Hizo line za voda ambazo watu wanakatwa hela zinaanza code ganiKuna mtu leo anasema amekatwa kama elfu nne hivi kwenye Mpesa yake na hajui Kwan kakatwa.
Hapa najaribu kuuliza Salio kwenye Mpesa app naona inagoma kabisa
Pasipo kupepesa macho, airtel ni moja ya mtandao ambao matapeli kila itwayo leo huutumia kutuma sms za kila aina, mpaka muda huu sijajua tatizo ni nini??
Natumia mtandao wa tigo pia, kwakweli nisiwe mnafiki nakaa mpaka miezi 6 yaan huwezi kuona sms yeyote ya kitapeli, sijui tuma kule, mimi mwenye nyumba nasubiria kodi yako, mwanao kaanguka shule, na mambo mengine.
Nimejaribu kusajiri laini mpya nikasema ngoja niiweke tu ndani kwa mwezi mzima pasipo kuweka hata vocha, aisee ninayoshuhudia sijui nifanyeje, yaan ukirudi ukipitia simu unakuta sms mpaka 4 za kitapeli.
Airtel ombeni ushauri hata mitandao mingine labda mjifunze wenzenu wameweza kuwabana vipi hawa matapeli ambayo kila muda tuma humu???
Inafika nyakati mpaka kufungua sms unaona ujinga maana kwa siku hukosi sms mbili hadi 4 za matapeli, tatizo ni nini???
AIRTEL HEBU WACHUNGUZENI WALE WANAOPITA MTAAN KUSAJIRI LAIN LABDA INAWEZA KUPUNGUZA KELO.