Msimamo wa wana CCM juu ya MCC ni dharau na udanganyifu kwa walipa kodi

UKWELI KUHUSU MCC NA MISAADA KWA TANZANIA
Baada ya Tanzania kunyimwa msaada wa Shilingi Trilioni Moja na Shirika la Kimarekani la Millenium Challenge Corporation (MCC), viongozi wa kiserikali, akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Agustine Mahiga, Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na makada kadhaa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kama Humphrey Polepole, kila mmoja kwa wakati wake, wamejaribu kuwapotosha na kuwapumbaza Watanzania, wakijaribu kupenyeza propaganda na uongo wa aina kuu tatu:
• Kwanza, Wanajifanya wao ni Wazalendo kwelikweli na kudai kuwa “Uhuru wa Tanzania hauwezi kuingiliwa wala kuthaminishwa kwa Shilingi Trilioni Moja za Kimarekani”. Na kwamba watahakikisha maendeleo ya Tanzania yanashughulikiwa kwa kuongeza “mapambano dhidi ya rushwa na kukusanya kodi kwa wingi”.
• Pili, wanadai Serikali ya Tanzania haitaki misaada na haitaathirika kwa namna yoyote ile kwa kunyimwa msaada huo. Waziri wa Fedha, Dk Philip Mpango alifikia hatua ya kusema kuwa “hata bajeti ijayo ya serikali haikuzijumuisha fedha hizo za MCC”, na kwamba bajeti ijayo itajitosheleza bila kutegemea fedha za MCC.
• Tatu, wanajikanganya kwa kudai kuwa uamuzi wa MCC haukuwa wa haki – Tanzania ilionewa. Hapa, Waziri Mahiga alidai kuwa MCC walipaswa kujadiliana kwanza na Serikali kabla ya kusitisha msaada huo. Mahiga alikwenda mbali zaidi akidai “demokrasia ya Tanzania haiwezi kupimwa kwa kutazama uchaguzi wa Zanzibar tu” na kusisitiza kuwa Tanzania ni nchi inayofuata utawala bora na demokrasia.
Kwa nafasi yangu kama Waziri wa Mambo ya Nje wa Upinzani, Mbunge na Mzalendo wa Kweli wa Taifa hili, nachukua fursa hii kwa mara nyingine tena kuwaeleza Watanzania ukweli dhidi ya uongo na upotoshwaji mkubwa uliofanywa na Wana-CCM hao bila kujali maslahi ya Watanzania na Mustakabali wa Taifa hili:
Ukweli Unaopotoshwa:
1. Nianze na suala la uzalendo. Wanaojifanya Wazalendo kwa kupinga uamuzi wa MCC, si wazalendo wa kweli wa nchi hii – ni Wazalendo Uchwara.
Uamuzi wa MCC kusitisha msaada kwasababu ya kuchukizwa na uchaguzi haramu wa marudio kule Zanzibar na Sheria kandamizi ya makosa ya mitandaoni (Cyber Crime) iliyoipitishwa kibabe na Serikali hii, ulikuwa ni uamuzi sahihi na uliojali maslahi endelevu si tu ya watu wa Taifa hili bali ya maslahi ya Dunia hii. Chaguzi haramu kama ule wa Zanzibar zinaweza kabisa kuchochea matukio ya ugaidi, vita vya wenyewe kwa wenyewe na kukwamisha maendeleo kwasababu ya kulazimisha kuweka viongozi madarakani kimabavu bila kujali hatima endelevu ya Taifa na Dunia kwa ujumla. Demokrasia na Uhuru wa Watu ndiyo rutuba kuu ya kupata maendeleo makubwa, ya maana na endelevu.

