sajo
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 3,336
- 6,028
Msanii mkongwe wa Hip Hop nchini, Salutaba Mwakimwagile maarufu kama Salu T amefariki dunia jijini Mbeya leo tarehe 15 Aprili 2023. Msanii huyo amefariki akiwa anaendelea kupewa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.
Akitoa taarifa ya awali, Msanii mwingine wa HipHop, Taikun Ally maarufu kama Mchizi Mox ameeleza kuwa jumanne tarehe 12 Aprili 2023, Salu T akiwa mkoani Mbeya katika harakati zake za maisha, alipata ajali ya gari iliyomsababishia majeruhi na maumivu ya mgongo. Imeelezwa kuwa hali ya Salu T ilikuwa mbaya na hivyo kupewa rufaa ya kwenda hospitali ya Taifa Muhimbili lakini hali yake haikuruhusu kusafiri na hivyo aliendelea kubaki hospitali ya Rufaa Mbeya mpaka umauti ulipomkuta.
Salu T amewahi kutamba na ngoma kama Chunga Sana aliomshirikisha msanii AY (2006) na kutayarishwa na Producer Lindu.
na ngoma nyingine nyingi, ikiwa ni pamoja na album iitwayo HAZINA.
Mchizi Mox ameeleza kuwa msiba wa Salu T upo nyumbani kwao marehemu mitaa ya Round about ya Mbuyuni, Kinyerezi Dar es Salaam na mazishi yanatajiwa kufanyika Jumatatu tarehe 17 Aprili 2023 jijini Dar es Salaam.
Pole kwa familia ya Salu T na wanaHipHop wote.
Mungu ailaze pema roho ya Salu T.