Msiba unapovuta watu kuliko kuuguza

ni tabia mbaya sana wengine ndio wanakaa kupanga kima cha chini cha kutoa mchango wakati wangefanya hivyo wakati marehemu anaumwa angeweza kupata matibabu mazuri
pia focus yao inakuwa kufanikisha mazishi ya kifahali bila kujali familia ya marehemu kama aliiacha!
 
Ndio iko hivyo.

Na kuna watu inafikia mpaka kumnyanyapaa Mgonjwa.

Yaani hata inapotokea kwenda muangalia mgonjwa Hospitalini, mgonjwa anaomba ageuzwe utaona watu wanakaa mbali na mgonjwa.

Mfano hai mimi rafiki yangu mmoja Dada ake alikuwa anaumwa, sasa tumeenda kumuangalia Mgonjwa Hospitalini, watu wa karibu wamejaa kumzunguka Mgonjwa.

Mgonjwa ameomba ageuzwe basi huwezi amini watu wote pale wamejikausha, ikabidi mimi niwaombe wanipishe nipite mbele nilipofika mbele naanza kumgeuza Mgonjwa rafiki yangu nae akasogea, tukasaidiana kumgeuza.

Basi huwezi amini kazi yetu ilikuwa kumgeuza mgonjwa, hazifiki dakika tano Mgonjwa anaomba ageuzwe tena.

Kilichonikera zaidi kuna mademu wapo wanauza sura tu, mpaka uwaambie hebu mfunikeni vizuri Mgonjwa tunataka kumgeuza.

Yaani hawana hata msaada.

Mbaya sana kumnyanyapaa Mgonjwa, kumbuka ugonjwa hauna mtu mmoja.

Inaweza kukutokea ugonjwa wewe uliemzima siku yoyote
 
Dah umenikumbusha mbali sana ,yaani watu wamebadilika sana miaka ya leo
 
Binadamu sasa wa napenda kutatua tatizo sio kutafuta tatizo na hapo msibani wengi utawaona siku ya kuzika tu baada ya hapo kila.mtu yupo busy aliyekwenda amekwenda
 
Binadamu wamekuwa sio wakweli, mtu anaweza kukuambia anaumwa ukimpa hela anaenda kunywa bia, kwa hiyo hata kama mtu anasema ukweli ni vigumu watu kumuamini, kwa hiyo ikitokea amefariki ndiyo wanajua ni kweli na wanasaidia kwenye mazishi

Acheni visingizio nduguyo akilazwa hospital ndio anaenda kunywa beer? Looh
 
Kama majira kwa mwaka yanabadilika, hata haya maswala nyeti lazima yabadilike.
Binadam tumekoswa utu na uthamani hata kidogo.
 
kuuguza sio sawa na kuzika
kuzika ni mara moja ila kuuguza inachukua hata mwaka mzima au miaka
Umenikumbusha kuna msiba mmoja mchungaji aliwashushua ndugu, ilikuwa hivi: huyo marehemu alikuwa ameugua muda mrefu kama miezi 6 hivi. Sasa kwenye mazishi wakawa wanaitana mara mwenyekiti wa kamati ya mazishi aje kutoa shukrani. Wakati wa ibada, mchungaji akasema "huyu marehemu aliugua muda mrefu,nimesikia kuna mwenyekiti wa kamati ya mazishi, lakini sijasikia mwenyekiti wa kamati ya kumuuguza marehemu, je thamani ya utu huonekana mtu akishafariki tuu?"
BOB LUSE
 
Hilo.ndio tatizo! hata mimi mgonjwa niliyemuuguza kufika mkoani.nikakuta kamati kibao.mimi hata moja simo!.
 
Unajua watu uogopa kwa sababu ya kuhisi kuwa marehemu anakuona kama hujamchangia au kwenda kumzika... mtu akifa unahisi anaweza kukutokea mahali popote
 
kweli mkuu.hao wauza sura nao wapo.wanaenda kuweka ushahidi kuwa walifika hospitali na kueneza umbeya wa maradhi ya mgonjwa bila msaada wowote
 
Binadamu sasa wa napenda kutatua tatizo sio kutafuta tatizo na hapo msibani wengi utawaona siku ya kuzika tu baada ya hapo kila.mtu yupo busy aliyekwenda amekwenda
kweli mkuu ndio maana siku ya kuzika kunakuwa na nyomi.wakizika wamemaliza kazi.wanasubiri msiba mwingine.
 
Kama majira kwa mwaka yanabadilika, hata haya maswala nyeti lazima yabadilike.
Binadam tumekoswa utu na uthamani hata kidogo.
sio utu hata aibu hatuna! sijui ndio uzungu pori!
 
Unajua watu uogopa kwa sababu ya kuhisi kuwa marehemu anakuona kama hujamchangia au kwenda kumzika... mtu akifa unahisi anaweza kukutokea mahali popote
Kumbe watu wanachanga kuogopa kichapo cha marehemu
hapana chezea NSYUKA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…