Msekwa Atoboa siri ya Butiama

Kwa walio msakama Seif nawapa pole ,maana Seif sio tatizo jamani ,tatizo la CCM kwa Zanzibar ni kupoteza mamlaka na kuchuliwa na upinzani ,hilo ndio tatizo.

Seif ni kigezo tu na yeyote atakaewekwa badala ya Seif basi hali itakuwa ile ile au worse kuliko inavyofikiriwa,CCM imeshindwa mara zote tatu na itaendelea kushindwa mpaka mwisho wa Dunia ,maana waliochoka na CCM sio CUF viongozi bali waliochoka na CCM ni wananchi kwa ujumla hizi sababu za kusema, CUF ni chama cha wapemba, mara cha waaarabu mara cha kidini mara kinapinga mapinduzi hazina mshiko kabisa ni hawa viongozi wahafidhina kujaribu kujipa moyo labda watapata sapoti kutoka mataifa ya nje lakini hakuna wanachokipata afuweni yao ni pale CUF wanapolegeza kamba wakasema haya na tukaeni tujaribu kupanga basi ndio hapo tu.

Lakini kwa kweli wananchi wote wa Zanzibar CCM imewafika kooni na imeshawachafua roho wanaitapika asubuhi na jioni ,maana ikiwa Mh.Karume alisema kura yake na ya Mkewe tu zinatosha kumfikisha Ikulu basi hapo.

Mnatakiwa mfahamu kuwa CCM imeshapoteza kila kitu haina chochote zaidi ya ubabe na mapolisi na majeshi na ndio kama mlivyoona ubabe wao walipofika Butiama na kusema kama mnataka mseto basi turudishieni ASP yetu ,hapo ndio kabisa waliponiacha hoi maana kama NEC nao wangechemka kwa dharau hio wakasema rudini na ASP yenu na CCM itabaki kama ilivyo, mbona ingelikuwa aibu ,yaani kama Mwenyekiti angelikuwa ni Nyerere wangeondoka Butiama na kadi za CCM wakaziacha hapo hapo yaani wangelivuliwa uanchama ,angewauliza suali moja ni nani anaekubaliana na maneno hayo ya mheshimiwa aliesema kuwa kama utaundwa mseto warudishiwe ASP..hapo tu ndio ungelikuwa mwisho wa Karume dynasty na watu wakaendelea na yao ,lakini wapi Muungwana hana mtaji wa kuongoza CCM kwa kishindo.Ndio ikabidi aone heri apendayo Mungu.
 
Muafaka wa CCM na CUF kuhusu Zanzibar ni mgumu kutekelezeka bila kufanya marekebisho ya msingi kuhusu Mwungano wenyewe na katiba yake ikakubalika na wananchi wa pande zote mbili. Mtazamo wangu ni kuwa katiba kama ilivyo imee kimoja kinachotawala pande zote za Mwungano.

Je rais wa Zanzibar akitoka CUF akiingia kwenye baraza la mawaziri, kama katiba inavyosema, je atayakubali maamuzi yake endapo yatakuwa kinyume na sera ya chama chake? Hivyo hata hiyo serikali ya mseto kikatiba ngumu kutekelezeka bila kwanza kuibadili.

Katiba inabidi iweze kucover all scenarios ambazo nchi inaweza kukumbwa badala ya kuibadili kulingana na hali. Je Mwungano wetu ambao unakubalika na kila chama cha siasa unaueleza vipi kiserikali? Serikali mbili kuelekea serikali moja au serikali mbili kuelekea serikali tatu? Wakati umefika wa kuyakabili haya maswala magumu na kutolewa uamuzi ili vyama viweze kutekeleza sera za kuendeleza wananchi badala ya kuulinda Mwungano.

