Mtaalam wa Kipemba: Kikosi cha Taifa Stars dhidi ya Uganda Cranes kiwe hivi Jumapili na Kisibadilke hadi dakika 90...tunashinda 3 kwa 1

  1. Aishi Manula
  2. Hassan Kessy
  3. Gadiel Michael
  4. Erasto Nyoni
  5. Kelvin Yondan
  6. Jonas Gerald Mkude
  7. Simon Msuva
  8. Farid Musa
  9. Mbwana Samata
  10. John Boko
  11. Shiza Kichuya

Kisibadilishwe hadi dakika 90 kwani hata ‘ Kinyota ‘ na ‘ Kindumba ‘ ndiyo kitatupeleka kwa mara ya pili baada ya miaka 38 huko AFCON na Nahodha ajitahidi akichagua upande wa Kuanzia tuanzie Goli la Kusini ili tumalizie na la Kaskazini.

Kwa Kikosi hiki nilichokiweka hapa GENTAMYCINE mpaka dakika hii naandika huu ‘ Uzi ‘ Waganda wameshajitahidi Kuzipunguza ila kuna Goli 3 kwa 1 ( 3 – 1 ) ambapo hata hilo Goli lenyewe litakuwa ni ama la Sisi Kujifunga au ni la Penati.

Kuhusu ‘ Mzigo ‘ wa Timu ( nadhani hapa Watu wa Mpira ) na wale ( wana Utamaduni Wenzangu ) mtakuwa mmeshanielewa akabidhiwe kati ya Farid Musa au Hassan Kessy na asipewe Nahodha Mbwana Samata kwani wenye ‘ Nyota ‘ na huo ‘ Mzigo ‘ kwa Siku hiyo ( ili Kuipa Ushindi na Kuikinga pia ) ni hawa Wachezaji Wawili niliowataja hapa.

Namalizia tena kwa Kusisitiza hiki Kikosi nilichokiweka hapa ndicho Kipangwe Siku hiyo na kama kuna Mtu yoyote anaweza ‘ akaufowadi ‘ huu ‘ Uzi ‘ kwa Benchi la Ufundi na hadi kwa Rais wa TFF na walio karibu na Timu yetu ya Taifa afanye hivyo haraka na Wachezaji hawa niliowataja hapa kuanzia leo waanze Kujiandaa na Kujipanga huku wakijua kabisa Wao ndiyo wanatupeleka AFCON Misri mwezi June 2019.

Kila la kheri Taifa Stars.

Nawasilisha.
Wewe jamaa mbea sana, sina hakika kama una marinda yote. Nitaenda kariakoo nikununulie dela, vipi ni kikuku unataka cha shaba, fedha au dhahabu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom