SoC01 Mtanzania yeyote, hata asiye na Elimu ni muhimu ajifunze lugha ya Kiingereza

Stories of Change - 2021 Competition

hustler Tz

Member
Mar 16, 2018
8
22
Habari zenu wanajukwaa la Story of change.
Katika uzi huu nataka kuelezea ulazima wa kujifunza lugha ya kiingereza kwa mtanzania hata asie na elimu kubwa. Hili suala huwa haliongelewi kabisa na kumekuwa na upotoshaji mkubwa sana kuhusu lugha ya kiingereza.

JE, HUO UPOTOSHAJI UPOJE?

Hapa nchini Tanzania, hasa miaka ya hivi karibuni kumekuwa na upotoshaji mkubwa kuhusu lugha ya kiingereza. Hasa viongozi wakubwa serikalini ndio wamekuwa wahusika wa hili. Watanzania wameaminishwa kuwa lugha ya kiingereza ni ukoloni na kujifunza lugha hiyo si uzalendo na hata kuna kiongozi mmoja aliwahi kusema kuwa "hata mwanafunzi akimaliza form four na hajui kiingereza ni sawa kabisa kwani hatukwenda kumfundisha kiingereza bali tumeenda kumpa elimu" . Sasa swali ni kwamba, elimu gani hiyo aliopata wakati lugha ya kufundishia haijui??

Lugha ya kiinereza kwa sasa haihusiani tena na ukoloni bali ni njia kuu ya kuwaunganisha watu duniani kote. Lugha ya kiingereza inatumika katika biashara na kijamii pia. Mitandao karibia yote ya kijamii inatumia lugha ya kiingereza.

KWANINI KIINGEREZA SI UKOLONI KWASASA?

Kwa karne ya sasa ukisema kuwa kujifunza kiingereza ni ukoloni basi wewe utakuwa hujui hata dunia inaendaje kwasasa. Lugha ya kiingereza ndio Lugha kubwa na iliosambaa zaidi duniani.

Nchi kubwa na zenye ushawishi duniani kama Marekani, Uingereza, Canada, Australia na Afrika kusini zinatumia lugha ya kiingereza. Pia nchi nyingi za Afrika zinatumia lugha ya kiingereza.

Lugha ya kiingereza si ukoloni bali ni nafasi ya kuiunganisha dunia kwa lugha moja.

JE, TOFAUTI YA MTANZANIA ANAEJUA KIINGEREZA NA ASIEJUA KIINGEREZA NI IPI?

Mtanzania anaejua kiingereza anakuwa na upeo mkubwa wa kujua mambo mengi duniani ukilinganisha na yule asiejua. Hapa haijalishi elimu yao.

Mtanzania anaejua kiingereza anakuwa na akili iliyopevuka katika kuchambua mambo mengi zaidi. Mtu asiejua kiingereza hataweza kamwe kuendana na kasi ya dunia kwa sasa (Teknolojia).

USHAURI KWA SERIKALI

Serikali inatakiwa kuanzisha program mbalimbali za kuhamasisha watu kujifunza kiingereza ili kuwasaidia kuendana na kasi ya dunia ya kimaendeleo na teknolojia.

Kuna mambo mengi sana ya muhimu ya kujifunza kwenye mitandao lakini kwakua mengi yameandikwa kwa kiingereza na watu wengi hawajui kiingereza basi watu wengi huishia kufanya mambo yasiyo na manufaa yoyote.

Chaguo ni kujifunza kiingereza au kukubali kuishi katika zama za mawe ndani ya karne ya 21.

Nawasilisha.

images (16).jpeg
 
Hii ni kweli, huku ninakoishi ninaona wanayopitia wamama wa kitanzania waliokuja kuishi na watoto/ndugu zao. Wakati wenzao wa jamii za Kenya, Ghana, Nigeria nk nk wako bize wanapiga hela, wao wanakaa tuu nyumbani kikwazo kikubwa kikiwa ni lugha. Kuna fursa nyingi sana kwa mtu kujua ligha ya Kingereza maana haujui miaka 5, 10 au 20 utakuja kuwa wapi.
 
Ni kweli kabisa..umetoa mfano hai kabisa. Nilishawahi kukutana na mama mmoja akaniambia ameshindwa kufanya biashara zake kimataifa kwakua hajui kiingereza japo ana ujuzi mzuri tu wa hizo bidhaa.
 
Habari zenu wanajukwaa la Story of change.
Katika uzi huu nataka kuelezea ulazima wa kujifunza lugha ya kiingereza kwa mtanzania hata asie na elimu kubwa. Hili suala huwa haliongelewi kabisa na kumekuwa na upotoshaji mkubwa sana kuhusu lugha ya kiingereza.

JE, HUO UPOTOSHAJI UPOJE ?

Hapa nchini Tanzania, hasa miaka ya hivi karibuni kumekuwa na upotoshaji mkubwa kuhusu lugha ya kiingereza. Hasa viongozi wakubwa serikalini ndio wamekuwa wahusika wa hili. Watanzania wameaminishwa kuwa lugha ya kiingereza ni ukoloni na kujifunza lugha hiyo si uzalendo na hata kuna kiongozi mmoja aliwahi kusema kuwa "hata mwanafunzi akimaliza form four na hajui kiingereza ni sawa kabisa kwani hatukwenda kumfundisha kiingereza bali tumeenda kumpa elimu" . Sasa swali ni kwamba, elimu gani hiyo aliopata wakati lugha ya kufundishia haijui??

Lugha ya kiinereza kwa sasa haihusiani tena na ukoloni bali ni njia kuu ya kuwaunganisha watu duniani kote. Lugha ya kiingereza inatumika katika biashara na kijamii pia. Mitandao karibia yote ya kijamii inatumia lugha ya kiingereza.

KWANINI KIINGEREZA SI UKOLONI KWASASA?

Kwa karne ya sasa ukisema kuwa kujifunza kiingereza ni ukoloni basi wewe utakuwa hujui hata dunia inaendaje kwasasa. Lugha ya kiingereza ndio Lugha kubwa na iliosambaa zaidi duniani.

Nchi kubwa na zenye ushawishi duniani kama Marekani, Uingereza, Canada, Australia na Afrika kusini zinatumia lugha ya kiingereza. Pia nchi nyingi za Afrika zinatumia lugha ya kiingereza.

Lugha ya kiingereza si ukoloni bali ni nafasi ya kuiunganisha dunia kwa lugha moja.

JE, TOFAUTI YA MTANZANIA ANAEJUA KIINGEREZA NA ASIEJUA KIINGEREZA NI IPI?

Mtanzania anaejua kiingereza anakuwa na upeo mkubwa wa kujua mambo mengi duniani ukilinganisha na yule asiejua. Hapa haijalishi elimu yao.

Mtanzania anaejua kiingereza anakuwa na akili iliyopevuka katika kuchambua mambo mengi zaidi. Mtu asiejua kiingereza hataweza kamwe kuendana na kasi ya dunia kwa sasa (Teknolojia).

USHAURI KWA SERIKALI

Serikali inatakiwa kuanzisha program mbalimbali za kuhamasisha watu kujifunza kiingereza ili kuwasaidia kuendana na kasi ya dunia ya kimaendeleo na teknolojia.

Kuna mambo mengi sana ya muhimu ya kujifunza kwenye mitandao lakini kwakua mengi yameandikwa kwa kiingereza na watu wengi hawajui kiingereza basi watu wengi huishia kufanya mambo yasiyo na manufaa yoyote.

Chaguo ni kujifunza kiingereza au kukubali kuishi katika zama za mawe ndani ya karne ya 21.

Nawasilisha.

View attachment 1856433
Uko sahihi mkuu 100%.Dhana kwamba Kingereza sio muhimu imeibuka miaka ya hivi karibuni.Ukichunguza kwa makini trend hii utagundua kwamba tatizo hili limekwenda sambamba na kipendi ambacho elimu yetu imeharibika sana kwa sababu mbali mbali,lakini sababu kubwa ikiwa ulegezaji wa masharti ya kuweza kupata elimu bora.

Kwa mfano adoption ya UPE(Universal Primary Education) na kuruhusu waalimu wa UPE wawe waalimu.Mtoto aliyefeli Std VII atafundishaje,ni mjinga tu anayeweza kuamini kwamba that is possible.