“Ni uwendawazimu kwa Mtanzania yeyote yule kujifanya anatetea “uzalendo” wa Taifa lake kwa kushambulia Mataifa na Mashirika ya nje, kwa suala ambalo Serikali yetu yenyewe ndio inayokandamiza demokrasia na kuminya uhuru wa watu wa Taifa hili”
“Uzalendo si kupinga kila kitu kinachotendwa au kuamuliwa na watu au taasisi za Taifa jingine, bali ni kupinga udhalimu wa aina yoyote ile bila kujali unatendwa na nani; uzalendo wa kweli si kupinga mataifa na mashirika ya kigeni bila sababu za msingi, bali ni kupinga udhalimu unaofanywa na yeyote yule, ukiwemo udhalimu unaofanywa na Serikali yetu dhidi ya watu wa Taifa hili; uzalendo ni kusimamia mambo ya msingi na kupinga mambo ya hovyo”.
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema:
“Kaburu ni Kaburu tu….hata awe na rangi nyeusi…bado anabaki kuwa ni Kaburu tu”
Hatuwezi kutetea udhalimu wa Serikali yetu eti kwasababu tu watu wa nje wamechukua hatua dhidi ya serikali yetu. Serikali yetu sio Mungu, ikikosea ni lazima tuikosoe. Tuache kutetea ujinga.
Inasikitisha kuona kuwa Wamarekani na MCC yao wameonyesha uzalendo wa kusimamia mambo ya msingi, kuliko hawa Wazalendo Uchwara wa CCM wanaotetea udhalimu wa serikali hii, bila kujali hasara kubwa ya mahusiano ya kidiplomasia na kimaendeleo wanayoisababishia Tanzania”
Ni ujinga kufikiri kuwa eti Taifa litapata maendeleo ya uhakika kwa mtindo wa kutumbua majipu tu. Matatizo ya Tanzania kamwe hayawezi kufananishwa na mtu mwenye majipu ambapo yakitumbuliwa tu basi matatizo hayo yanakwisha – hapana. Kama ni ugonjwa, basi Tanzania yetu inaugua Kansa na Kansa haitumbuliwi. Kansa hushughulikiwa kwa kupiga mionzi au kukata viungo.
Kansa inayoitafuna Tanzania ni Kansa ya kuwa na mfumo kandamizi wa kiutawala na kisheria; mfumo unaowaminya watu uhuru wa kujiwekea serikali na viongozi bora wanaowataka; mfumo unaowanyima Watanzania uhuru wa kuikosoa na kuiwajibisha vizuri serikali yao; ni mfumo huu mbovu unaoipa CCM jeuri ya kufanya itakavyo ndio uliosababisha MCC kusitisha misaada. Wenzetu wanajua fika hakutakuwa na tija kutoa msaada kwa serikali yenye vijinasaba vya udikteta kama hii – udikteta na maendeleo havipatani - ni Mbingu na Ardhi!
2. Nizungumzie na kauli za hovyo.
Eti “serikali haitaki misaada” kama alivyosema Waziri wa Fedha Dk. Philip Mpango na kudai kuwa “Tanzania haitaathirika kwa kukosa fedha za MCC”
Ukweli ni kwamba kuna tofauti kubwa sana kati ya kukataa msaada na kunyimwa msaada. Kukataa msaada ni heshima lakini kuomba msaada na kunyimwa ni aibu kubwa. Tanzania iliingia kwenye program ya kusaidiwa na MCC. Haiwezekani Serikali inyimwe fedha kwa kushindwa kutimiza vigezo halafu viongozi wa kiserikali na CCM wajifanye hawakuzitegemea fedha hizo.
Tanzania si tu ilizitegemea fedha za MCC, bali pia bado inategemea misaada ya nchi na mashirika mbalimbali ya kimataifa.
Kwa mfano, wakati mawaziri wakidai kuwa wanaanza kuiendesha nchi hii hivi sasa bila kutegemea misaada, hali halisi ya sekta ya afya inaonyesha kuwa kwa muda mrefu mashirika mbalimbali ya kimarekani ndiyo yamekuwa yakinusuru afya za Watanzania kuliko serikali yetu.
Hapa nchini kuna NGOs nyingi za kimarekani zinazotekeleza miradi ya afya zaidi ya 50 kwenye maeneo mbalimbali. Mashirika hayo ni kama Johns Hopkins, FHI 360, White Ribbon Alliance na maengineyo. Baadhi ya miradi wanayoitekeleza inahusu kusaidia ununuzi na ugavi wa dawa nchini; kuwajengea uwezo watoa huduma za afya nchini, hasa kwenye eneo la afya ya mama na motto, kuelimisha jamii jinsi ya kubadili tabia na mienendo ili kujikinga na magonjwa ya zinaa na milipuko kama Ukimwi na kipindupindu na mengineyo, na miradi mingine inahusu kuboresha zahanati na vituo vyetu vya afya kwenye maeneo mbalimbali nchini. Hii ndiyo kusema kuwa ni ujinga wa hali ya juu kuwa na viongozi wa serikali wanaoongea uongo usiokuwa na faida yoyote ile kwa Watanzania. Ikitokea nchi zote wahisani, mashirika ya misaada na NGO’s zao za kimataifa zikaacha kuisaidia Tanzania ni dhahiri kuwa hali itakuwa ni mbaya sana kwa Wananchi walio wengi.