Tatizo jingine kubwa ni la kutoaminiana kabisa kati ya CCM na CUF. Nakumbuka wakati wa kampeni za 1995 msemaji wa CUF akiwa TVZ alitaka watu wachague CUF kwa vile hakipokei amri toka bara!! Sasa mimi raia wa kawaida nakumbuka haya je wenyewe si ndo wameapiza iwe na iwe CUF haoni ndani. Labda aliteleza ulimi wakati mbaya kwani baada ya hilo aliondolewa kimya kimya. CCM nao kujibu mapigo wamekipakizia CUF kuwa cha waarabu na kuikchagua ni kumrudisha Sultani. Propaganda hizi zinapopandwa kwa wananchi wa kawaida ni hatari na hazifutiki kirahisi.

Tukumbuke jirani zetu waliposhikiana mapanga walisahau kuwa huyu ni jirani niliyeomba kwake chumvi nami nikampa maharage alipokosa mboga. Chonde chonde wanasiasa wetu msitufarakanishe kwa furaha zenu. Twajua wote hamtakaa hapa bali nje na familia zenu. CCM wakumbuke kuwa kura ya maoni kuhusu vyama vingi ni 20% tu walikubali. Pamoja na hiyo CCM, kwa kuogopa kuondoka kwa kitsunami, ilikubali ili iweze kudhibiti mageuzi.

Je sasa mnayadhibiti au mnayafungia? Vyama vyetu viache siasa za uhasimu na kukaa chini kuangalia maslahi ya hao mnaotaka kuwaongoza.
 
...tuta spin tunavyotaka na kuongea kila kitu lakini tatizo la Zanzibar ni CCM ambao hawakubali kuachia,fanya election ambayo ni fair & free utajua mchawi wa siku zote ni nani,lakini CCM wanavyocheza na vichwa vya watu mungu anajua,lakini yote haya yana mwisho,ningekuwa JK ningesema enough na sasa acha Demokrasi ifanye kazi...hizi propaganda za kusema sultani atarudi ndio mwanzo wa yote haya na kurudisha nyuma maendeleo,angalia sasa zaidi ya miaka 15 ni majungu tuu na hakuna maendeleo,yana mwisho lakini
 
2008-09-30
Na Simon Mhina


Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Pius Msekwa, ameshangaa madai ya Jaji Joseph Warioba kwamba vikao vya chama hicho vimejaa visasi na kukomoana na kumtaka aache kile alichokiita `usongombwingo`.

Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu kutoka Tarime jana, Msekwa alihoji kwa kusema: ``Wewe Mwandishi unajua maana ya Usongombwingo? Usongombwingo ni umbea uliojaa uzushi na uongo.``

Akifafanua, Msekwa alisema kwa vile vikao anavyolalamikia Warioba vya Umoja wa Wanawake (UWT) vilikuwa vya siri, na wala yeye hakuwa mjumbe, kwa vyovyote alipelekewa taarifa za vikao hivyo na wambea na hivyo kujikuta anajiingiza kwenye usongombwingo bila kujijua.

Msekwa alisema ameshangazwa na kauli ya Warioba kwamba Baraza Kuu la UWT lilitumika kumkomoa mmoja wa wanachama wake aliyeomba kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa, Halima Mamuya na kumpa alama `E`.

Alisema ameshangaa kuwa Warioba amepata wapi habari za Mamuya kupata alama `E` wakati vikao vya UWT vinahudhuriwa na wanawake watupu.

``Mimi nimeshangaa kama kweli Warioba katoa shutuma hizo kapata wapi taarifa za vikao vya UWT?

Vikao vile ni vya wanawake watupu, yeye alikuwepo? Hata wewe wa Nipashe unaponiuliza pia nakushangaa, mimi ni mwanaume hivyo huko UWT sikuwepo, labda muulize huyo huyo aliyetoa shutuma, labda yeye alikuwepo siwezi kujua mimi niko Tarime,`` alisema Msekwa huku akiangua kicheko.