Kumekuwa pia na mitaala ya hovyo hovyo tu isiyo kidhi kabisa haja ya kuweza kuwapatia watoto wetu elimu bora. Kwa mfano ubadilishwaji wa mitaala kila wakati na hivyo kuharibu kabisa continuity na kukosa consolidation.Kumekuwa pia na Waalimu wasio na weledi wa kuwa waalimu,kwa mfano waalimu waliopewa jina la Vodafasta.Kijana kafeli flat Form IV,kakaa kijiweni 3yrs,anapelekwa Chuo kwa mwaka mmoja halafu eti anakuwa mwalimu!It's ridiculous,na huyu anaambiwa akafundishe Kingereza! Hawezi huyu.

Ipo issue nyingine iliyopenyezwa kiaina na Watanzania tumeikubali kabisa,but it is wrong,na inatupatia wataalamu wasio na ufanisi.Mtu kafeli,halafu anarudia darasa au kafeli Form IV au Form VI,halafu ana-resit.Hawezi shule huyu,atafute shuhuli nyingine ya kufanya, mafanikio sio kwenye elimu tu.

Halafu lipo swala la vyeti fake.Hili nalo limetuharibia sana.Mtu aliyepata elimu kwa ku-forge vyeti ni incompetent, hawezi kuwa na weledi.Hata hivyo katika hali ya kushangaza tulivamiwa na wimbi la vihiyo wa vyeti fake tukachukulia poa tu.Sasa mtu wa hivi akiwa mwalimu wa Kingereza unategemea nini,si atatupatia mhitimu kihiyo wa Kingereza.

Kwa bahati mbaya sasa watu hawa walipanda kwenye system wakawa decision makers.Tungetegemea nini hapo, kwa kuwa wenyewe Kingereza chao ni cha Ras Simbaa,lazima wata down play umuhimu wa Kingereza,lakini sio kweli,Kingereza na Kiswahili vyote ni muhimu,Tanzania sio kisiwa kwa hiyo ni lazima lugha zote mbili zitiliwe mkazo.

Sijui Watanzania nani katuloga.Sisi wengine tunaamini kabisa(na ni kweli)kwamba upo mpango wa maadui zetu kuharibu elimu yetu ,ili tuendelee kuwa tegemea kwao for technologies na kwenye negotiations mbali mbali watuingize mkenge kiulani.
 
Hongera sana kwa maoni mazuri. Watu wameaminishwa ujinga kuwa kiingereza ni ukoloni..
 
Habari zenu wanajukwaa la Story of change.
Katika uzi huu nataka kuelezea ulazima wa kujifunza lugha ya kiingereza kwa mtanzania hata asie na elimu kubwa. Hili suala huwa haliongelewi kabisa na kumekuwa na upotoshaji mkubwa sana kuhusu lugha ya kiingereza.

JE, HUO UPOTOSHAJI UPOJE ?

Hapa nchini Tanzania, hasa miaka ya hivi karibuni kumekuwa na upotoshaji mkubwa kuhusu lugha ya kiingereza. Hasa viongozi wakubwa serikalini ndio wamekuwa wahusika wa hili. Watanzania wameaminishwa kuwa lugha ya kiingereza ni ukoloni na kujifunza lugha hiyo si uzalendo na hata kuna kiongozi mmoja aliwahi kusema kuwa "hata mwanafunzi akimaliza form four na hajui kiingereza ni sawa kabisa kwani hatukwenda kumfundisha kiingereza bali tumeenda kumpa elimu" . Sasa swali ni kwamba, elimu gani hiyo aliopata wakati lugha ya kufundishia haijui??

Lugha ya kiinereza kwa sasa haihusiani tena na ukoloni bali ni njia kuu ya kuwaunganisha watu duniani kote. Lugha ya kiingereza inatumika katika biashara na kijamii pia. Mitandao karibia yote ya kijamii inatumia lugha ya kiingereza.

KWANINI KIINGEREZA SI UKOLONI KWASASA?

Kwa karne ya sasa ukisema kuwa kujifunza kiingereza ni ukoloni basi wewe utakuwa hujui hata dunia inaendaje kwasasa. Lugha ya kiingereza ndio Lugha kubwa na iliosambaa zaidi duniani.

Nchi kubwa na zenye ushawishi duniani kama Marekani, Uingereza, Canada, Australia na Afrika kusini zinatumia lugha ya kiingereza. Pia nchi nyingi za Afrika zinatumia lugha ya kiingereza.

Lugha ya kiingereza si ukoloni bali ni nafasi ya kuiunganisha dunia kwa lugha moja.

JE, TOFAUTI YA MTANZANIA ANAEJUA KIINGEREZA NA ASIEJUA KIINGEREZA NI IPI?