Mathalan, takwimu zinaonyesha kuwa nchini Tanzania mwanamke mmoja kila saa anapoteza maisha kwasababu ya kukosa huduma bora za afya wakati akiwa mjamzito na wakati wa kujifungua. Kwa maneno mengine, takribani wanawake 24 nchini Tanzania hupoteza maisha kila siku na takribani wanawake 9,000 hupoteza maisha kila mwaka si kwasababu Mungu amependa, bali kwasababu serikali ya CCM kwa muda mrefu imeshindwa kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto nchini.
Aidha, takwimu za utafiti wa Hali ya Idadi ya Watu na Afya – Demographic and Health Survey” wa miaka ya hivi karibuni, zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 42 ya watoto wote nchini wamedumaa, hasa kwasababu ya utapiamlo au lishe duni. Idadi hii ni kubwa mno na inatishia mustakabali wa Taifa. Mtoto aliyedumaa akili yake haitaweza kufanya kazi kwa ufanisi kwa asilimia mia moja. Hii inasababisha Tanzania kuwa katika hatari ya kuwa Raslimali Watu wasioweza kuzalisha kikamilifu na hivyo kuathiri zaidi ukuaji wa uchumi na maendeleo ya jamii.
Mashirika mengi ya kimataifa, yakiwemo ya Marekani, Uingereza, Ujerumani, Uholanzi, Canada ndiyo yanayojaribu kuisaidia Tanzania kuboresha huduma za afya na kupunguza vifo vingi vinavyoepukika na kutekeleza miradi ya kuimarisha huduma za lishe ili kupunguza udumavu wa watoto kwenye yetu. Kwa mantiki hii, ni ujinga wa hali ya juu kwa viongozi wa serikali hii kujifanya hawataki misaada, wakati wanajua ukweli kuwa bado nchi yetu inahitaji misaada wakati ikijaribu kujikongoja ndipo tuweze kujitegemea
Nasisitiza kuwa Tanzania si kisiwa na kamwe haiwezi kuishi kama kisiwa - tunahitaji kushirikiana vema na mataifa mengine, kufanya kazi kwa karibu na mashirika ya ndani na ya kimataifa katika kusukuma maendeleo yetu na maendeleo ya dunia. Hii ni dunia ya kutegemeana na kuhitajiana, si kifedha tu bali kuingiliana vizuri kibiashara, kimisaada na kidiplomasia. Serikali yetu imekosea, inapaswa kujirekebisha, iache kiburi. Kiburi si maungwana
Hatua ya Mawaziri wa Magufuli kudai kuwa Tanzania haitaathirika kwa kuzikosa Trilioni Moja za MCC ni ujinga mwingine uliopitiliza. Ni lazima tutaathirika kama ifuatavyo.
• Fedha za MCC zilikuwa zielekezwe kwenye miradi ya umeme vijijini kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA). REA ina wafanyakazi zaidi ya 450, kusitishwa kwa msaada huo kunaweza kuharibu ajira za Watanzania wenzetu na familia zao.
• Uchambuzi wa taarifa za serikali yenyewe unaonyesha kuwa gharama ya mtu kufungiwa umeme ilianza kupungua hadi kufikia shilingi 67,000. Hatua ya MCC kusitisha msaada wake inaweza kusababisha gharama za kuwafungia watu umeme vijijini kupanda sana na Watanzania wengi wanaweza kuendelea kubaki gizani kwasababu ya kushindwa kumudu gharama hizo.
• Ipo hatari kwa serikali hii kupandisha viwango vya kutoza kodi kwenye bidhaa na huduma mbalimbali ili kujaribu kupata fedha za kufidia pengo la fedha zilizokuwa zitolewe na MCC. Hali hiyo itatuweka Watanzania kwenye mzigo mkubwa wa gharama za kulipa kodi na kusababisha makali ya maisha kwasababu tu ya uchu na ulevi wa madaraka wa serikali ya CCM.
• Ni vema Watanzania wakaacha kurubuniwa na CCM iliyoshindwa kutatua matatizo yao kwa muda mrefu. Trilioni moja ni fedha nyingi sana. Ni 5% ya bajeti ya nchi yetu..
Ukichukua Trilioni 1 ukaiweka kwenye noti za elfu 10 utapata jumla ya noti 100,000,000. Kila noti ina urefu wa sentimita 12. Kwa hiyo tukizidisha tunapata sentimita 1,200,000,000 (100,000,000×12). Kilomita 1 ni sawa na sentimita 100,000. Kwa hiyo tukichukua sentimita 1,200,000,000 tukagawanya kwa 100,000 tunapata kilomita 12,000. Umbali wa kutoka Johanesburg (Afrika kusini) hadi Cairo (Misri) ni kimomita 6,259. Kwa hiyo kilomita 12,000 ni sawa na kutoka Johanesburg hadi Cairo mara mbili.
Maana yake ni kwamba ukiweka Trilioni 1 katika noti za elfu 10 unaweza kuzipanga kuanzia Johanesburg hadi Cairo mara mbili bila kuacha hata sentimita moja njiani.
Yani uchukue noti za elfu "kumi" uzipange kuanzia Johanesburg upande nazo hadi Botwsana, kisha Harare, Lusaka, Tunduma, Dar, Nairobi, Khartoom, hadi Cairo bila kuacha hata sentimita moja njiani, kisha ukifika Cairo unaanza tena upya kuzipanga kwa kurudi hadi Johanersburg. Hizo ndio fedha ambazo Marekani wametunyang'anya baada ya kufanya uhuni kule Zanzibar na kupitisha sheria kandamizi bila kujali.

