Mshahara anaolipwa Mkwasa unaleta picha gani kwa Watanzania?

Kwamhuzi

JF-Expert Member
Nov 15, 2014
1,762
401
Nimesikia mshahara wa Mkwasa ni Millioni 28.Kikwete Rais wetu wa Tanzania anapata Millioni 32.

Kwa mlinganisho huo tu ni wazi kuna jambo haliko sawa kabisa.Niseme wazi,kwamba simuonei Mkwasa wivu, lakini nirudie tena kuna jambo haliko sawa.

Inasemekana mshahara anaopata Mkwasa ni ule aliokuwa anapata kocha mzungu aliyeondoka, sawa lakini there is something I miss.

Tunapaswa kuelewa kwamba mshahara unatakiwa ku-reflect umuhimu na unyeti wa what one is going to deliver. Ndio michezo ni muhimu,lakini sidhani kama ni priority kwa nchi yetu kwa sasa.

What is wrong with us, watoto wetu wanapata elimu duni kwenye shule za kata na hakuna mkakati wowote wa kuziboresha, huduma za afya ni mgogoro, kilimo chetu ni duni na miundombinu yote ya kukiboresha ni hohehahe, watoto wetu hawana madawati, wanakaa chini, message gani tunapeleka kwa wananchi wetu.

Message gani pia tunapeleka kwa wafanyakazi wengine, kwamba kazi zao sio za muhimu kama ya Mkwasa na kwamba ndiye atakaye deliver the most kuliko wafanyakazi wengine wote?

Kwanza michezo ni starehe tu ingeweza kusubiri kwanza tukashuhulia issues za msingi kwa wananchi wetu,than tuka-invest kwenye michezo kama ni lazima baadae hali yetu ikiwa nzuri.

Jamani hivi kweli starehe ni muhimu kuliko maendeleo ya wananchi wetu.Hapana,we have our priorities upside down,ni lazima tujichunguze upya.

There is something seriously wrong with our upstairs.
 
Nani alikuongopea kuwa tofauti ya mshahara wa Rais wa JMT na Mkwasa ni tofauti ya 4M ? Ina maana mabosi wake Mkwasa (kina malinzi et al ) wanalingana na mkulu wa kaya mshahara?

Kaa chini ujipange na upya mkuu hapa ni JF na sio FB kwa watoto.

Mtanisamehe mliofunga , ila kwa wale kina "kobe" wenzangu na mimi nadhani tupo pamoja.
 
Wacha alipwe hata milioni50, ila watanzania tunataka kushiriki afcon 2017, worldcup 2018. Akishindwa kutuvusha tutamfukuza.

Hapa ndipo huwa nafurahishwa na "soka" la Tanzania, hata kama kocha akifanya vizuri shida ikawa uzembe, kutotaka kufundishika kwa mchezaji, lawama zinakuja kwake na anafukuzwa, then anakuja mwingine.

Ni kitu kizuri system hii iko kwa wachezaji tu, ila ingekuwa katika elimu, sijui!
 
Dogo shilingi milioni 28 zinakuumiza sana? Rais kulipwa 32 isikuumize kichwa.

Kuna watumishi wa serikali wanalipwa mshahara mkubwa kuliko wa rais kama ulikuwa hujui.

Baadhi ya wakurugenzi wa mashirika ya umma mashahara wao ni mkubwa kuliko wa Rais.
 
Nani alikuongopea kuwa tofauti ya mshara wa vasco da gama na mkwasa ni tofauti ya 4M ? inamaana mabosi wake mkwasa (kina malinzi et al ) wanalinga na mkulu wa kaya mshahara? kaa chini ujipange na upya mkuu hapa ni JF na sio FB kwa watoto .
Mtanisamehe mliofunga , ila kwa wale kina "kobe" wenzangu na mimi nadhani tupo pamoja.

Kwanini Unapenda Kuwakejeli Wakristo Kiasi Hiki? au Mwenzetu Unainama Kama Siyo Kuinamishwa Kweli Kama Afanyavyo Huyo Kobe?
 
Acha atafune, mzawa zimeenda nje mno huku tukibakia kichwa cha mwendawazimu!
 
Kwani walimu wa shule zetu wanatofauti gani na huyo kocha,sisemi kocha alipwe kama kocha ila serikali iwajali na makocha hawa wa watoto wetu
 
Kwamhuzi

Huu ni wivu wa kupindukia. Umeandika haya kwa sababu ni mmakonde mwenzetu au nini, mbona ukulalamika alipokuwa akilipwa kiasi hicho mzungu ambaye hakuipeleka timu yetu popote?
 
Last edited by a moderator:
Mtoa uzi una wivu balaa. Binafsi nimefurahi sana Mkwasa kulipwa hiyo hela. Ni zamu yake kula, namshauri Mkwasa ajitahidi kudumu angalau miezi sita ili akitoka atoke na kamtaji flani hivi. Hongera Malinzi
 
Back
Top Bottom