Mtanzania anaejua kiingereza anakuwa na upeo mkubwa wa kujua mambo mengi duniani ukilinganisha na yule asiejua. Hapa haijalishi elimu yao.

Mtanzania anaejua kiingereza anakuwa na akili iliyopevuka katika kuchambua mambo mengi zaidi. Mtu asiejua kiingereza hataweza kamwe kuendana na kasi ya dunia kwa sasa (Teknolojia).

USHAURI KWA SERIKALI

Serikali inatakiwa kuanzisha program mbalimbali za kuhamasisha watu kujifunza kiingereza ili kuwasaidia kuendana na kasi ya dunia ya kimaendeleo na teknolojia.

Kuna mambo mengi sana ya muhimu ya kujifunza kwenye mitandao lakini kwakua mengi yameandikwa kwa kiingereza na watu wengi hawajui kiingereza basi watu wengi huishia kufanya mambo yasiyo na manufaa yoyote.

Chaguo ni kujifunza kiingereza au kukubali kuishi katika zama za mawe ndani ya karne ya 21.

Nawasilisha.

View attachment 1856433
Umeongea pointi sana kijana!
 
Mkuu hata mwigulu anajua ki-english lakini upeo wake n hamna kitu.....sio wote wenye upeo mkubwa wanajua ki-english and vice versa.
 
kafeli Form IV au Form VI,halafu ana-resit.Hawezi shule huyu,
Hapa nakupinga mkuu kwa sababu zifuatazo.

Kuna watu wanafeli kwa sababu mbalimbali.

1.hajahudhuria vipindi lakini angelihudhuria angelielewa vizuri tu na angefaulu.

2.kuna watu wanafeli kwa sababu waliyoyasoma hayakutoka kwenye mtihani.

3.wanafeli kwa sababu ya kusahau.

4.wanafeli kwa uzembe.

5.wanasoma lakini hawaelewi.

Makundi hayo matano yoote basi kila kundi tunatakiwa tulipe nafasi ya kurwkebisha mapungufu ambayo yalimfanya mwanzo afeli.

Elimu haina maana kwamba upate watu ambao watafanya kila jambo kwa usahihi kwa pamoja.

Kufeli ni katika kusoma ndio maana hata vyuoni kuna SUP kukupa nafasi ya wewe kufanya tena mtihani ukiwa below ya marks husika na huu ni mfumo upo hata katika Nchi ambazo pengine unaona mfumo wao wa elimu ni mzuri.

Hivyo kule shule kule kurisiti ndio kama sup ya chuo tu,sasa ukisema hii kurisiti isiwepo basi na sup isiwepo pia kwa sababu hizi zote zinampa mwanafunzi fursa ya kufanya mtihani baada ya ule wa mwanzo kufeli.

Hivyo kwa hiyo point naona sio sawa kukataza watu kurisiti.
Halafu lipo swala la vyeti fake.Hili nalo limetuharibia sana.Mtu aliyepata elimu kwa ku-forge vyeti ni incompetent, hawezi kuwa na weledi.Hata hivyo katika hali ya kushangaza tulivamiwa na wimbi la vihiyo wa vyeti fake tukachukulia poa tu.Sasa mtu wa hivi akiwa mwalimu wa Kingereza unategemea nini,si atatupatia mhitimu kihiyo wa Kingereza.
Anaweza akawa hayupo competent katika kuwa na cheti original lakini akawa yupo competent katika fani hiyo.

Nina jamaa yangu alifoji cheti ile fukuza ya magufuli ikamuondoa,sasa hivi yuko private sector fulani anaoiga kazi kama ana cheti original.

Hivyo pia tofautisha kati ya cheti feki na ujuzi,unaweza kuwa na cheti feki lakini ujuzi ukawa halisi.

Maoni yangu mtu akikutwa na cheti feki aangaliwe kama anaweza vizuri kazi ya yenye professional ya cheti chake basi aambiwe akatafute cheti original ili tusimkose mtu huyo ati kwa sababu ya cheti ambacho kimsingi hakifanyi kazi.
 
Hapa nakupinga mkuu kwa sababu zifuatazo.

Kuna watu wanafeli kwa sababu mbalimbali.

1.hajahudhuria vipindi lakini angelihudhuria angelielewa vizuri tu na angefaulu.

2.kuna watu wanafeli kwa sababu waliyoyasoma hayakutoka kwenye mtihani.

