aliyekuwa anajua nini kitatokea toka alipoteuliwa kuwa Mgombea mwenza na huo tunasema ulikuwa mpango wa Mungu ulikuwa wala sio Mpango wa CCM.
Historia ya Samia haikuanzia 2015, angalia bandiko hili ni la mwaka gani, hapa ndipo Samia alipoanzia!, ni 2010 na sio 2015!.

The same applies to urais wa Samia, hakuna mtu yoyote alijua kuwa kuna siku rais wa JMT anaweza kufa akiwa madarakani!, hivyo siku zote Makamo wa rais alikuwa anateuliwa tuu bila kumhesabia anaweza kuja kuwa rais wa JMT kwasababu hakuna aliyewahi kufikiri rais wetu anaweza kufa!.

Hivyo naamini hata wakati Samia ni Makamo wa JPM, hakuwahi kuwaza kuwa kuna siku JPM anaweza kuitwa kwa Baba yake na yeye kuwa rais wa JMT!, hivyo ilivyotokea JPM akaitwa Baba yake na Samia kawa rais, watu wote wanajua imetokea tuu, ni mipango ya Mungu, lakini hakuna watu wanaojua kumbe kuna watu, walitoa kauli zenye nguvu ya kuumba, waliomuomba Mungu, wakamuumbia urais wa JMT ili Samia awe rais na kweli Mungu akasikia hivyo kauli hizo zikamuumbia Samia urais, hivyo usikute hata Samia mwenyewe anajihesabu amekuwa rais wa JMT kwa kudra tuu za Mwenyeenzi Mungu, kumbe hajui sio kudra tuu, kuna watu waliomba, na wakapewa!.

Kwanza anza kuangalia ni lini watu walianza kumspot Mama Samia, mimi nilimspot 2010 New Cabinet: Baadhi ya Majina ni Haya Hapa!.
Wanabodi,
Bado niko hapa mjini Dodoma, nikijivinjari katika viwanja vya Bunge kwa haya na yale.

Japo mpaka sasa kitendawili cha Waziri Mkuu bado hakijatenguliwa, nimeonelea niwatajie baadhi ya majina mapya kwenye new cabinet.

2. Mwingine ni Samia Suluhu Hassan.
Huyu mama ni very powerful in Zanzibar na miongoni mwa wanawake wachache wa shoka kutoka Zanzibar. Ni Mjumbe wa CC na NEC wa CCM.
Very high profile woman from Zanzibar, baada ya kuhudumu kwa miaka 10 kwenye Baraza la Wawakilishi, sasa ameingia Bunge la JMT, atapewa important portfolio kumuandaa ama kuwa rais wa Zanzibar kisha kuja bara, au kuwa VP 2015.
Pasco
Bandiko hili ni la 2010, angalia hiyo 2010 tulisema nini kumhusu Samia, na nini kilikuja kutokea... mkiambiwa baadhi ya kauli zinaumba, mjue ni kweli kauli huumba!.

Kisha 2015 Siku ya Wanawake Duniani: Je, tuna Wanawake wenye sifa za Presidential Material?
Kauli Umba ya kuunda VP mwananke kwa Tanzania
Kufuatia kilio cha muda mrefu cha wanawake kunyimwa fursa, je ni kweli tunao wanawake wenye sifa na uwezo wa kutupeleka kwenye 50/50?. Hebu na tuanzie na wanawake wenye sifa za urais, je tunao?

Hebu tuwakumbuke the top ten female politicians in Tanzania, na nafasi wanazoshika! Je, wamefikaje hapo, kwa kupanda wenyewe, au wamebebwa ndipo wakafika hapo? Je, wana sifa za urais?
  1. Top No.1 ni Mhe. Samia Suluhu Hassan.
    Huyu mama ni very powerful in Zanzibar na miongoni mwa wanawake wachache wa shoka kutoka Zanzibar. Ni Mjumbe wa CC na NEC wa CCM.
    Very high profile woman from Zanzibar, baada ya kuhudumu kwa miaka 10 kwenye Baraza la Wawakilishi, ameingia Bunge la JMT for 5 years sasa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamo wa Rais. Ndiye alikuwa Makamo Mwenyekiti wa Bunge la Katiba. Huyu ni presidential material, sasa ni kumuandaa kwanza kuwa rais wa Zanzibar kwa kumpumzisha Dr. Shein kipindi chake cha pili, kisha 2020 aje urais wa Muungano, ili hili ifanyike, itabidi, CCM iachane na ule utaratibu wake wa two terms za urais, kwasababu kusubiria 2025, kwa huyu mama itakuwa too little too late, age itakuwa imemtupa mkono.
Natoa wito kwa wanawake, kama ni kweli mna uwezo, jitokezeni kwenye urais, ili hata msiposimamishwa, angalau 2015, tuwe na makamo rais mwanamke, au Waziri Mkuu Mwanamke!

