Mtanganyika ni nani?

Umeenda Zanzibar au hadith tu za simulizi. Mbona wapo Wabara wengi wanaishi na wamewekeza Zanzibar. Wapo Wangazija, wahindi, Wachina, Wazungu wewe unabakia kulia tu. Hizi Siasa za kutafuta mchawi zinawapotosha sana, nenda kawekeze Zanzibar na utaishi kama Mzanzibar. Nina jamaa zangu wanaishi Zanzibar na sijasikia wakilalamika.
Unalozungumzia ni historical. Zanzibar ni nchi ya wahamiaji lakini baada ya Muungano, watanganyika waliohamia waliwekewa vizuizi katika kutambuliwa kama wazanzibari na hivyo kunyimwa baadhi ya haki za uraia ( kumiliki ardhi ikiwa mojawapo)ambao raia wa Zanzibar walikuwa nazo. Kuna wakati hata kuoa binti wa kizanzibari ilikuwa shida. Hata katika ajira mtanganyika anahesabiwa kama mgeni.

Amandla...
 
Mimi naona kama unachanganya mambo. Hakuna nchi duniani ambayo ilikuwa na mipaka ya asili. Mipaka yote ni artificial na ilibuniwa na wajanja katika juhudi za kutawala watu wenye tofauti za kijamii. Mara nyingi hii ilifanyika kwa vita, ndoa au kuwarubuni watu waliowakuta. Wazungu walipoenda Marekani walikuta kuna makabila tofauti yanaishi huko. Kwa hila, mauaji ubabe na dhulma ndio wakabuni hiyo nchi inayojulikana kama USA. Pamoja na kulazimisha hivyo, palikuwa na jaribio la kujitenga. Na mpaka sasa bado linaweza kuongezeka kama Puerto Rico itaomba kuwa jimbo la Marekani. UK hivyo hivyo, ni upanga na dhulma dhidi ya wascot na wengine ndio hiyo mipaka iliundwa na mpaka leo ni tusi kubwa kumuita mscot muingereza. Spain hivyo hivyo ( wacatalonia mpaka kesho hawataki kuitwa waspanish).

Hapa kwetu kama ilivyokuwa katika sehemu kubwa ya Africa mipaka na mgawanyiko wa continent yetu katika sehemu za utawala tunaouita nchi ulifanyika Berlin ambako hatukualikwa na hatukuwa na uwakilishi. Mkutano huo ndio uliozaa German East Africa. Zoezi la kuweka mipaka kati ya himaya ya Ujerumani, Ureno na Uingereza lilikatishwa na vita kuu ya pili. Mtu unaweza kusema wajerumani ndio waliwalazimisha watu wote waliokuwa wanaishi katika himaya yake kuanza kujitambua kama wamoja, kama subjects wa Kaiser wa Ujerumani. Juhudi hizi zilipingwa sana na wakazi wa maeneo hayo.

Baada ya mjerumani kushindwa himaya yake iliyokuwa Afrika Mashiriki ikagawiwa kwa wabelgiji na waingereza. Muingereza akaipa jina la Tanganyika eneo lake. Na watu waliokuwa wakiishi humo wakajitambua kama watanganyika. Hili jina na identity hii iliendelea hata baada ya uhuru wake mpaka siku ilipoungana na Zanzibar. Kwa sasa hamna nchi inayoitwa Tanganyika. Lakini kutokuwepo kwa nchi inayoitwa Tanganyika katika ramani hakuwanyimi watu ambao asili yao ilikuwa ni katika eneo hilo kujitambua kama Tanganyika. Hao ndio watanganyika wa sasa. Wanaofanya hivyo bado wanaamini kuwa iko siku hilo eneo litatambuliwa tena kwa Tanganyika. Hamna mtu anayeweza kuwakataza kuwa na ndoto hiyo. Vilevile kuna wale ambao jina Tanganyika halina maana kwao, na wanajitambua zaidi kama watanzania. Hao nao hiyo ni haki yao.

Amandla...
Mkuu sijachanganya kitu isipokuwa nawamsha Wadangantika mjue kuwa nyie ni kitu kimoja mligawanywa pasipo hiari yenu. African Association ilianzishwa na Waafrika wa Bara na Visiwani na hata kablanya ASP haijaungana mwaka 1957 mwl. Nyerere alienda Zanzibar akitaka vyama vyote vya waafrika waunganishe nguvu dhidi ya ZNP. Na hata Upande wa TANU baadhi viongozi na Masheikh wa Zanzibar walikuwa wakisbiriki baadhi ya vikao vya Chama.

We came the long way together isipokuwa tuligawanywa. Na Tanganyika waisemayo isingepata Uhuru kama wangedai Zanzibar ni sehemu ya nchi moja maana Pwani yote ya Bara ilikuwa sehemu ya Utawala wa Sultan Said bin Sultan. Infact alikuwa na Mawalii hadi bara na wakiheshimiwa.

Kwa hiyo, nasema hakuna kitu Mtanganyika wala Mzanzibar, zinaweza kuwepo nchi kama Dar, Mwanza, Dodoma, Tabora, Ubguja, Pemba lakini sote ni watu wale wale.
 
Kwa hiyo unacholilia ni jina? Ok tunakuita Bara umepungua nini?viiongozi? Maana ukisema Serikali maana yake unataka viongozi ilihali Serikali ya JMT inafanya kazi zile zile.

Wenzenu huko Ulaya mpaka Wahindi wanaongoza nyie mnakalia Utanganyika. Afrika kazi kugombania urithi matokeo mnakosa wote. Toka familia zetu hadi nchi ni ugonvi wa mirathi ya ardhi.