Ni wakati wa kuacha kushabikia utumbuaji majipu wakati Taifa linaugua Kansa - Kansa haitumbuliwi!. Tanzania yetu itapona kwa kufanya mageuzi makubwa ya kimfumo na kujenga nidhamu na haiba njema katika diplomasia ya kimataifa. Hii ni dunia ya kutegemeana na kuhitajiana, si kifedha tu bali kuingiliana vizuri kibiashara, kimisaada na kidiplomasia.
Hata mataifa tajiri kabisa duniani hayakufika hapo yalipo kwa jitihada zao yenyewe, yalitegemea pia mataifa na mashirika ya kimataifa. Tunapaswa kujenga uwezo wa kujitegemea huku tukitegemeana na wenzetu. Tunataka kufikia uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 kama India na Malaysia...hata .hawa tunaotaka kuwafikia nao walisaidiwa na bado wanasaidiwa. India ni moja ya nchi zilizo kwenye programu ya kusaidiwa na MCC
3. Napinga pia madai mengine ya uongo kuwa Tanzania tulionewa. Hatukuonewa. Serikali yetu ilivijua vizuri na mapema vigezo vyote vya kupata fedha za MCC, lakini ilipuuza kwa sababu ya kuendekeza uchu na ulevi wa madaraka.

Mwisho.
 
Ukumbuke Tanzania ni kubwa mara mbili ya jimbo la California kijiografia.

Watu wa ccm wanaoongoza hii nchi hawaeleweki,mkopo wanataka lakini masharti hawataki,masharti yenyewe rahisi.

Ccm na Mcc ni sawa na mwanamke alieolewa huku bado anang'ang'ania kulala na chupi. Ndoa unataka kuvua chupi hutaki,kubaki kwenu hutaki.
 
  1. Kila mtu kwa nafasi yake (waalimu, wajiriwa serikalini na sekta binafsi, wakulima, wafanyabiashara/wajasiliamali na kadhalika) awajibike kwa kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na uaminifu bila ujanja ujanja (Kama vile kukwepa kodi, rushwa, uvivu na kadhalika).
  2. Tuachane na mentality ya kwamba bila misaada hatuwezi kuendelea ama kusimama wenyewe.
  3. Tulipe kodi kwa kadri ipaswavyo
  4. Tufichue wala rushwa, wabadhirifu wa mali za umma, na wakwepa kodi
  5. Tupunguze ama tuachane kabisa na biashara za uchuuzi (kununua na kuuza) au umachinga
  6. Tukazanie kwenda kwenye biashara za kilimo na ufugaji.
  7. Tujikite zaidi kwenye innovations za IT
  8. Tuache uswahili wa kuahidi vitu/mambo bila kuvitekeleza au kuwa na excuses nyingi zisizo na mashiko.
  9. Tuwe na mentality kwamba serikali ni catalyst (provokes) ya wewe kujiletea maendeleo ya kiuchumi badala ya yenyewe kuwa agent (acting on behalf of you) wa kukuletea maendeleo.
  10. Let's be positive with a can-do attitude and dependent to none.
Mimi siko tayari kufanya haya kisa jecha kasababisha tukose misaada,haya wafanye watu wa ccm na jecha wao,wengine tuendelee kula maisha ya misaada.
 
Mjomba lipa kodi fanya kazi....unapunguzaje gape kwa msaada wenye mashart???

Funga mkanda acha kutegemea nguo ya kuazima kwani haistiri makalio

1.Utawala bora.
2. Ulinzi na Usimamizi wa haki za Wananchi - kisiasa, kijamii na kiuchumi.”


Masharti haya yanaubaya gani?Kwanini serikali ishindwe kuyafuata?Kuna tatizo gani hapo kuwa na misingi ya UHURU na HAKI ZA BINADAMU?

Hivi ukiwa minzani uanbadilika na kuwa mgeni??Kama tulikubali kuwa na vyama vingi basi tukubali kwamba muda unabadilika na penye AMANI lazima kuwe na HAKI
 
Goliath mfalamagoha

1. Tanzania tulikwenda kuomba pesa za MCC wenyewe. Hatukulazimishwa

2. Ya Jecha ni aibu kwa Taifa, makada wa CCM wanaona aibu kuzungumzia upuuzi ule

3. MCC wamekatalia pesa zao kwa vigezo vyao tulivyowahi kufuzu mwanzao

Wanaosema Uzalendo, lengo lao tuungane kulaani MCC ambao hawana makosa!
Hilo tumekataa. Uzalendo hauujengwi kartika unafiki

Sasa hivi wanaandika nyuzi nyingi kulaani UKOLONI, hawakuwahi kulaani pesa za MCC