Kikao cha Baraza Kuu la UWT kilichopitisha majina hayo na kumpa Mamuya alama E kilikuwa chini ya Mwenyekiti wake, Anna Abdallah ambaye ni mke wa Msekwa.

Msekwa pia alisema kisheria mtu anayetoa tuhuma ndiye anayetakiwa athibitishe.

Alisema kwa vile yeye bado hajapata taarifa rasmi juu ya madai hayo, hawezi kuzungumzia `usongombwingo` kwa vile akifanya hivyo atakuwa anajiingiza katika mambo asiyoyajua.

Alisema kimsingi Chama hakiwezi kuingilia maamuzi ya vikao vya jumuiya zake, kabla ya kuletewa taarifa zilizorasmi.

``Tunaziamini jumuiya zetu na taratibu zao, hatuwezi kuwaingilia kwa kutoa maamuzi kabla hawajatuletea taarifa rasmi juu ya vikao vyao na yale waliyojadili na kuamua,`` alisema Msekwa.

Kuhusu Nape Nnauye ambaye naye amepewa alama `E` katika mchujo huo kwenye Jumuiya ya Vijana (UVCCM), Msekwa alisema hata kwenye jumuiya hiyo, taarifa za vikao vya mchujo hazikufika rasmi.

Havi karibuni Warioba alikaririwa na gazeti hili akishutumu tabia iliyoibuka hivi karibuni ya wajumbe wa vikao mbalimbali vya CCM kuvitumia kulipa kisasi na kuwakomoa wanachama wanaoomba kuwania nafasi mbalimbali na kuwapa alama wasizostahili.

Warioba alisema Mamuya na Nape hawakustahili kupata alama `E` inayomaanisha muombaji hajui hata itikadi ya CCM.


SOURCE: Nipashe
 
punguani wewe msekwa huyo anajua mpaka lini watakuondoa hapo ccm
kunguru mkubwa uwe na adabu na waliokutangulia hiko cheo ni c=ha heshima
sio sehemu ya kuzia jina
 
Hapa Warioba amechemsha, huyu Mama Mamuya alitakiwa kutinga kwenye sheria kutokana na ufisadi ailoufanya huko kina mama akiwa katibu, ni fact wala sio kusingiziwa kua alikwapua kama shillingi millioni kati ya 5-10 za umoja huo kwa ujanja na alishikwa red handed wala hakuwa na ubishi akakimbia na kujiuzulu,

Lakini maneno ya majibu ya Msekwa ni unwarranted na un necessary na ni pia out of line ya decency, kwa sababu politically Warioba ni very senior kwake!
 
Kauliza za Makamba , Tambwe na Msekwa kwa vijembe na hata Mkapa ni zile zile sasa leo sitashangaa akaongea kama mtu ambaye hana akili nzuri kwa kuwa ni hulka yake .He is also a very power monger huyu Mzee .
 
alikwapua kama shillingi millioni kati ya 5-10 za umoja huo kwa ujanja na alishikwa red handed wala hakuwa na ubishi akakimbia na kujiuzulu,

lshillingi millioni kati ya 5-10 loh@@!!!!!!!!!

na
 
epa jamani hamjuwaona hao??????kila mtu anakula kazini kwake!!!!!!
 
Huyu mzee siku hizi mimi nampuuza,zamani nilikua namuona mwenye busara sana kumbe ni kilaza aliyetukuka
 
Hivi Msekwa anataka kutuambia kwamba mkutano wa Wanawake UWT huwa hauna nakala ambazo zinawakilishwa ktk kamati ya chama.. Hivi kweli mambo ya Wanawake humalizwa na wanawake wenyewe kiasi kwamba katibu wa chama hajui kinachoendelea hata baada ya vikao vyap...hakuna taarifa yoyote inayomfikia yeye wala mwanaume yeyote kama ni maamuzi ya kikao hicho!..

Kazi kweli kweli..
 
