sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,230
Kuna rundo la watu wenye wasiopenda wema wa kijana wameegamia kwenye fikra potofu kwamba ilibidi huu msaada utoke kimya kimya, Jibu ni "NO" "HAPANA!!!" Kuna misaada inabidi itoke kimya kimya mfano kumsaidia omba omba wa barabarani au kumsaidia ndugu yako kodi, Ila kwa hali ya huu msaada wa kufikia watu 500 kijana kafanya la maana kwasababu watu wenye hali za chini wengi wao hawana hizi smartphones ila sisi wenye nazo ndio tumewataarifu, Kitu kingine ni kwamba aina hii ya msaada ukifanywa kimya kimya inaweza kuonekana kama mbinu ya kusafisha pesa au kukwepa kodi, Ni vema kijana kafanya huu msaada uwe wazi.
Makadirio ya kiasi kitachotumika: hapa kijana kalenga kulipia kodi za nyumba kwa familia zenye hali duni, kwa makadirio hizi nyumba kodi huwa hazizidi elf 40 hadi elf 60 kwa mwezi, ila tukikadiria ni elf 50 basi kwa miezi mitatu ni 150,000, kwa nyumba 500 ni takribani milioni 75, Ni kiasi ambacho ni kingi huenda kijana angenununia gari au kuitumia kuandaa video kali za kazi zake ila kwa kuwa ni msanii mwenye mafanikio makubwa na ni kioo cha jamii kaamua kujibana kikomandoo arudishe fadhila kwa jamii inayomzunguka
============
Fuatilia Diamond alivyotimiza ahadi yake
Diamond Platnumz aanza kutoa msaada wa kodi ya miezi 3 kwa kaya 500 - JamiiForums