Itazame Sudan, Ethiopia, Somalia, DRC ni ujinga tu wa kugombania mali ati hizi zangu! Wako wapi? Miaka nenda ni vita!

Jengeni UMOJA WENU kuikomboa Afrika Kiuchumi sio kugombania mali. Kutwa kupigania mali, hata Mkipewa Urithi mnauza kwa Wageni mnarudi katika umaskini. itazame Kariakoo!
Mkataa kwao ni mtumwa, ona mnaongozwa na Wanzibar na wanaimega nchi ya Tanganyika, Wakati Mbara kamwe hata awe rais hana mamlaka kuimega Zanzibar
 
Ndugu zangu, Mwalimu Nyerere siintu alituasa bali ametuachia tunu kubwa ya Utaifa wetu kuwa nchi hii inaitwa Tanzania. Ni jina walochagua waasisi wetu na wakaamua wenyewe kuunganisha nchi zetu mbili kama ilivyo asili ya ndoa zetu tukazaliwa sisi. Hatuwezi badilisha Ubini wetu kwa sababu ya urithi wa mali.
Mzimu huo acha tuchague cha kufanya wenyewe ambao bado tupo hai.
 
Unalozungumzia ni historical. Zanzibar ni nchi ya wahamiaji lakini baada ya Muungano, watanganyika waliohamia waliwekewa vizuizi katika kutambuliwa kama wazanzibari na hivyo kunyimwa baadhi ya haki za uraia ( kumiliki ardhi ikiwa mojawapo)ambao raia wa Zanzibar walikuwa nazo. Kuna wakati hata kuoa binti wa kizanzibari ilikuwa shida. Hata katika ajira mtanganyika anahesabiwa kama mgeni.

Amandla...
Yamepitwa na wakati mkuu tulikuwa tukienda Zanzibar na Passport, leo hii huendi nayo. Anaweza mtu kusema unatakiwa kubeba Passport na ukaamini. Hofu ya Zanzibar ni Population ambayo hata katika mipango miji tunazingatia. Sasa mbona Bara inawakataa Diaspora wanaoishi nje? Je hao sio Watanganyika? Tatizo letu sisi Waafrika ni MALI. Yaani mtu anaona huyu mweusi mwenzangu akija atachukua changu basi! Uchoyo, inda, roho mbaya na unafiki. Lakini aje Mzungu, Mchina au Mwarabu atapokelewa na ardhi atapewa ati mwekezaji. Kajenga nini Hotel! anakula hela yenu wenyewe! Inferiority complex inatumaliza
 
Mzimu huo acha tuchague cha kufanya wenyewe ambao bado tupo hai.
Huwezi chagua wazazi - Baba na Mama yako wameshakupa jina lako. Ukitaka jina la Babu huyo ni mzungu mshenzi unayemchukia sana alimtesa bibi yako. Unalitaka jina hilo ili uonekane na wewe mzungu au?
 
Mkuu sijachanganya kitu isipokuwa nawamsha Wadangantika mjue kuwa nyie ni kitu kimoja mligawanywa pasipo hiari yenu. African Association ilianzishwa na Waafrika wa Bara na Visiwani na hata kablanya ASP haijaungana mwaka 1957 mwl. Nyerere alienda Zanzibar akitaka vyama vyote vya waafrika waunganishe nguvu dhidi ya ZNP. Na hata Upande wa TANU baadhi viongozi na Masheikh wa Zanzibar walikuwa wakisbiriki baadhi ya vikao vya Chama.

We came the long way together isipokuwa tuligawanywa. Na Tanganyika waisemayo isingepata Uhuru kama wangedai Zanzibar ni sehemu ya nchi moja maana Pwani yote ya Bara ilikuwa sehemu ya Utawala wa Sultan Said bin Sultan. Infact alikuwa na Mawalii hadi bara na wakiheshimiwa.

Kwa hiyo, nasema hakuna kitu Mtanganyika wala Mzanzibar, zinaweza kuwepo nchi kama Dar, Mwanza, Dodoma, Tabora, Ubguja, Pemba lakini sote ni watu wale wale.
Sidhani kama Seyyid Said aliwahi kutawala pwani yote ya Bara. Alikuwa na makubaliano na baadhi ya city states kama Kilwa, Malindi, Mikindani n.k. Hakuna chief yeyote wa makabila ya pwani aliyemhesabu Sultan kama mtawala wake na hivyo kumpelekea mapato. Kuheshimiwa kwa hao mawalii hakukuwa na maana ya kuwa alikuwa anawatawala. Mawalii walikuwa wawakilishi wake. Ndio maana ilikuwa hata wakitaka kupitisha bidhaa zao (ikiwa pamoja na watumwa) katika sehemu nyingi walikuwa wanatozwa ushuru. Tanganyika wangedaije Zanzibar wakati haikuwa kuwa sehemu yake? Kale kakanda ambacho Sultan alidai kuwa ni chake (kuzunguka Dar es Salaam) kilipeewa wajerumani 1890 kwenye mkataba wa Heligoland-Zanzibar.

African Association hakikuanzishwa kwa ajili ya siasa. Kilikuwa ni chama cha burdani na kijamii. Kwa sababu hiyo sio ajabu kuwa na matawi Zanzibar ambako kulikuwepo wengi wenye asili ya Tanganyika.

Hauwezi kufananisha miji na nchi. Mimi sijawahi kukutana na raia wa Marekani ambae alijitambulisha kama New Yorker, au hata Texan. Wote nje ya mipaka yao wanajitambulisha kama wamarekani. Hii ni tofauti na wazanzibari ambao wako wanaojitambulisha kama wazanzibari na sio watanzania. Hatuwezi kulazimisha identity.Watanganyika tukiwa kwetu tunajitambulisha kama wakerewe, wachaga, watanganyikan.k. lakini nje ya mipaka yetu bado tunajitambulisha kama watanzania. Hamna ubaya katika hili.

Amandla...
 
Yamepitwa na wakati mkuu tulikuwa tukienda Zanzibar na Passport, leo hii huendi nayo. Anaweza mtu kusema unatakiwa kubeba Passport na ukaamini. Hofu ya Zanzibar ni Population ambayo hata katika mipango miji tunazingatia. Sasa mbona Bara inawakataa Diaspora wanaoishi nje? Je hao sio Watanganyika? Tatizo letu sisi Waafrika ni MALI. Yaani mtu anaona huyu mweusi mwenzangu akija atachukua changu basi! Uchoyo, inda, roho mbaya na unafiki. Lakini aje Mzungu, Mchina au Mwarabu atapokelewa na ardhi atapewa ati mwekezaji. Kajenga nini Hotel! anakula hela yenu wenyewe! Inferiority complex inatumaliza
Wazanzibari wengi mpaka kesho hawamtambui rais wao kama mzanzibari. Mtanganyika haruhusiwi kumiliki ardhi isipokuwa kama mwekezaji mgeni. Hilo na diaspora sijui hata limeingiaje humu? Serikali inachokataa ni kuwatambua kama raia wa Tanzania lakini haina mamlaka au uwezo wa kuwakataza kujitambua kama watanzania. Wengi tuu hata huko waliko wanajivunia utanzania wao ingawa ni raia wa nchi nyingine.
Mimi sidhani kama mtu wa diaspora akija kama mwekezaji nae atanyimwa ardhi kama wawekezaji wengine wageni wanapewa. Hao wageni hawapewi uraia kwa sababu tuu wamewekeza ndio maana sijui wanaingiaje katika mjadala huu.

Amandla...
 
Tanganyika ipi?
Uchambuzi wako wa awali mbona umejichanganya mwenyewe!

Kwa upande mmoja unakubali uwepo wa Tanzania na tuenzi waasisi wake. Pia unakubali kuwepo kwa Tanganyika kwa utawala wa Mwingereza. Isitoshe unakubali uwepo wa makabila mapya yatokanayo na mwingiliano na misukosuko kijamii (rejea mfano wa kabila la Wakerewe kutokana na kutokuelewana kwa ndugu wa kihaya).

Iweje sasa unauliza ati Tanganyika ipi?

Ni Tanganyika iliyopata uhuru 9/12/1961 ikaingia kwenye ramani ya dunia na moja na nchi mwanachama wa "Commonwealth" na "United Nations".

Watanganyika ni wote waliozaliwa kabla na baada ya Uhuru, kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Unguja na Pemba), tarehe 26/4/1964. Kwa sababu hiyo hiyo, Watanzania ni wote waliozaliwa baada ya tarehe ya Muungano. Ila nasikia Wazanzibari hawakubali kuitwa Watanzania na Wapemba hawakubali kuitwa Wazanzibari.

Je, wewe Mkandara ni Mtanganyika au Mtanzania? Kikabila, kwa mfano wako, Mkerewe ni Mhaya?
 
Maneno yako Ni mazuri lakini yamejaa Hila ,unafiki na Nia ovu juu ya ukweli na Uhalisia wa TANGANYIKA.

Tunaipatwje TANZANIA YETU NZURI bila ya Tanganyika na Zanzibar kuungana?
Swali la KWANZA:-
1).Kwanini tunafuta TANGANYIKA na Zanzibar ikibakia na RAIS wake?
2).Kwanini Zanzibar naye haufutwi mpaka leo,kunani hapo?
3).Kwanini TANGANYIKA siku za Leo mnaiita Tanzania BARA?
4).Kwanini Kuna WIZARA zilizo za Muungano na zisizo za Muungano?
-Ni wazi kuwa TANGANYIKA iko hai ndio maana BANDARI ZILIZOGUSWA na kuigizwa kwenye Mpango wa kumpa Mwarabu na DP WORLD yao sio Bandari za Zanzibar Bali Ni BANDARI ZETU za Tanganyika peke yake.

Ni TAHIRA Peke yake aliyepumbazwa na RUSHWA na kupofuka kiasi Cha kutoiona TANGANYIKA kabisa.

Inahitajika MTU awe Mpumbavu wa kiwango Cha juu Sana ndio anaweza kukataa UHALISIA ULIOPO KWAMBA TANGANYIKA NI NCHI.

MAMA SAMIA na Baadhi ya wazanzibar wanajua wanachokifanya kwa makusudi yenye kubenwa Nia ovu juu TAMGANYIKA.
1).MAMA NI MTU WA DINI KWELI KWELI Kwake kutoa Bandari kwa mikataba MIBOVU isiyo na MASLAHI yoyote kwa TANGANYIKA na TAIFA kwa ujumla,Kwa upande wake KUWAPA waislamu WENZAKE'' Bandari ZETU bila UKOMO wa muda anaona ANAPATA THAWABU/BARAKA.

Ukamwambie BARAKA AU THAWABU haipatikani kwa kukabidhi Bandari ZETU MILELE kwa wajomba zako Waarabu.

Msijidaganyikesuala hili la Bandari Nina uhakika litawatokea puani mpende msipende KATIKA JINA LA YESU KRISTO.
Mmejiwekea magenge ya wakati wachache mnaitafuna Nchi hii Kama mchwa anakuka nyasi.

Unajaribu kutumia Hotuba za BABA wa taifa,Mwl. J K Nyerere kutetea UOVU WA KUTOA BANDARI KWA DP WORLD,
Leo JULIUS KAMBARAGE NYERERE angefufuka ajionee uozo wa viongozi wetu wa Serikali,ANGEKUBALIANA NA WIZI UNAOFANYWA KWA KUGEUZWA NA KUPEWA JINA ZURI UWEKEZAJI???