In fact Magufuli/CCM walitumia MCC katika kampeni.
Magufuli alikuwa waziri wakati MCC inatoa na tunapokea pesa! Hakukataa kwa uzalendo

Kinachoendelea sasa hivi ni Taifa kutengwa na dunia

Yote yanatokea kulinda watu pengine 10 kule Zanzibar kwa gharama ya watu milioni 45

Anayebeba mzigo wa matatizo haya ni Magufuli, siyo MCC

Anayetakiwa kuwaambia Watanzania milioini 45 kwanini watu wachache wanayumbisha Taifa ni Magufuli, Siyo MCC wala Marekani

MCC wapo sahihi kabisa hakuna kosa walilotenda wala hatujaonewa na Marekani au EU

Badala ya kutafuta sababu za hovyo ambazo Watanzania wengi wanazikataa , jicho , kauli na kila kitu tukielekeze kwa Magufuli mwenye jibu tumefikaje hapa na tunakwenda mbele tukiwa tumetengwa na jamii ya kimataifa kwanini!

Kwasasa wananchi hawaoni, siku itakapoanza kuuma wananchi watasaga meno.
Hawa wanaowaambia Uzando hawataumia na chochote! wanawahadaa ili mkate wao uendelee kuwepo mezani. Wanajua katika nafsi zao MCC/EU/US hawana kosa lolote

Mwenye majibu ni Magufuli na CCM wala si Jecha, Shein na Sif Idd. Ni magufuli

Magufuli awaambie Watanzania tumefikaje hapa?

MCC wapo sahihi, UE/Marekani hawana ukoloni wala hawajaonea mtu.
 
Huwezi kujadili mkwamo bila kuadress chanzo cha mkwamo!. Kuadress chanzo cha mkwamo ni kupata permanent solution ya mkwamo wa sasa na mingine mingi iliyopo na inayoendelea kuja na itakayotokea hapo mbele inayohusishana na chanzo cha tatizo.

Kama hujaelewa, rejea kwa nini MCC wamefukuza TAnzania na kuzuia fedha zao ambazo wwe unaziita mkwamo. Hautwezi kuendeza sera za kuganga njaa wakati tatizo lipo ila kwa maslahi ya wachache linalazimishwa kwa hila lifunikwe.

At least not with intellectuals!.
Hawataki kabisa kuongelea chanzo wakijua hakuna hoja. Hicho kinachoitwa mkwamo hakipo, kilichopo ni matatizo kwetu si MCC

MCC wapo sahihi jamani. Kuna jitihada za kuwabambikizia uovu MCC./EU/ Marekani ili kuficha ukweli kuwa madudu ya ZNZ ndicho chanzo. Na wala MCC hawakuchukua hatua bola kujiridhisha! la hasha!

Waangalizi wote wa uchaguzi kuanzia EAC/AU/C.Wealth/ EU/ Marekani wamesema uchaguzi wa Octoba 25 haukuwa na tatizo

Hao wote hawaonekani anatfutwa MCC/Marekani kama tatizo ili kusahaulisha umma kuwa kilichofanyika March 20 hata uchaguzi wa High school wasingefanya vile

MCC wamekataa na pesa zao, tulikubali vigezo vyao na kupata, safari hii hatukufikia wamegoma. Period.

Tatizo lipo CCM/Magufuli si MCC wala Marekani

Tukitengwa na dunia, si kosa la MCC na wala hatupaswi kabisa kulaumu Marekani
Tuwaulize Magufuli/CCM tumefikaje hapo si kutumia maneno ya mkwamo.

Hakuna mkwamo tumekwamishwa ili fulani awe Rais fulani awe makamu n.k

Hadithi zinatungwa kila siku kusafisha uozo. Uzalendo wa kuficha matatizo haupo, sasa wanahamisha goli wanasema Marekani mara waziri Nyaland, mara Lowassa mara, maseneta walikataliwa Ikulu n.k. ilimradi kusahaulisha umma kuwa ya ZNZ ndicho chanzo

MCC wapo sahihi 100%
 
Sisi tunaendelea kuwasikiliza tu! Hata huko nyuma nchi za ulaya zikidai uchaguzi ni wa haki na huru! Lakini sasa hv upinzani Zbar wameonyesha kukataa unafki wao na wao wanaanza kujipendekeza
 
Pitia hapa (Kwa hisani ya gazeti la Mwananchi)

MAONI YA MHARIRI: Ni vema kuepuka ukasuku suala la MCC

Jiridhishe mwenyewe kuwa MCC haikuwa na faida kwa Mtanzania!

Hoja hapa ni kuwa wale wanaosema MCC ni ukoloni, mbona hatukuwasikia wakati MCC ikitekeleza miradi hiyo? Huu ukoloni wanaosema umeanza lini? Baada ya 'kukatwa' katika mafao.

