Mtanzania mwingine aliyeenda kufanya kazi akutwa amefariki Oman. Familia yaomba Ubalozi wa Tanzania ufuatilie

Mindyou

JF-Expert Member
Sep 2, 2024
1,715
4,455
Wakuu,

Mtanzania Asha Makame Ally, aliyeelekea nchini Oman kupambania ndoto zake, amepatikana akiwa amefariki dunia nchini humo, ndani ya nyumba aliyokuwa akiishi, huku mwili wake ukigundulika siku nne baada ya kifo chake.

Mwili wa Asha upo hospitalini nchini humo, lakini kuna changamoto kubwa katika kuruhusu mwili huo kuzikwa.

Kwa mujibu wa kaka yake, Rajabu Makame Ally, ametoa ushauri kwa Watanzania wengine wenye mpango wa kwenda nje ya nchi kuhakikisha wanafuata utaratibu, kupata vibali, na kufanya kazi walizoziendea.

Rajabu ameongeza kwa kuiomba serikali na balozi za Tanzania nchini Oman kufuatilia suala la mdogo wake, ili aweze kuzikwa nchini humo kutokana na hali ya mwili wake kuharibika.

Asha ni mzaliwa wa Jang'ombe visiwani Zanzibar.

 
Proud tobe a Muslim.
IMG_0625.jpeg
 
Back
Top Bottom