NINAIOENDA SANA TANZANIA YETU KULIKO CHAMA CHOCHOTE CHA SIASA,
NINAIOENDA SANA TANGANYIKA MAANA NDIO NCHI PEKEE ILIYOUNGANA NA ZANZIBAR TUKAPATA TANZANIA.

Nachelea kusema pamoja na maombi,Dua na Sala nyingi na njema za kuliombea TAIFA LETU,MPATE WATANZANIA SIAI SIO MALAIKA TOFAUTI NA MATAIFA JIRANI YALIYOWAHI KUMWAGA DAMU.
AMANI INATUMZWA NA KULINDWA KWA KUTENDA HAKI.

NI VYEPESI MNO NCHI KUINGIA KWENYE MACHAFUKO KULIKO MNAVYOFIKIRIA.Sikilizeni maono yetu Wananchi na muachane na DP WORLD ya DUBAI.Msituingize kwenye MACHAFUKO na uumwagaji wa damu desturi ya kuuana haizoeleki.

Itendeeni mema Tanganyika na sio kutumia JINA TANGANYIKA kwa kuwahadaa WANANCHI ili muendelee kuiibia TANGANYIKA RASILIMALI ZAKE.

MUNGU IBARIKI TANGANYIKA!!!
MUNGU IBARIKA TANZANIA!!!!
 
Yamepitwa na wakati mkuu tulikuwa tukienda Zanzibar na Passport, leo hii huendi nayo. Anaweza mtu kusema unatakiwa kubeba Passport na ukaamini. Hofu ya Zanzibar ni Population ambayo hata katika mipango miji tunazingatia. Sasa mbona Bara inawakataa Diaspora wanaoishi nje? Je hao sio Watanganyika? Tatizo letu sisi Waafrika ni MALI. Yaani mtu anaona huyu mweusi mwenzangu akija atachukua changu basi! Uchoyo, inda, roho mbaya na unafiki. Lakini aje Mzungu, Mchina au Mwarabu atapokelewa na ardhi atapewa ati mwekezaji. Kajenga nini Hotel! anakula hela yenu wenyewe! Inferiority complex inatumaliza
Diaspora wanaoishi nje sio Watanzania
Kwa sababu wengi au karibia wote walioukana uraia wa Tanzania.
Sasa wanakuwaje Watanzania?
 
Niwaambieni hivi. Juhudi za Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar ulikuwepo toka kabla ya Nyerere wakati AA ikiendesha shughuli zake kote bara na Visiwani. Cecil Matola na Mzee Kreist Sykes wakiongoza makao Makuu Dar kwa sababu Mtawala wa kote alikuwa Muingereza. Sultan alikuwa kama King Charles wa Uingereza.

Kwa hiyo, hata zilipoanza harakati za Uhuru AA ya Zanzibar walishirikisha watu kutoka bara kutaka kuunda Chama chao, jina sikumbuki lakini Mzee Sapi alitakiwa kuwa nwenyeji hakuweza kufika maana alikuwa kenda Uingereza.

Kulikuwepo mshirikiano mkubwa baina ya bara na Visiwani kichama asiwadanganye mtu isipokuwa walilazimika kufanya hivyo kwa sababu tayari Muingereza alishamtambua Sultan na kumpa ulinzi wakati Bara amekabidhiwa na UN.
Sidhani kama Seyyid Said aliwahi kutawala pwani yote ya Bara. Alikuwa na makubaliano na baadhi ya city states kama Kilwa, Malindi, Mikindani n.k. Hakuna chief yeyote wa makabila ya pwani aliyemhesabu Sultan kama mtawala wake na hivyo kumpelekea mapato. Kuheshimiwa kwa hao mawalii hakukuwa na maana ya kuwa alikuwa anawatawala. Mawalii walikuwa wawakilishi wake. Ndio maana ilikuwa hata wakitaka kupitisha bidhaa zao (ikiwa pamoja na watumwa) katika sehemu nyingi walikuwa wanatozwa ushuru. Tanganyika wangedaije Zanzibar wakati haikuwa kuwa sehemu yake? Kale kakanda ambacho Sultan alidai kuwa ni chake (kuzunguka Dar es Salaam) kilipeewa wajerumani 1890 kwenye mkataba wa Heligoland-Zanzibar.

African Association hakikuanzishwa kwa ajili ya siasa. Kilikuwa ni chama cha burdani na kijamii. Kwa sababu hiyo sio ajabu kuwa na matawi Zanzibar ambako kulikuwepo wengi wenye asili ya Tanganyika.

Hauwezi kufananisha miji na nchi. Mimi sijawahi kukutana na raia wa Marekani ambae alijitambulisha kama New Yorker, au hata Texan. Wote nje ya mipaka yao wanajitambulisha kama wamarekani. Hii ni tofauti na wazanzibari ambao wako wanaojitambulisha kama wazanzibari na sio watanzania. Hatuwezi kulazimisha identity.Watanganyika tukiwa kwetu tunajitambulisha kama wakerewe, wachaga, watanganyikan.k. lakini nje ya mipaka yetu bado tunajitambulisha kama watanzania. Hamna ubaya katika hili.

Amandla...
Mkuu umasema kitu gani hapa. Seyyid Said alitawala pwani yote ya Bara kumbuka kwamba Sayyid alikuja kabla ya Mjarumani na Muingereza. Yaani toka pwani Mogadishu hadi mpaka wa Msumbiji baada ya kumondoa Mreno.
Na Mreno pia aliuondoa utawala wa Shiraz ambao alitawala eneo hilo hilo na Msimbiji likiitwa AZANIA. Naomba google ama isome historia yetu kwa watangulizi wetu kwa sababu hata Tippu Tip alikuwa Sultan kule DRC.

Sii kweli kwamba AA kilikuwa chama cha Starehe maana Waanzilishi wake walikuwa Wafanyakazi Bandarini, Mabaharia, Watumishi wa Serikali ya Mkoloni.

AA kilichokuwa chama labda niseme UNION kutetea haki za Wafanyakazi. Lakini watu hao hao (baadhi) baadae ndio walokuja kubadilisha mwelekeo wa chama kuwa chama cha Siasa.

Watu wengi wanasema kuwa kilikuwa kijiwe cha starehe kwa sababu kina Sykes walikuwa Wanamuziki na hivyo kuchukulia kwamba AA na TAA vilikuwa vyama vya starehe laa hasha. Toka AA kwenda TAA hadi TANU ilikuwa tu kubadilisha jina kulingana na malengo. Hata AA kuwa ASP ilikuwa na malengo yake. Leo tuna CCM kwa sababu zake. Naweza sema CCM haikupigania Uhuru, kweli kabisa lakini mwenye kuelewa anajua tunazungumzia TANU na ASP.

Hoja ya Wazanzibar, hii imekuja kutokana na muundo wa Serikali tu lakini haipunguzi kitu kwetu. Tena naweza sema Zanzibar wana haki ya kulalamika maana mzigo wote wanaubeba wao kwa kuitaka Zanzibar. Sisi Bara, Bunge Moja la JMT linaendesha ya Mambo ya Muungano na 99% mambo ya Bara. Tumeua ndege wawili kwa jiwe moja wakati Zanzibar inawa cost big time kulipa viongozi wote ambao ni kama wajumbe wa nyumba 10 kwa eneo la mraba.

Tulitakiwa kuwa na nchi MOJA tu. Hapi tunepunguza mabaraza yote ya Zanzibar wakashiriki mabaraza ya JMT kuondosha gharama za ma VX, mafuta, posho. Viongozi wa Zanzibar wanaitaka Tanganyika ili nasi tusikie machungu yao. Na pengine sababu isije tokea tukaunda Tanzania MOJA wakakosa nafasi hizi za ULAJI..
 
Niwaambieni hivi. Juhudi za Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar ulikuwepo toka kabla ya Nyerere wakati AA ikiendesha shughuli zake kote bara na Visiwani. Cecil Matola na Mzee Kreist Sykes wakiongoza makao Makuu Dar kwa sababu Mtawala wa kote alikuwa Muingereza. Sultan alikuwa kama King Charles wa Uingereza.

Kwa hiyo, hata zilipoanza harakati za Uhuru AA ya Zanzibar walishirikisha watu kutoka bara kutaka kuunda Chama chao, jina sikumbuki lakini Mzee Sapi alitakiwa kuwa nwenyeji hakuweza kufika maana alikuwa kenda Uingereza.

Kulikuwepo mshirikiano mkubwa baina ya bara na Visiwani kichama asiwadanganye mtu isipokuwa walilazimika kufanya hivyo kwa sababu tayari Nuingereza alishamtanbua Sultan na kumpa ulinzi wakati Bara amekabidhiwa na UN.

Mkuu umasema kitu gani hapa. Seyyid Said alitawala pwani yote ya Bara kumbuka kwamba Sayyid alikuja kabla ya Mjarumani na Muingereza. Yaani toka pwani Mogadishu hadi Msumbiji baada ya kumondoa Mreno.
Na Mreno pia aliuondoa utawala wa Shiraz ambao alitawala eneo hilo hilo likiitwa AZANIA. Naomba google ama isome historia yetu kwa watangulizi wetu kwa sababu hata Tippu Tip alikuwa Sultan kule DRC.

Sii kweli kwamba AA kilikuwa fhama chama Starehe maana Waanzilishi wake walikuwa Wafanyakazi Bandarini, Mabaharia, Watumishi wa Serikali ya Mkoloni.

AA kilichokuwa chama labda niseme UNION kutetea haki za Wafanyakazi. Lakini watu hao hao baadae ndio walokuja kubadilisha mwelekeo wa chama kuwa chama cha Siasa.

Watu wengi wanasema kuwa kilikuwa kijiwe cha starehe kwa sababu kina Sykes walikuwa Wanamuziki na hivyo kuchikulia kwamba AA na TAA vilikuwa vyama vya starehe laa hasha. Toka AA kwenda TAA hadi TANU ilikuwa tu kubadilisha jina kulingana na malengo. Hata AA kuwa ASP ilikuwa na malengo yake. Leo tuna CCM kwa sababu zake. Naweza sema CCM haikupigania Uhuru, kweli kabisa lakini mwenye kuelewa anajua tunazunfunzia TANU na ASP.

Hoja ya Wazanzibar, hii imekuja kutoka na muundo wa Serikali tu lakini haipunguzi kitu kwetu. Tena naweza sema Zanzibar wana haki ya kulalamika maana mzigo wote wanaubeba wao kwa kuitaka Zanzibar. Sisi Bara, Bunge Moja la JMT linaendesha ya Mambo ya Muungano na 99% mambo ya Bara. Tumeua ndege wawili kwa jiwe moja wakati Zanzibar inawa cost big time kulipa viongozi wote ambao ni kama wajumbe wa nyumba 10 kwa eneo la mraba.

Tulitakiwa kuwa na nchi MOJA tu. Hapi tunepunguza mabaraza yote ya Zanzibar wakashiriki mabaraza ya JMT kuondosha gharama za ma VX, mafuta, posho. Viongozi wa Zanzibar wanaitaka Tanganyika ili nasi tusikie machungu yao. Na pengine isije tokea tukaunda Tanzania MOJA wakakosa nafasi hizi za ULAJI..
African Association ilikuwa na wajumbe mpaka Zambia, Malawi, Uganda vipi nao?
 
Maneno yako Ni mazuri lakini yamejaa Hila ,unafiki na Nia ovu juu ya ukweli na Uhalisia wa TANGANYIKA.

Tunaipatwje TANZANIA YETU NZURI bila ya Tanganyika na Zanzibar kuungana?
Swali la KWANZA:-
1).Kwanini tunafuta TANGANYIKA na Zanzibar ikibakia na RAIS wake?
2).Kwanini Zanzibar naye haufutwi mpaka leo,kunani hapo?
3).Kwanini TANGANYIKA siku za Leo mnaiita Tanzania BARA?
4).Kwanini Kuna WIZARA zilizo za Muungano na zisizo za Muungano?
-Ni wazi kuwa TANGANYIKA iko hai ndio maana BANDARI ZILIZOGUSWA na kuigizwa kwenye Mpango wa kumpa Mwarabu na DP WORLD yao sio Bandari za Zanzibar Bali Ni BANDARI ZETU za Tanganyika peke yake.

Ni TAHIRA Peke yake aliyepumbazwa na RUSHWA na kupofuka kiasi Cha kutoiona TANGANYIKA kabisa.

Inahitajika MTU awe Mpumbavu wa kiwango Cha juu Sana ndio anaweza kukataa UHALISIA ULIOPO KWAMBA TANGANYIKA NI NCHI.

MAMA SAMIA na Baadhi ya wazanzibar wanajua wanachokifanya kwa makusudi yenye kubenwa Nia ovu juu TAMGANYIKA.
1).MAMA NI MTU WA DINI KWELI KWELI Kwake kutoa Bandari kwa mikataba MIBOVU isiyo na MASLAHI yoyote kwa TANGANYIKA na TAIFA kwa ujumla,Kwa upande wake KUWAPA waislamu WENZAKE'' Bandari ZETU bila UKOMO wa muda anaona ANAPATA THAWABU/BARAKA.

Ukamwambie BARAKA AU THAWABU haipatikani kwa kukabidhi Bandari ZETU MILELE kwa wajomba zako Waarabu.

Msijidaganyikesuala hili la Bandari Nina uhakika litawatokea puani mpende msipende KATIKA JINA LA YESU KRISTO.
Mmejiwekea magenge ya wakati wachache mnaitafuna Nchi hii Kama mchwa anakuka nyasi.

Unajaribu kutumia Hotuba za BABA wa taifa,Mwl. J K Nyerere kutetea UOVU WA KUTOA BANDARI KWA DP WORLD,
Leo JULIUS KAMBARAGE NYERERE angefufuka ajionee uozo wa viongozi wetu wa Serikali,ANGEKUBALIANA NA WIZI UNAOFANYWA KWA KUGEUZWA NA KUPEWA JINA ZURI UWEKEZAJI???

NINAIOENDA SANA TANZANIA YETU KULIKO CHAMA CHOCHOTE CHA SIASA,
NINAIOENDA SANA TANGANYIKA MAANA NDIO NCHI PEKEE ILIYOUNGANA NA ZANZIBAR TUKAPATA TANZANIA.

Nachelea kusema pamoja na maombi,Dua na Sala nyingi na njema za kuliombea TAIFA LETU,MPATE WATANZANIA SIAI SIO MALAIKA TOFAUTI NA MATAIFA JIRANI YALIYOWAHI KUMWAGA DAMU.
AMANI INATUMZWA NA KULINDWA KWA KUTENDA HAKI.

NI VYEPESI MNO NCHI KUINGIA KWENYE MACHAFUKO KULIKO MNAVYOFIKIRIA.Sikilizeni maono yetu Wananchi na muachane na DP WORLD ya DUBAI.Msituingize kwenye MACHAFUKO na uumwagaji wa damu desturi ya kuuana haizoeleki.

Itendeeni mema Tanganyika na sio kutumia JINA TANGANYIKA kwa kuwahadaa WANANCHI ili muendelee kuiibia TANGANYIKA RASILIMALI ZAKE.

MUNGU IBARIKI TANGANYIKA!!!
MUNGU IBARIKA TANZANIA!!!!
Ulosema yote nakuelewa na nakubali nawe lakini kilichokosekana hapo nini? jina tu la Tanganyika ulopewa na mkoloni ndio unalilia. Sasa ndugu yangu wewe utakula jina? Kuwa na jina Tanganyika utafaidika na kipi au fahari ya macho! maana unapoomba kitu ujue faida na hasara zake.

Jina tu la Tanganyika kweli au kuna jingine? Kwani tukiitwa Tanzania Bara (Tanzania Mainland) kinapungua kitu gani? Acha wao wajiite Zanzibar sijui Wazanzibar ni fahari kwao lakini inawagharimu. Kwangu mimi hiyo ni Tanzania Visiwani, Zanzibar ni mji.

Kuwa na rais wanamlipa, baraza la Wawakilishi wanalipwa na kodi zao kifupi Serikali nzima inalipwa na wananchi wakati Ofisi moja ingeweza kuhudumia Bara na Visiwani. Mzee Karume akiwa Makamu wa rais alifanya mambo mengi makubwa kuliko hawa viongozi wote waliofuatia.

Cancer ya Mwafrika ni fikra za Ukabila na Udini tu. Unakuta tunapugania kwa nini Mawaziri wengi Wakristu! Je anapokuwa Muislaam anawasaidiaje Waislaam? Mimi sijaona iwe, Mwinyi Kikwete au Mama Samia na Mawaziri wote wanafanya kazi ya Chama na sii kabila wala dini.