CCM/ Serikali ya Magufuli ieleze wananchi ukweli hata kama unauma

MCC hawana kosa kabisa, hawalazimishi ukoloni maana hata sasa hivi walipotuondoa hawajasema watatubana turudi. Wamegome pesa zao ambazo leo tunaziita za kikoloni

Tena yupo juha mmoja kasema, eti pesa za MCC hazina maana kwasababu makampuni yanayosimamia miradi ni ya Marekani hivyo pesa zitarudi Marekani. Huyu mwenzetu hajatueleza na barabara ya Horohoro wataondoka nayo?

Yaani hadithi za kubabaisha tuu ili wananchi wasiulize, CCM/Magufuli mnatupeleka wapi?

Wananchi waiofadika na majokofu, solar , barabara n.k. wasihoji kipi kina faida kwa umma, kuwalinda Rais/Makamu/ na katibu mwenezi kule kwa Jech au watu milioni 45

MCC na Marekani hawana kosa! Siyo wakoloni na tusifiche madudu ya March 20 kwa kuwatafuta wachawi. Wachawi wetu wapo miongoni mwetu!

Masilahi ya umma kwanza.

MCC wapo sahihi 100%
 
Pitia hapa (Kwa hisani ya gazeti la Mwananchi)

MAONI YA MHARIRI: Ni vema kuepuka ukasuku suala la MCC

Jiridhishe mwenyewe kuwa MCC haikuwa na faida kwa Mtanzania!

Hoja hapa ni kuwa wale wanaosema MCC ni ukoloni, mbona hatukuwasikia wakati MCC ikitekeleza miradi hiyo? Huu ukoloni wanaosema umeanza lini? Baada ya 'kukatwa' katika mafao.

CCM/ Serikali ya Magufuli ieleze wananchi ukweli hata kama unauma

MCC hawana kosa kabisa, hawalazimishi ukoloni maana hata sasa hivi walipotuondoa hawajasema watatubana turudi. Wamegome pesa zao ambazo leo tunaziita za kikoloni

Tena yupo juha mmoja kasema, eti pesa za MCC hazina maana kwasababu makampuni yanayosimamia miradi ni ya Marekani hivyo pesa zitarudi Marekani. Huyu mwenzetu hajatueleza na barabara ya Horohoro wataondoka nayo?

Yaani hadithi za kubabaisha tuu ili wananchi wasiulize, CCM/Magufuli mnatupeleka wapi?

Wananchi waiofadika na majokofu, solar , barabara n.k. wasihoji kipi kina faida kwa umma, kuwalinda Rais/Makamu/ na katibu mwenezi kule kwa Jech au watu milioni 45

MCC na Marekani hawana kosa! Siyo wakoloni na tusifiche madudu ya March 20 kwa kuwatafuta wachawi. Wachawi wetu wapo miongoni mwetu!

Masilahi ya umma kwanza.

MCC wapo sahihi 100%
Kwa kuongezea, ukweli ni kwamba serikali iliingia mkataba na MCC Mwezi February, 2008 kwa masharti husika kama tulivyojadili - juu ya haki, demokrasia, utawala bora... Tukumbuke kwamba Mwaka 2008 ilikuwa ni Miaka Saba kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, uchaguzi uliokaba demokrasia Zanzibari na haki (uchaguzi wa Muungano - Sheria ya mtandao).

MCC ililenga miradi kote Tanganyika (Muungano) na Zanzibar kwani katika maelezo yake wakati wa Kusaini mkataba husika na serikali, MCC walijadili changamoto kubwa juu ya hali ya 39% ya watanganyika kuishi below the national poverty line na 49% wazanzibari kuishi below the national poverty line. Makubaliano yakawa kwamba njia sahihi ya kupambana na umaskini iwe katika kulenga sekta kuu tatu kama ifuatavyo:

1. Nishati
2. Barabara
3. Maji

Serikali ya CCM ikaridhia masharti na makubaliano hayo. Na kama alivyojadili @Nguruvi3, miradi hii ilikuwa ni sehemu muhimu sana ya ilani ya uchaguzi ya chama cha Mapinduzi mwaka 2015, uchaguzi wa Muungano na nchini Zanzibar, miaka Saba baada ya mkataba baina na Serikali na MCC1, mkataba wa zaidi ya TZS Trilioni moja.

