Msiba wa Rais Mkapa: Kwa nini Ubalozi wa UAE Tanzania haujashusha bendera nusu mlingoti?

businesslink

Senior Member
Mar 20, 2019
129
114
Serikali na Wizara ya Mambo ya Nchi za nje ulitoa mwongozo juu ya suala la kushusha nusu mlingoti bendera zote kwa Balozi zote za nie zilizopo hapa Tanzania kutokana na Msiba huy wa kitaifa tulio nao.

Ubalozi wa Falme za Kiarabu hapa Tanzania bendera zake bado zio juu kabisa toka msiba wetu wa Kitaifa utokeee.

Ina maana Wizara ya Mambo ya Nchi za nje haukutoa mwongozo kwa huu Ubalozi au kuna kitu ambacho hatukielewi?
 
Kidiplomasia nilidhani ni nchi zote tumbe kuna baadhi ya nchi zinakuwa exempted kwenye haya mambo.
 
Maelekezo yaliyotoka ni kwa Balozi zetu zote Duniani, sio balozi zilizopo Tanzania. Kila nchi ina maamuzi ya bendera yake, ndiyo maana Uhuru akatangaza kuhusu Bendera ya Kenya kupepea nusu mlingoti. Nchi ambazo hawajafanya hivyo haituhusu.

Kila mtu anadeal na bendera yake
 
Muongozo wanapata toka wizara zao za mambo ya nje. Watashusha kama kwao wakifiwa na serikali yao itasema washushe nusu mlingoti. Hawapokei maagizo toka wizara ya mambo ya nje ya tanzania.
 
Ya PALESTINA pale karibu na njiapanda ya Muhimbili au Don Bosk Upanga ipo mawinguzi siku zote
 
Mwisho mtawakamata kwa kutokwenda msibani, jamani mkifiwa muwe wavumilivu, sio kila mtu anaelewa uchungu wa majobzi yenu.

Mwisho mtaanza kuwakagua kama wamelia au la, msiba wenu sio wao.

Waacheni watu waishi maisha yao.

Mkuu umeielezea vyema dhana nzima ya kufiwa.

Kumfukuza au kumzuia mwombolezaji kufika nayo inaingia huko humo. Hayana tija wala afueni yoyote kwa mfiwa wala marehemu.

Waswahili wanasema vyema: kuwa na "subira."
 
Back
Top Bottom