Hata hivyo viti maalum kwa Wanawake ni Ujinga mtupu ikiwa wanawake hao hawahusiki na maswala ya Wanawake.

Kwangu mimi Tanganyika ni uzao wa MKOLONI yaani nchi ilogawanywa kwa mfumo wa divide and rule tukazipoteza Rwanda na Burundi. Leo hii tuna wakimbizi wengi kutoka Burundi na Rwanda raia wa Tanzania tofauti yetu ni mipaka tu.

Siku tutakuwa na Tanganyika, basi ujue hatutakuwa salama kesho. Mikoa ya kanda ya Ziwa Geita na Mara watajitoa kwa sababu dhahabu yao inachukuliwa kwa jina la Tanzania na Tanganyika.

Mtwara nao watadai Gas yao kwa sababu fikra ni zile Ile kugawana URITHI kwa kisingizio cha NCHI

Kumbuka tu kabla ya Mjarumani hatukuwa na Tanganyika. Bara iliongozwa na Machief wake ambao mpaka kesho wanataka watambuliwe. Libya leo hii Machief ndio viongozi mbali na Serikali ilosimikwa. Ugonvi hauishi kwa sababu ya Mafuta..
 
African Association ilikuwa na wajumbe mpaka Zambia, Malawi, Uganda vipi nao?
Wote ndugu zetu, kwani mzee wako akizaa Uganda, hao sii ndugu zako? Lakini inabakia wana maisha yao au sio!
 
Diaspora wanaoishi nje sio Watanzania
Kwa sababu wengi au karibia wote walioukana uraia wa Tanzania.
Sasa wanakuwaje Watanzania?
Mnadanganywa ndio maana mnaitwa WADANGANYIKA. Hakuna Mtanzania anayeishi nje aliukana Utanzania kwa sababu kuna process na balozi zetu hujulishwa pale mtu anapoukana Utaifa wake.

Hutakiwi kusikiliza parapanda za vucuzela ukaamini pasipo kutumia akili yako. Mtu akiukana Utanzania leo hii Serikali ya Tanzania itajulishwa kuwa mtu huyu kwa jina hili, passport namba hii sio tena raia wa Tanzania na pasi yake inarejeshwa Tanzania. Unaachia Passport ya Tz, Ndio utararibu wa Kimataifa. Sasa Waulize list hiyo kama wanayo.
 
Niwaambieni hivi. Juhudi za Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar ulikuwepo toka kabla ya Nyerere wakati AA ikiendesha shughuli zake kote bara na Visiwani. Cecil Matola na Mzee Kreist Sykes wakiongoza makao Makuu Dar kwa sababu Mtawala wa kote alikuwa Muingereza. Sultan alikuwa kama King Charles wa Uingereza.

Kwa hiyo, hata zilipoanza harakati za Uhuru AA ya Zanzibar walishirikisha watu kutoka bara kutaka kuunda Chama chao, jina sikumbuki lakini Mzee Sapi alitakiwa kuwa nwenyeji hakuweza kufika maana alikuwa kenda Uingereza.

Kulikuwepo mshirikiano mkubwa baina ya bara na Visiwani kichama asiwadanganye mtu isipokuwa walilazimika kufanya hivyo kwa sababu tayari Nuingereza alishamtanbua Sultan na kumpa ulinzi wakati Bara amekabidhiwa na UN.

Mkuu umasema kitu gani hapa. Seyyid Said alitawala pwani yote ya Bara kumbuka kwamba Sayyid alikuja kabla ya Mjarumani na Muingereza. Yaani toka pwani Mogadishu hadi Msumbiji baada ya kumondoa Mreno.
Na Mreno pia aliuondoa utawala wa Shiraz ambao alitawala eneo hilo hilo likiitwa AZANIA. Naomba google ama isome historia yetu kwa watangulizi wetu kwa sababu hata Tippu Tip alikuwa Sultan kule DRC.

Sii kweli kwamba AA kilikuwa fhama chama Starehe maana Waanzilishi wake walikuwa Wafanyakazi Bandarini, Mabaharia, Watumishi wa Serikali ya Mkoloni.

AA kilichokuwa chama labda niseme UNION kutetea haki za Wafanyakazi. Lakini watu hao hao baadae ndio walokuja kubadilisha mwelekeo wa chama kuwa chama cha Siasa.

Watu wengi wanasema kuwa kilikuwa kijiwe cha starehe kwa sababu kina Sykes walikuwa Wanamuziki na hivyo kuchikulia kwamba AA na TAA vilikuwa vyama vya starehe laa hasha. Toka AA kwenda TAA hadi TANU ilikuwa tu kubadilisha jina kulingana na malengo. Hata AA kuwa ASP ilikuwa na malengo yake. Leo tuna CCM kwa sababu zake. Naweza sema CCM haikupigania Uhuru, kweli kabisa lakini mwenye kuelewa anajua tunazunfunzia TANU na ASP.

Hoja ya Wazanzibar, hii imekuja kutoka na muundo wa Serikali tu lakini haipunguzi kitu kwetu. Tena naweza sema Zanzibar wana haki ya kulalamika maana mzigo wote wanaubeba wao kwa kuitaka Zanzibar. Sisi Bara, Bunge Moja la JMT linaendesha ya Mambo ya Muungano na 99% mambo ya Bara. Tumeua ndege wawili kwa jiwe moja wakati Zanzibar inawa cost big time kulipa viongozi wote ambao ni kama wajumbe wa nyumba 10 kwa eneo la mraba.