Miaka saba baadae, yani Mwezi November mwaka Jana(2015) baada ya CCM kupitia Jecha, kukaba demokrasia (uchaguzi wa Zanzibar) na CCM kubaka haki (Sheria ya mtandao), serikali ya Magufuli ilitoa tamko ambalo kimsingi ilikuwa ikijibu wasiwasi wa MCC kuhusu hali husika. Tamko la Balozi Sefue lilionyesha wazi kwamba Serikali ya CCM ilitambua wasiwasi wa MCC kwamba masharti yaliyokubaliwa baina yake na MCC yalikuwa yakipuuzwa.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, alitolea ufafanuzi suala hilo alipozungumza na gazeti
La Nipashe Novemba 29, 2015, akisema kuwa "Serikali haina wasiwasi kuhusu mashariti ya MCC juu ya Zanzibar kwani yatafanyiwa kazi kabla ya bodi ya mcc kukatana na kutoa uamuzi. "

Swali kwa watetezi wa serikali ya CCM dhidi ya suala hili - Je Balozi Sefue hakuwa anajua kinachoendelea?

Cha ajabu zaidi ni kwamba baada ya mcc kutoa uamuzi wake juzi, Waziri wa Fedha akaja na kauli nyingine kwamba Serikali ilishajua kuhusu uamuzi wa MCC na hivyo tayari ilishajiandaa kukabiliana na uamuzi huo. Ajabu nyingine ni pale waziri wa mambo ya nje, mwanadiplomasia aliyebobea alipotoa malalamiko na shutuma dhidi ya MCC kama vile wameshtukizwa na wameonewa.

Swali linalofuatia ni je, kauli za Sefue, Mahiga na Mpango zinatupa ujumbe gani zaidi ya ubabaishaji?

Suala la Sheria ya Mtandao ya mwaka 2015. Ukweli ni kwamba MCC ilisainiwa mwaka 2008 na moja ya masharti ilikuwa ni usimamizi wa haki za wananchi. Hii ilikuwa ni Miaka Saba kabla ya Sheria ovu ya mtandao kupitishwa na bunge ambalo kambi ya upinzani ilisusia kikao, mwaka 2015. Kimsingi Sheria hii ilipitishwa na wabunge wa ccm peke yake. Miezi michache baadae mwaka huo huo Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, akasaini muswada husika kuwa Sheria.

Kwanini leo tushangae MCC to combine maamuzi Yao dhidi ya Sheria ya Mtandao (uchaguzi mkuu wa JMT) na ubakaji wa demokrasia (uchaguzi Zanzibar) wakati ukweli ni kwamba masharti haya yalikubaliwa baina na MCC na serikali ya CCM katika wakati mmoja (2008) na kuja kukiukwa na serikali hiyo hiyo ya CCM miaka saba baadae kwa wakati mmoja (2015)?
 
Changamoto siyo hela. Angalia mbele ujue chanzo cha tatizo. Huwezi kumlaum nzi kujaa ndani ya nyumba yako ambayo umejaza mizoga.

Tujadili ubakaji wa Demokrasia na utawala mbovu Tanzania kwa mfano halisi wa yaliyotokea Zanzibar na athari zake kwa taifa ambapo kupoteza supportive friends in moja tu ya athari.

La pili tujadili matumizi mabaya ya sheria hila na gandamizi. Cyber Crime Law ni moja wapo na zingine pamoja na athari zake kwa upana kwa Watanzania huru. Kuwakamata watu na kuwaswekwa ndani huku ukiharibu hata vitendea kazi vyao kwa kosa ambalo halipo. Ni upumbavu wa hali ya juu, na unaoongoza duniani kumzuia mtu asijumulishe alama za matokeo yake ya mitihani ambayo tayari yameshasahihishwa na amerudishiwa. Vinginevyo hakuna sababu ya kuwafundisha watu helsabu za kujumlisha kama hata kujumlisha hawaruhusiwi. Na sheria zingine kama hizi na zinachozalisha katika taifa letu kwa watu binafsi na taifa kwa ujumla.

Hii biashara ya MCC ni moja ya matokeo hayo. Acha kutulazimisha tujadili matokeo ya tatizo tulilonalo. Tujadili chanzo cha tatizo na tiba yake. Hakuna kitu utafanya chenye kuleta tija katika jamii yenye utawala gandamizi, usio wa haki na usiojali raia.

Kulazimisha ambako ccm wanafanya kwamba eti kosa ni la wafadhili sasa tujadili mbadala, ni upumbavu. Ni sawa na kulazimisha kubeba maji kwenye kikapu.

Toa hoja zako juu ya chanzo cha matatizo na athari zake kwa upana kwa Watanzania na taifa lote kwa ujumla ambao MCC ni moja ya matokeo hayo. Kinyume cha pale, NYAMAZA.
Mkuu nadhani kwanza tuwe wakweli na nafsi zetu wenyewe maana ukweli utatuacha huru. Kuhusu Ubakaji wa Demokrasia kama ulivyoeleza hapo juu halafu tutazame sababu walizotoa MCC kama ndio tatizo sio fedha.

