Amemsifia akasema nini? Tukijua amemsifia nini ndio tunaweza kusema ni sifa asizostahili au la!
Kweli watz tubadilike,yani inakua sifa za marehemu akiwa hai mbaya,akifa oooh alikua mzuri,wakati ule mlimsema sana JK leo kamaliza muda wake amegeuka mzur?we jamaa naona chuki binafsi inakutafuna. jk anastahili sifa aliyopewa na msigwa. nenda tena shule ya propaganda
Hivi upinzani msimamo wao ni upi? Kuanza kumkumbuka Kikwete mapema hivi ni kujichimbia kaburi.
Msigwa kuanza kumsifia Kikwete bungeni inanipa picha kuwa upinzani unakufa mbele ya Magufuli. Mnashindwa kujenga hoja, mangapi Kikwete mlimsema leo tena mnamkumbuka. Upinzani ovyo kabisa hamna msimamo. Acha CCM watuongoze tu
Ukweli unatabia moja,haufi!
"Mimi nasikitishwa na jambo moja, tumefika hapa kutokana udhaifu wa Rais Kikwete, uzembe wa bunge na wabunge na tumefika hapa kutokana na upuuzi wa CCM, nasema hivi nina ushahidi.” Mnyika (2012)
Ni kweli si dhambi kuanza kumsifia JK lakini kwa jinsi walivyomkataa JK leo wanamkumbuka. Ni unafiki.
Amina.Nilishasema zamani kabisa kwa upinzani wa nchi hii bora ccm itawale milele mpaka pale nchi itakuja kupata upinzani wa kweli hata ikifika 2050
Sasa mbona wengine wanamponda kwa kusaini sheria ya mtandao ambayo wanadai inakandamiza uhuru wao?Kama kwa uhuru wa habari Kikwete ana kila sababu za kupewa sifa mkuu
CHADEMA ni kikundi cha wafanyabiashara wa siasa....nilikuaga huko enzi za Zitto na Babu Slaa....nikang'amua mapema...nikatoka kabisa kwa wazungusha mikono
Kinachopondwa sio tu kusaini ile sheria ila kusaini bila kurekebisha kwa baadhi ya vipengele ambavyo haviko sawa na baadhi ya maandishi namna yalivyokaaSasa mbona wengine wanamponda kwa kusaini sheria ya mtandao ambayo wanadai inakandamiza uhuru wao?
Jibu langu lingekuwa na maana sana kwako laiti ungejua kilichoandikwa na huyo ndugu niliyemjibu! Yeye anasema JK ameleta uhuru mpana kwa wanahabari.Kinachopondwa sio tu kusaini ile sheria ila kusaini bila kurekebisha kwa baadhi ya vipengele ambavyo haviko sawa na baadhi ya maandishi namna yalivyokaa
Mfano: inatamka kifungo kisichopungua miezi 6 au faini isiyopungua mil 2 au vyote kwa pamoja
Hapa ukiangalia kwa makini utagundua inaelezea kiwango cha chini tu cha adhabu bila kuweka ukomo wake yaani ISIYOZIDI AIDHA MIEZI KADHAA AU MILIONI KADHAA.
Kweli hutanijua maana mimi sio wa kule kwenuMbona hatukujui we mganga njaa?
Sasa mbona wengine wanamponda kwa kusaini sheria ya mtandao ambayo wanadai inakandamiza uhuru wao?
Ok, sikusikia aliongea nini. Ila kama kalinganisha kitu kimoja tu cha bunge kuoneshwa live hapo hajakosea.Akichangia bungeni alitamka bila kuficha awamu hii ya tano inataka kuminya uhuru wa habari wakati awamu ya nne ilikuwa jasiri na kurusha live bunge tunamkumbuka jk kwa kuwa jasiri wa uhuru wa habari.....
Ilibidi nicheke....leo mnamkumbuka tena. Wakati jamaa alikuwa anawasigina mkatoka bungeni kila uchwao. Msigwa uwe na msimamo
Kikwete alikuwa kiongozi mbovu kabisa katika historia ya Tanzania. Hilo halina ubishi na ndio msimamo wangu. Lakini pamoja na ubovu wooooote, sio kwamba hakuna areas ambazo unaweza kumsifia! Zipo. Na mtu akimsifia kwenye areas hizo hatakuwa amefanya makosa. Ndio maana nikasema ni muhimu kujua amesifiwa nini?Kweli watz tubadilike,yani inakua sifa za marehemu akiwa hai mbaya,akifa oooh alikua mzuri,wakati ule mlimsema sana JK leo kamaliza muda wake amegeuka mzur?