Tetesi: Msanii Diamond Platnumz (Dangote) aumbuka Kenya:

Unashangaa kijana wa tandale mwenye elimu ya kuunga unga kukosea kiingereza!!!!kuna jamaa ana PHD(ya kusomea si ya kupewa) kiingereza kinamsumbua! kwa kifupi kwenye suala la kuongea kiingereza tunatakiwa kujifunza toka kwa diamond: kukubali kujifunza bila kujali kiwango cha elimu wala kuona aibu unapokosea ndio msingi wa kujua hiyo lugha.

Haswaaaaaa nakuunga mkono. Hakuna mTZ anajua kingereza na ajitokeze sasa. Monds mi nam admire sana. Juhudi yake aliyofanya sote twapaswa kuiga. Nimemuona akihojiwa sana na vituo vya nje anaongea vizuri sana. tumpe moyo na kuiga toka kwake. Wakenya wanataka kumshusha tu......... Mond usikate tamaa, ongea kwa sana ukiwaona tena
 
Umeleta haya yote hapa jamvini ukiwa na lengo gani? Unaonekana una chiki binafsi na Nasib mambo mengine umechapia tu - ndiyo baadhi ya Watanzania walivyo wivu tu hamna kingine. Kama wewe ni Mtanzania mzalendo uwezi kumkandia Mtanzania mwenzako kwa kushadidia upuuzi wa vyombo vya habari vya Kenya ambavyo ujui lengo lao ni nini - hata akili ya kutambua kwamba Wakenya walifanya hivyo makusudi wakiwa na lengo la kumfanya Nasib ajisikie munyonge kwani waliona ugumu gani kama wange conduct mahojiano kwa lugha ya Kiswahili wangekosa nini,mbona Rais wao (Uhuru Kenyatta) mikutano mingi anapo kutana na wananchi uzungumza kiswahili fasaha. Walimtegea Nasib ili wapate sababu za kumubamiza ndio walivyo, kwani Nchini Kenya nani ajui kuzungumza/kuelewa kiswahili hata kama ni cha kubabaisha?

Labda kwa kukuelimisha kidogo ni kwamba Mataifa yanayo jitambua Duniani uenzi lugha zao za Kitaifa siyo lugha za kigeni, niliwahi kuwambia hapa kwamba Waingereza ushangaa sana Nchi za Kiafrika zinaso diriki kusema eti lugha yao ya Kitaifa ni Kingereza!! - binafsi niliwahi kushuhudia kwa macho yangu huko Uingereza Mkenya akidhalilishwa na Mwingereza tulipo karibishwa kwenye chakula cha jioni, mwenyeji wetu huyo alitaka kujua culture za nchi wanako toka waalikwa mojawapo likiwa swali ya lugha zao za kitaifa i.e wanaelewana vipi wakati kila nchi ina makabila tofauti na lugha tofauti, tukajieleza - ilipofika zamu ya Mkenya aliposema eti National language ya Kenya ni kingereza mwenyeji wetu alishangaa kidogo - mwanzo Mkenya huyo alifikiri akisema hivyo basi Mwingereza atamuona wa maana, kumbe nikujidhalilisha - siwezi kurudia mwenyeji wetu alivyo mjibu Mkenya - sasa na sisi Waswahili wa hapa Tanzania tunarudia ulimbukeni wa kufikiri ukizungumza lugha ya kigeni flawlessly basi wewe una akili sana au hiyo tu inaonyesha umendelea - what does masterly of English gotta do in Music Industry??
Umenena mkuu
 
Ndio maana mimi nikiwaona watu wanaongea viingleza najipitia kimyakimya tu, mambo ya usumbufu mi sipendagi.
 
Back
Top Bottom