1. Kama unakumbuka hakuna mwaka ulokuwa na Ubakaji mbaya wa demokrasia na tulipoteza roho za watu kama mwaka 2000 wakati wa uchaguzi wa Zanzibar. Hawa wakimbizi wote unaowaona nchi za nje ni kutokana na uchaguzi ule, sasa ilikuwaje hawa MCC ndio kwanza wakaingia mkataba na serikali ya Mkapa baada ya kuanzishwa kwake mwaka 2004 hadi Bush akapiga kambi nchini Tanzania kwa majisifu makubwa kwamba hajawahi kupokelewa nchi yoyote kama alivyopokelewa Tanzania! Msije danganywa kwamba imeanza majuzi tu alipoingia JK maana kinachobadilishwa ni majina na malengo!

2. Ni wakati huo huo pia hata kabla ya kuwepo sheria hii ya Cybercrime, waandishi wengi walitiwa ndani, magazeti kufungiwa pasipo kifungu cha sheria ama wengine kupoteza maisha yao hatukusikia cha MCC wala wapuuzi wengine wakiinua sauti zao kukata misaada. katika mambo yote JK kidogo alijipatia sifa mwanzoni kwa kuwapa Uhuru japo kidogo waandishi wa habari na kina siye wasema hovyo! Hii Jamii forums, haikuwa hivi hata kidogo waulize wenyewe kina Maxence.

3. Kuna sababu kubwa zaidi ilopitishwa na MCC mwaka 2012 juu ya miradi yake ili kupunguza Corruption nchini, Tanzania tulipewa mikopo kwa sababu hiyo Je, Rushwa ilizidi kuongezeka nchini au laa! Na kwa nini hawakukata misaada yao! haya sijui tukatapeliwa na Vyandarua vya kuzuia Mbu vya mama Bush, sijui kwa asilimia ngapi Malaria imepungua nchini na yeye kaingiza ngapi! nadhani vifo viko pale pale au vimeongezeka wakati hawa watu wanaijua dawa ni kupambana na mbu wenyewe kama wanavyofanya makwao wakimwagilia madawa!

4. Haya majuzi tu mwisho mwisho wa awamu ya JK aliptisha Cybercrime. Hao MCC walisema wanaifungia misaada Tanzania huku wakisutasuta kuikata kwa sababu ya RUSHWA japo EU tayari walishanza kukata, badala yake MCC wameendelea na mkataba mwingine wa Tanzania compact II wakati nchi ipo kileleni kwa Rushwa! Leo Magufuli kawashughulikia mafisadi na Rushwa kulingana na matakwa ya mkataba wao ndio kwanza wanakuja na sababu za Cybercrime ilopitishwa na Kikwete!. Je, inaingia Akilini hii kweli?

Swali la kujiulza zaidi ni hili:- Ni lini Zanzibar wamewahi kuwa na uchaguzi wa wazi, haki ama unaowapa wananchi wake mamlaka kamili ya kuchagua viongozi wake? Lini CCM walikubali kuweka uwanja sawa kwa vyama vyote pasipo kujipangia Ushindi kwa nguvu zote iwe visiwani au Bara maana sikumbuki na sidhani kama upo uchaguzi Zanzibar toka 1995 hadi kesho na hata nikirudi mwaka 1958! Sasa kwa nini siku zote wasiikate misaada hiyo kutokana na sababu zao isipokuwa sasa hivi wakati sababu ni zile zile toka 1995 - WHY NOW?
 
UKAWA, hata hoja isiyo na mashiko mtaikomalia maana kwa sasa hamba sera, kwani hela ya MCC, imetoka kwa walipa kodi, hata title yako ni kichekesho, UKAWA huchukua vilaza kuandika.
Mada kubwa imekumeza nenda kapike
 
T


Unfortunately, tutaendelea kujadili pesa za wenyewe kwa miaka zaidi ya 30 ijayo kwani tuna deni la nje ambalo sasa ni zaidi ya TZS Trilioni 29. Kwa miaka kumi ijayo, kati ya 10-15% ya mapato ya serikali yatakayotokana na kodi za wananchi yataenda kwa "wenyewe" huko nje.

Rais Magufuli atatumia muda wake na fedha nyingi zaidi za walipa kodi kuwalipa "wenyewe" huko nje kuliko kuwekeza katika miradi ya maendeleo kwa ajili ya walipa kodi.

Miaka kati ya mitano na nane kutoka sasa, kuna dalili kwamba tutaingia katika debt crisis kutokana na fedha za wenyewe. Kwahiyo tuombe uzima na tuwe tayari kujadili kwa kina na kwa mapana zaidi kuliko sasa kuhusu fedha za 'wenyewe' huko mbeleni. Lakini ukipenda, unaweza kushiriki mjadala huu mapema zaidi ili usije kuwa mtu wa kushtukizwa na mgogoro mkubwa huko mbeleni.
Naona ndiyo anachokifanya wanafunzi hawapati mikopo
 
Back
Top Bottom