Hivi Msekwa anataka kutuambia kwamba mkutano wa Wanawake UWT huwa hauna nakala ambazo zinawakilishwa ktk kamati ya chama.. Hivi kweli mambo ya Wanawake humalizwa na wanawake wenyewe kiasi kwamba katibu wa chama hajui kinachoendelea hata baada ya vikao vyap...hakuna taarifa yoyote inayomfikia yeye wala mwanaume yeyote kama ni maamuzi ya kikao hicho!..

Kazi kweli kweli..

Well said Mzee Mkandara!,
Warioba hatojibu shutuma za Mzee Msekwa,kwa kufanya hivyo atauua huu mjadala(kifo cha mende),kama ukisoma kwa makini maneno ya Mzee Msekwa utagundua kuwa kuna mengi zaidi ya hayo......hakukuwa na sababu yoyote ya kujibu shutuma za Mzee Warioba kwa maneno ya mtaani,Msekwa anatafuta vita vya maneno ambavyo mwisho wake si mzuri......Sijui nani kawaloga hawa wenzetu (CCM),Naona kila siku kuna beef jipya huko.....Ni vyema wamuone Mama Mbunge/Mchungaji ili aombee amani itawale ndani ya Chama Tawala.
 
1.Nini hasa maana ya neno usongombwingo........nafikiri ni usongombingo ni hali fulani isiyo shwari...........both ukweli/uongo waweza sababisha songombingo

Ni nani aliyesema/tamka hilo neno

Huyu Msekwa ndiye aliyesema eti......."watu wana wivu wa Kike"......leo kaja na mpya unsongombwingo..........hivi kulikuwa na ulazima wa wee Mzee kujibizana na Warioba kupitia mwandishi tena ktk simu?

.........sasa wewe Mzee Msekwa hayo maneno yako ndio huleta songombingo and nothing less
 
Ni yaleyale ya siasa kama ajira ya familia. Msekwa alishayasogoa haya yote kwenye bedroom yao na mkewe, yote kabisa kabla hayajatokea, alitegemea maswali haya na bila shaka aliandaa majibu. Kiwango cha majibu ya mtu hata kama amejiandaa kinategemea uwezo wake kiakili. Hata shuleni nilipofundisha kuna wakati nilikuwa nawatajia kabisa wanafunzi maeneo ambako mtihani ungetoka, na kweli natoa hukohuko, lakini utashangaa majibu ambayo wengine wanatoa!

Kama familia, Msekwa na mkewe wanajua ni nani hawamtaki huko UWT na kwingineko wanakohusika, kwa hiyo tutegemee majibu yoyote yale!
 
Msekwa akiri ufisadi umeiumbua CCM kwa sababu ya kulindana

msekwaufisadi.jpg


Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa,amekiri kuwa kashfa za ufisadi toka kwa baadhi ya viongozi wa CCM zinakiumbua chama hicho tawala.

*Kuanzisha Chuo Kikuu cha Maadili Iringa

Na Fredy Azzah
Mwananchi


MAKAMU Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa, amesema kashfa za ufisadi zinazowakabili baadhi ya viongozi wake, zimekiumbua chama hicho pamoja na serikali yake.

Akiwahutubia wanafunzi wa matawi ya CCM ya vyuo vikuu vilivyopo jijini Dar es Salaam, wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 10 ya kifo cha Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere jana, alisema ufisadi ambao umewakumba wengi umesababishwa na tabia ya viongozi kulindana na kutosimamia kikamilifu maadili ya uongozi yaliyoainishwa ndani ya katiba ya CCM.

Alisisitiza kuwa tabia hiyo ni kinyume na misingi ambayo Baba wa Taifa, aliwaachia Watanzania.

