MTIKISIKO: Vifaa vyote vya tiba vinavyoingizwa nchini sasa kukatwa kodi, dawa zote sasa kulipiwa

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,596
36,018
Nchi yetu inaweza kujikuta kwenye sintofahamu kubwa siku zijazo kama mambo yataenda kama ilivyopangwa, imefahamika.

Sasa vifaa tiba vyote ambavyo enzi za tawala zote zilizopita vilikuwa vikiingizwa nchini kutokea nje bila kukatwa kodi, hatimaye vitakatwa kodi. Aidha kumbukwe kuwa serikali kupitia MSD tayari kwa miaka miwili kuanzia sasa itakuwa ikiagiza dawa zote muhimu kutoka India na China hivyo kupeleka maumivu makali kwa wananchi.

Katika hatua nyingine ni kuwa sasa dawa zote zitakazopatikana hospitali za ndani zitakuwa zikilipiwa (baadhi hazitatolewa tena bure) huku hospitali ya Muhimbili tayari ikiwa imeanza zoezi hilo.

Ikiwa vifaa tiba vyote vinavyoagizwa nje vitaanza kukatwa kodi, hali itakuwa mbaya zaidi kwa wananchi wa kawaida ambao ndiyo hasa wenye mzigo. Aidha tayari pendekezo hilo limetolewa.
 
Kwanini dawa ziwekewe masharti ya kuagizwa India na China?

Tunaweza kuagiza ulaya au Uarubuni ambako kuna viwango vya juu tu

Tunajua India na utapeli, na serikali sasa inawapa mwanya

Kuna sehemu nyingi sana tunaweza ku source dawa Kenya, Egypt , Uropa , middle east na zina viwango vizuri sana

Hili la kuwasukuma MSD kununua Dawa za INDIA ambazo hata mitaani wananchi wanazitilia shaka nadhani lina mkono wa mtu na mikono ya watu!

Matter of time mtakujasikia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…