Tulitakiwa kuwa na nchi MOJA tu. Hapi tunepunguza mabaraza yote ya Zanzibar wakashiriki mabaraza ya JMT kuondosha gharama za ma VX, mafuta, posho. Viongozi wa Zanzibar wanaitaka Tanganyika ili nasi tusikie machungu yao. Na pengine isije tokea tukaunda Tanzania MOJA wakakosa nafasi hizi za ULAJI..
Mkuu unataka kutupoteza.
Seyyid Sayid hakuwahi kutawala pwani nzima ya Tanganyika kwa sababu wakati anakuja hapakuwa na nchi ya Tanganyika. Katika pwani hiyo kulikuwa na miji ambayo ilikuwa ikijitawala kama Kilwa, Mombasa, Mikindani n.k. Miji hii ilikuwa vituo vya biashara na ilikuwa ikipigana yenyewe kwa yenyewe. Wa Omani walikuwa wanakaribishwa mara kwa mara kusaidia upande mmoja dhidi ya mwingine. Mwaka 1698 waliitawala Zanzibar baada ya kuwashinda wareno. Seyyid Said alikuja baadae na kikubwa alichofanya ni kufanya Stone Town kuwa makao makuu ya usultani wa Oman. Tofauti na unavyosema Seyyid Said hakutawala Mogadishu bali alipeleka mwakilishi 1843 na alikuwa anamlipa tribute Sultan Yusuf Mahmud Ibrahim wa Geledi. Hicho unachosema kuwa ni ilikuwa milki ya Sultan iliainishwa na wajerumani na waingereza mwaka 1886 na kilianzia Capo Delgado hadi Kipini (Kenya). Sehemu hii ilichukuliwa na Ujerumani kama sehemu ya makubaliano kati ya Ujerumani na Uingereza yaliyojulikana kama Heligoland-Zanzibar Treaty. Sultan wa Zanzibar hakuwahi kuhusika na utawala wa Tanganyika baada ya wajerumani kuingia.

Uhusiano kati ya Zanzibar na Tanganyika ulikuwa mkubwa kwa sababu ya shule ya wamisionari wa UMCA iliyokuwa Zanzibar ( nyingine ilikuwa ya CMS iliyokuwa Mombasa)ambazo ziliemisha wasomi wa kwanza wakitanganyika. Wasomi hawa walikuwa wakina Samwil Chiponde na Benedict Madalito Mmakua walishirikiana na wasomi wenzao kama Cecil Matola ( mwalimu wa Government School), Edwin Brenn, Rawson Watts ( hawa walitoka CMS), Kleist Sykes karani wa kampuni ya reli Ali Saidi ( mzaramo mkaguzi wa majengo) Ramadhani Ali ( mfanyabiashara na
bingwa wa ngoma ya Marini) wakiongozwa na Martin Kayamba ambae alikuwa mjukuu wa Kimweri ye Nyumbai walianzisha chama cha Tanganyika African Civil Service Association. Wakati wanaanzisha chama hicho Martin Kayamba ndie aliyekuwa mtumishi wa umma mwenye kikubwa Tanganyika. Chama hicho kilianzishwa 1922.
Mwaka 1929 wakina Matola, Sykes, Saidi, Ali, na wengine wakaanzisha African Association ambayo rais wake alikuwa Cecil Matola. Chama hiki kilijikita zaidi kwenye masuala ya kijamii na burudani.

Katikati ya miaka 1930, Mganda Erica Fiah alianzisha chama cha Tanganyika African Welfare and Commercial Association ambacho kilikuwa cha kisiasa zaidi. Fiah alianzisha pia gazeti la Kwetu na alikuwa mfuasi wa Marcus Garvey.

Vijana wao waliporudi kutoka kupigana katika vita Kuu ya Pili ya Dunia walikuta AA imedumaa. Mwaka 1948 walifanya mapinduzi na kukbadilisha jina kuwa Tanganyika African Association ( wengine wanasema tofauti kati ya wazanzibari na watanganyika zilichangia ubadilishwaji huo wa jina) mwaka 1948. Viongozi wa TAA walikuwa ni Dokta wa kihaya Vedasto Kyaruzi aliyechaguliwa kuwa Rais na Abdulwahid Sykes aliyechaguliwa kama Katibu. Wakati wa mabadiliko haya Kleist Sykes aliyekuwa baba yake Abdulwahid Sykes alikuwa Rais wa AA baada ya Cecil Matola kufariki. Hawa vijana waliposhika usukani ndio walibadilisha iliyokuwa AA kuwa ya kisiasa zaidi. Hali hii iliendelea mpaka 1954 ambapo TAA ikageuzwa kuwa chama kamili cha kisiasa kilichoitwa TANU. CCM haikupigania uhuru kama chama cha siasa lakini kwa sababu kilitokana na TANU wanastahili kupewa heshima hiyo kwa upande wa Tanganyika.

Sikuelewi unaposema kuwa Zanzibar wanabeba mzigo mkubwa katika huu Muungano wakati kwa kiasi kikubwa bajeti ya JMT inabebwa na Tanganyika na wazanzibari wana haki ya kupata huduma yeyote kama watanzania wakati watanganyika hizo huduma sio stahili yao wakiwa Zanzibar. Tunaona mbunge kutoka Zanzibar ambaye amechaguliwa na watu ambao hawazidi 100000 anaweza kupewa uwaziri wa wizara ambayo haipo Zanzibar! Wazanzibari wana haki ya kupewa nafasi za uongozi katika taasisi ambazo ziko bara na zinaendeshwa na mapato yanayozalishwa bara. Uonevu gani unaouzungumzia? SMZ inalipa viongozi wake tuu na inamamlaka kabisa kupunguza idadi ya viongozi kama wanaona wanakuwa mzigo. Serikali ya JMT haihusiki kwenye hilo.

Amandla...
 
Back
Top Bottom