Paskali.
Tanzania ilipata VP, mwanamke kwa mara ya kwanza, baada ya uchaguzi wa 2015, kuna wengi wanadhani ilijitokea tuu, Tanzania kuwa na VP mwanamke!, hawajui kuwa huo u VP wa mwanamke, kuna watu wenye kauli zenye powers za kuumba, walitoa kauli za kutaka tupate VP mwanamke, toka Machi 8, 2015!.

Then Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!”
kiukweli huyu ni mwanamke wa kupigiwa mfano, mtanisamehe sina maneno ya Kiswahili ya kujitosheleza kumuelezea, she is just so womanly, so genuine, so simple, very humble na down to earth!, ana a very rare charisma, which is very hard to find kwa viongozi wetu wengi wa kisasa.

She is just everything a woman needs to be!. Ingekuwa ni amri yangu ningetaka wanawake wenye uongozi, madaraka na mamlaka waige mfano wa Mwanamke huyu and to be honest I wish if Mungu angemua, huyu mama ndio akawa, then amini usiamini tutakuwa na Tanzania nzuri 100 times kuliko Tanzania hii tulionayo sasa!.

Ingekuwa ni amri yangu, ningemwambia tuu naniliu aamue 2020 asigombee his second term, na badala yake, ampishe ili awe huyu mama!.

Mungu ambariki sana Mama Samia na kuwabariki wanawake wote leo siku ya Wanawake Duniani.

Paskali
Hii ni kauli umba ya kumuumbia mtu urais wa JMT.

na hili "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza
Angalia kwa makini hii kauli umba hapa iliumba nini?
Makamo wa Rais wa JMT, Mhe. Samia Suluhu Hassan anauzungumzia Muungano, kiukweli huyu Mama Samia anauzumguza vizuri muungano huku akiongea kwa heshima, taratibu, kwa utulivu na unyenyekevu, na anaongea vizuri mpaka raha, na kwa wale wenzangu na mimi wenye udhaifu na macho fulani, kiukweli Mwenyenzi Mungu amemjaalia macho mashaalah, huchoki kumsikiliza, utatamani aendelee tuu kuongea na kipindi kisiishe!.

Kwa hoja za muungano Mama Samia alizoshusha, ningekuwa ni uwezo wangu, ningeshauri October 2020, Mama Samia ndiye ampokee Dr. Shein kule Zanzibar, ili 2025, aje ampokee Magufuli, maana kwa maoni yangu, kwa uongeaji huu, huyu mama ndiye Mzanzibari pekee anayekubalika kuweza kuchagulika kuwa rais wa JMT kutokea Zanzibar, vinginevyo Wazanzibari wausahau kabisa urais wa Muungano, wao mwisho wao ni umakamo wa rais pekee.

Kwa hoja kama hizi za huyu mama Samia, kama age sio issue sana, si huyu mama atatufaa sana 2025 au tuwashauri kwa vile Magufuli analamika sana kuhusu urais, mara ni mateso, mara ni kazi ngumu, mara ni mzigo mzito, tumshauri rais Magufuli, kwa vile Samia anatosha sana, hivyo tumpunguzie mateso, hana haja ya kuendelea na mateso, mzigo mzito na kazi ngumu ya urais, na hata kama ni wale tausi au wanyama wa Magogoni, au yale majabali ya Chamwino, tutamjengea Chato na kumuomba bora apumzike tuu mapema, na kumpisha Mama Samia ndio amalizie ngwe yake iliyobakia?.

Paskali
Hapa kuna mtu ameumbiwa urais wa JMT kwa kauli tuu!.

Naamini kama JPM angesoma hapa, halafu akaamua tangu ile ile ,2020 angempisha Samia, you never know by now labda...
P
 
Mwenyekiti na Rais wetu anatakiwa azungukwe na watu ambao ni very loyal na wenye nia ya dhati ya kumsaidia kushinda urais 2025 na si vinginevyo.
Hili linafanyika, sio umeona usajili mpya wa hivi karibuni unavyokimbiza watu mchakamchaka?, si umeshuhudia watu wanapelekewa moto, na kuwaunguza hadi wanaachia wenyewe?. Huu ndio mwendo mdundo hadi 2025, ila mimi msimamo wangu binafsi kwa 2025 kwanza ni Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye! ila pia kuna hizi sauti Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke sio za kuzipuuzwa!.
P
 
8. Unazaliwa utamaduni mpya ndani ya Chama kuwa mtu akitaka cheo fulan ndani ya Chama basi watamchafua aliyepo kwenye nafasi hiyo. Kwa utamaduni huu chama hakitakaa kitulie daima. Hili ni la Kuzuia lisitokee kabisa.

9. Kama Mwenyekiti ataridhia kujiuzulu kwa SG Chongolo basi kundi lililohusika kumwondoa madarakani lisitoe mrithi wake. Mrithi wa SG anatakiwa mtu anayetokea nje ya makundi ya Urais, mtu mwaminifu na
Naunga mkono hoja
P
 
Tuache waendelee kuuana, kuchafuana na kuraruana, wakishamalizana itakuwa poa.

Jiwe alishaenda kiutata....
Membe alishaenda kiutata.....
Atafuata nani?
 
Back
Top Bottom