LGE2024 Msimamizi wa Uchaguzi Dodoma: Marufuku viongozi kujipitisha kwenye vituo vya kupigia kura

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
1,419
3,622
Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dk. Frederick Sagamiko ameonya tabia ya viongozi wa vyama vya siasa kujipitisha katika Vituo vya Kupiga Kura wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima.

Dk. Sagamiko amesema hayo mkoani Dodoma leo alipokuwa akizungumza na Viongozi wa Vyama vya Siasa vinavyoshiriki uchaguzi huo utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu nchini kote na kuongeza kuwa kufanya hivyo ni kukiuka taratibu na kanuni za uchaguzi.

“Siyo kila Kiongozi wa chama cha siasa anatakiwa kuwepo kwenye Kituo cha kupigia kura, kuna watu wanataka kwenda kwenye kituo A hadi Z, nisingetamani kutengeneza taharuki wala migogoro tarehe 27. Sitaki kusikia tarehe 27 napigiwa simu nimezuiwa kuingia kwenye kituo cha kupiga kura.” Alisema Dk. Sagamiko.
1732204947215.png
 
Marufuku inawahusu viongozi wa upinzani CCM hawapo kwenye marufuku hiyo kwa kuwa wao ndio tume yenyewe kasaro ni kutovaa magwanda ya kijani.
 
Kwani kujipitisha kumekatazwa na kanuni ya ngapi ya uchaguzi?
Punguani huyo ukimuuliza atakwambia ana masters shenzi kabisa
 
Back
Top Bottom