Msiba wa Rais Mkapa: Kwa nini Ubalozi wa UAE Tanzania haujashusha bendera nusu mlingoti?

... kwani mabeberu wakiongozwa na beberu mkuu nao wamepeperusha nusu mlingoti?
 
Maelekezo yaliyotoka ni kwa Balozi zetu zote Duniani, sio balozi zilizopo Tanzania. Kila nchi ina maamuzi ya bendera yake, ndiyo maana Uhuru akatangaza kuhusu Bendera ya Kenya kupepea nusu mlingoti. Nchi ambazo hawajafanya hivyo haituhusu.

Kila mtu anadeal na bendera yake
... umenena vyema! Ubalozi na eneo linalozunguka jengo la ubalozi kimsingi ni nchi ya kigeni na ndio maana hata mhalifu akikimbilia ubalozi wa nchi ya kigeni kuna taratibu za kumkamata kwani inahesabiwa yuko nchi nyingine.

Kwa hiyo mleta mada, usiwaingilie UAE (na nchi nyingine zote) na mambo yao. Wenye hiari ya kufanya hivyo watafanya kwa maelekezo kutoka nchi zao; wasiotaka (nchi husika) ni hiari yao pia wala sio kosa and in general huo msiba wala hauwahusu! Balozi zinazotakiwa kupeperusha nusu mlingoti ni balozi za Tanzania katika nchi za kigeni hilo linawahusu moja kwa moja.
 
Muongozo wanapata toka wizara zao za mambo ya nje. Watashusha kama kwao wakifiwa na serikali yao itasema washushe nusu mlingoti. Hawapokei maagizo toka wizara ya mambo ya nje ya tanzania.
... sawa sawa kabisa.
 
Serikali na Wizara ya mambo ya nchi za nje ulitoa mwongozo juu ya suala la kushusha nusu mlingoti bendera zote kwa Balozi zote za nie zilizopo hapa Tanzania kutokana na Msiba huy wa kitaifa tulio nao.

Ubalozi wa Falme za Kiarabu hapa Tanzania bendera zake bado zio juu kabisa toka msiba wetu wa Kitaifa utokeee.

Ina maana Wizara ya Mambo ya Nchi za nje haukutoa mwongozo kwa huu Ubalozi au kuna kitu ambacho hatukielewi?
Jambo moja muhimu kujua ni kwamba, mahali palipo na 'jengo la ofili ya ubalozi' wa nchi yeyote panahesabika ni sehemu ya nchi hiyo. Hivyo basi ubalozini ni kama nchi: kushusha nusu mlingoti ni lazima uwe utaratibu wa nchi husika ndio umesikia kila palipo na ubalozi wa Tanzania washushe bendera nusu mlingoti.
 
Wapemba ni ndugu zao wa damu kabisa!
Umenikumbusha mbali sana enzi zie. Hawa jamaa walimtumia sana Komandoo kujaribu kumtikisa Mkapa wakati yuko mdarakani.

Walimchochea Komandoo na kumhadaa mpaka Komandoo akaiunga ZNZ kwenye jumuia ya nchi za kiarabu. Nakumbuka Mwalimu alikuwa hajafariki bado, Komandoo akapigwa mkwara na kupewa masaa 24 awe ameitoa ZNZ kwenye hiyo jumuia 😂😂😂😂😂

Mwalimu alipofariki tu, Komandoo akatuma wazee wa ZNZ wamletee salamu Mkapa kuwa anabadili katiba, kufuta ukomo wa muda wa madaraka ili Komandoo aendelee madarakani. Tena kwa vitisho, Mkapa akigoma, ZNZ wanavunja muungano na kujiunga na UAE 😄😄. Mkapa akasimama kidete.

Hao UAE wana roho kama za wajumbe wa CCM.
 
Serikali na Wizara ya mambo ya nchi za nje ulitoa mwongozo juu ya suala la kushusha nusu mlingoti bendera zote kwa Balozi zote za nie zilizopo hapa Tanzania kutokana na Msiba huy wa kitaifa tulio nao.

Ubalozi wa Falme za Kiarabu hapa Tanzania bendera zake bado zio juu kabisa toka msiba wetu wa Kitaifa utokeee.

Ina maana Wizara ya Mambo ya Nchi za nje haukutoa mwongozo kwa huu Ubalozi au kuna kitu ambacho hatukielewi?
Ni lazima kushusha?
 
Kuteremsha bendera ubalozini ni nchi yake itangaze rasmi kuwa inaombeleza ndio balozi atateremsha bendera.mnakuwa mazwazwa hamuelewi kulaumu tuu
 
Labda sio taratibu zao, na kwani bendera yao inatuhusu nini?! Muwaache msijewaletea balaa bure.

Uko sahihi mkuu. Wakati mwingine ni vema kuachana na petty issues. Huyu jamaa hata kama UAE wangeshusha bendera, huenda angeuliza mbona serikali haikufunga sehemu za starehe kwa sababu ya msiba wa taifa!!
 
Maelekezo yaliyotoka ni kwa Balozi zetu zote Duniani, sio balozi zilizopo Tanzania. Kila nchi ina maamuzi ya bendera yake, ndiyo maana Uhuru akatangaza kuhusu Bendera ya Kenya kupepea nusu mlingoti. Nchi ambazo hawajafanya hivyo haituhusu.

Kila mtu anadeal na bendera yake
Umenena vema Mkuu. Tatizo tulilonalo ni maarifa na ujuaji
 
Serikali na Wizara ya Mambo ya Nchi za nje ulitoa mwongozo juu ya suala la kushusha nusu mlingoti bendera zote kwa Balozi zote za nie zilizopo hapa Tanzania kutokana na Msiba huy wa kitaifa tulio nao.

Ubalozi wa Falme za Kiarabu hapa Tanzania bendera zake bado zio juu kabisa toka msiba wetu wa Kitaifa utokeee.

Ina maana Wizara ya Mambo ya Nchi za nje haukutoa mwongozo kwa huu Ubalozi au kuna kitu ambacho hatukielewi?
Itakuwa mpandisha bendera hajaambiwa labda.
 
Back
Top Bottom