Mara kwa mara Baba wa Taifa alikuwa anatumia methali inayosema; Mficha maradhi, kilio humfichuaâ. Katika utaratibu huu wa kumkumbuka na kumuenzi, hatuna budi kukiri upungufu huo tulio nao wa kutoweka usimamizi makini wa maadili ya viongozi wetu na ndiyo kiini cha kuwepo ufisadi na uzembe, alisema Msekwa na kuongeza:-

Kwa kuwa tulificha maradhi hayo, sasa kilio dhidi ya vitendo viovu vya baadhi ya viongozi wetu, ambavyo vimepewa jina la ufisadi, vimetuumbua.

Msekwa alisema kwa sasa serikali inapaswa kuchukua hatua za kujisahihisha; kwa kuhakikisha kuwa viongozi wote watakaobainika kujiingiza katika ufisadi wanafikishwa katika vyombo vya sheria.

Lengo la kuwachukulia hatua mara moja viongozi wanaokiuka maadili mema, linatukumbusha mafundisho mengine ya Baba wa Taifa, aliyokuwa akiyatoa kwa kutumia methali isemayo: Mtoto akichezea wembe, utamkata pale pale, hausubiri mpaka baadaye," alisema Msekwa ambaye aliwahi kuwa Spika wa Bunge la Tanzania na Katibu Mtendaji Mkuu wa CCM.
 
Kama anamaanisha anachosema basi itakuwa ni step kubwa kwa CCM. Na kwa kweli kujisafisha kwao kama watataka, kutaiweka nchi katika position tofauti na iliyopo sasa.
 
Msekwa umenena, watajeni kwa majina hao wezi wetu na muwafute uwanachama, kisha waende segerea na kufilisiwa, wachache ni RA, EL, EC et al., bila kumsahau TANESCo MD.
 
Date::10/14/2009Msekwa akiri Akiwahutubia wanafunzi wa matawi ya CCM ya vyuo vikuu vilivyopo jijini Dar es Salaam, wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 10 ya kifo cha Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere jana, alisema ufisadi ambao umewakumba wengi umesababishwa na tabia ya viongozi kulindana na kutosimamia kikamilifu maadili ya uongozi yaliyoainishwa ndani ya katiba ya CCM.

Alisisitiza kuwa tabia hiyo ni kinyume na misingi ambayo Baba wa Taifa, aliwaachia Watanzania.

Mara kwa mara Baba wa Taifa alikuwa anatumia methali inayosema; Mficha maradhi, kilio humfichuaâ. Katika utaratibu huu wa kumkumbuka na kumuenzi, hatuna budi kukiri upungufu huo tulio nao wa kutoweka usimamizi makini wa maadili ya viongozi wetu na ndiyo kiini cha kuwepo ufisadi na uzembe, alisema Msekwa na kuongeza:-

Kwa kuwa tulificha maradhi hayo, sasa kilio dhidi ya vitendo viovu vya baadhi ya viongozi wetu, ambavyo vimepewa jina la ufisadi, vimetuumbua.

Msekwa alisema kwa sasa serikali inapaswa kuchukua hatua za kujisahihisha; kwa kuhakikisha kuwa viongozi wote watakaobainika kujiingiza katika ufisadi wanafikishwa katika vyombo vya sheria.


Msekwa wewe ni mmoja wa Viongozi wa juu kabisa katika CCM, je, huko nyuma ulichukua hatua gani kupambana na hii tabia ya kulindana!? Na sasa kipi unachokifanya ili kuondoa uozo huu ndani ya CCM?

Badala ya kusubiri wale watakabaonika kamba wamejiingiza kwenye ufisadi ili washughulikiwe, kwanini msianze na wale ambao wameshabainika kwamba walijihusisha na ufisadi kama Chenge Vijisenti, Idrissa Rashid, RA na wengineo. Je, haya ni maeno ya kweli au ni katika kutaka kujisafisha kuelekea October 2010?
 
Huyo Msekwa mwenyewe amefanya kampeni za ubunge za kifisadi, sasa hapa analeta lip service tu.

Bread and circuses, who am I kidding? Not even bread, just stale circuses with some old fart clowns.
 
Back
Top Bottom