3.wanafeli kwa sababu ya kusahau.

4.wanafeli kwa uzembe.

5.wanasoma lakini hawaelewi.

Makundi hayo matano yoote basi kila kundi tunatakiwa tulipe nafasi ya kurwkebisha mapungufu ambayo yalimfanya mwanzo afeli.

Elimu haina maana kwamba upate watu ambao watafanya kila jambo kwa usahihi kwa pamoja.

Kufeli ni katika kusoma ndio maana hata vyuoni kuna SUP kukupa nafasi ya wewe kufanya tena mtihani ukiwa below ya marks husika na huu ni mfumo upo hata katika Nchi ambazo pengine unaona mfumo wao wa elimu ni mzuri.

Hivyo kule shule kule kurisiti ndio kama sup ya chuo tu,sasa ukisema hii kurisiti isiwepo basi na sup isiwepo pia kwa sababu hizi zote zinampa mwanafunzi fursa ya kufanya mtihani baada ya ule wa mwanzo kufeli.

Hivyo kwa hiyo point naona sio sawa kukataza watu kurisiti.

Anaweza akawa hayupo competent katika kuwa na cheti original lakini akawa yupo competent katika fani hiyo.

Nina jamaa yangu alifoji cheti ile fukuza ya magufuli ikamuondoa,sasa hivi yuko private sector fulani anaoiga kazi kama ana cheti original.

Hivyo pia tofautisha kati ya cheti feki na ujuzi,unaweza kuwa na cheti feki lakini ujuzi ukawa halisi.

Maoni yangu mtu akikutwa na cheti feki aangaliwe kama anaweza vizuri kazi ya yenye professional ya cheti chake basi aambiwe akatafute cheti original ili tusimkose mtu huyo ati kwa sababu ya cheti ambacho kimsingi hakifanyi kazi.
Unatetea kisichoweza kutetewa mkuu.Sababu zote ulizotoa ni za watu ambao IQ yao ni ndogo.Mkuu ni hivii,ukishakuwa John wa kufeli feli,huwezi shule na hii ina maana hata kazi inayohitaji shule hutaweza, katafute shuhuli nyingine ufanye sio lazima shule.Hata ukiwa kazini kuna shule mkuu,sasa kama wewe wa kufeli feli utakuwaje.Nadhani unatetea kwa kuwa na wewe ni wa kufeli feli!
 
Unatetea kisichoweza kutetewa mkuu.Ukishakuwa John wa kufeli feli,huwezi shule katafute shuhuli nyingine ufanye sio lazima shule.Hata ukiwa kazini kuna shule,sasa kama wewe wa kufeli feli itakuwaje.Nadhani unatetea kwa kuwa na wewe ni wa kufeli feli.
Ndio mkuu nilifeli,na nikarudia nikawa best kuliko wale ambao walifaulu.

Na hiyo ni kutokana kwamba mtu kufeli sio sababu kwamba ni kilaza,kuna sababu nyingi sana.

Hivyo nimetoa hoja nataka ijibiwe kwa hoja sio kuniletea lawama.
 
Sawa,wewe unaweza kuwa an exception,na these are few cases and we cannot work on exceptions,ni ujinga.Mkuu the majority of failures ni vilaza,anaye-deny hili ana personal reasons.
 
Exception lazima izingatiwe,huwezi jua huyu exception mmoja atakuja kufanya mapinduzi gani kwenye tasnia husika.

Kuweka mfumo ambao utawasapoti exception ni muhimu,muhimu kuweko na mazingira ambayo huo uchache wao hautaleta hasara katika mfumo huo.

Yaani mtu akiamua kurudia mtihani basi alipie kama ilivyo sasa na kama hajaamua iwe kataka yeye kutokurudia.

Na yapo mambo ambayo wafanyaji ni wachache lakini bado yametizamwa kwa upana wake.

Mfano ipo mifumo maalumu ya kuwafundisha viziwi japokuwa ni wachache lakini wamejaliwa.

Ipo mifumo ya kuwafundisha kusoma na kuandika watu ambao ni vipofu japokuwa ni wachache ukilinganisha na watu wazima wa viungo hivyo.

Kwa mantiki hiyo waendelee kuweka mazingira rafiki ya kuwaruhusu waliofeli kurudia mtihani kama vile ilivyokuwa sup ya chuo tu.
 
Back
Top Bottom