Msajili wa vyama vya Siasa unasubiri nini kuifutia usajili CHADEMA wakati inaendelea kukiuka sheria na kuchochea chuki na ubaguzi?

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
16,068
10,572
Ndugu zangu Watanzania,

Nauliza kwa uchungu mkubwa sana kuwa ofisi ya msajili wa vyama vya siasa ipo wapi? Inafanya kazi gani? Imelala wapi huko usingizi wa pono mpaka inashindwa kuona hatari kubwa inayoletwa na CHADEMA hapa nchini? Msajili unaendeleaje kupokea mshahara ambao ni kodi zetu watanzania wakati unatuweka hatarini watanzania na amani ya Taifa letu?

Sheria ya vyama vya siasa inakataza na kupiga marufuku kabisa kwa chama chochote cha siasa kufanya siasa zenye kuchochea ubaguzi kwa misingi ya Udini, ukabila na hata ukanda.sheria inakataza pia kwa chama cha siasa kunadi sera zinazohamasisha au zenye lengo la kuvunja muungano wetu au zenye lengo za kufanya siasa za upande mmoja tu wa muungano.

Lakini leo hii tunashuhudia CHADEMA kupitia viongozi wake wakichochea chuki kali sana na kupandikiza uasi wa kuuvunja muungano wetu pamoja na kuchochea ukanda pasipo kuchukuliwa hatua za aina yoyote ile.ni hatari sana hii inayokuja kwa Taifa letu ikiwa hali hii ya kupandikiza mbegu za ubaguzi itaachwa iendelee kuhubiliwa na kuenezwa na CHADEMA.hii siyo siasa tuliyoitaka watanzania.hatukutaka siasa za kuja kutugawa watanzania na kulipasua Taifa letu.

Tulihitaji siasa za hoja,siasa za sera mbadala, siasa za fikira na mawazo mbadala juu ya ujenzi wa Taifa letu,siasa za hoja ya namna bora ya kulipeleka mbele Taifa letu .Siasa za mawazo mapya ya namna bora ya kutumia rasilimali zetu kwa usahihi katika kuinua uchumi wa Taifa letu na kuboresha maisha ya watanzania wote pamoja na usambazaji wa huduma za kijamii pamoja na kupunguza utegemezi.

Lakini inaogopesha na kutisha sana tunapoona CHADEMA imebadili majukwaa ya kisiasa kuwa uwanja wa kuwasha moto wa kuchochea machafuko kwa Taifa letu.chadema wameishiwa hoja za kuwashawishi watanzania na sasa wameamua waanze kupandikiza mbegu za ubaguzi na chuki kwenye mioyo ya watanzania. Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa dhambi ya ubaguzi ni mbaya sana ,ni sawa na kula nyama ya mtu ambapo huwezi ukaacha ukishakula nyama hiyo.

leo CHADEMA wameanza kupandikiza mbegu ya ubaguzi ,jinsia , ukanda na mengine mengi.hawataishia hapo bali wataenda mbele zaidi kuanza ubaguzi wa mkoa na mkoa kwa kusema mkoa huu unachangia mapato makubwa sana na hivyo ujitenge na kupewa hadhi ya aina yake.

Msajili wa vyama vya siasa amka ofisini haraka sana uchukue hatua kali sana kabla nchi haijaingia katika matatizo ambayo yatalisambaratisha na kuligawa Taifa vipande vipande. Tumia sheria kuwaadhibu CHADEMA kwa kuwa tayari wameshavunja sheria zote za usajili wao .na sasa wanastahili kufutiwa usajili. Mambo yanaanzaga hivi hivi mpaka mwisho inakuwa donda ndugu litakalolitesa Taifa lote..

Kazi iendelee,Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa,.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Nape amekwishamjibu kwa hoja,nadhani kuna tatizo la kuhuisha katiba yetu mengine yatakaa sawa
CHADEMA ni lazima wakemewe kwa nguvu zote kwa hili wanalotaka kulileta hapa nchini baada ya kuwa wameishiwa hoja za kuwashawishi watanzania kuwaunga mkono.
 
Acheni kuleta siasa za kibaguzi katika Taifa letu.kama mmeishiwa hoja za kuwashawishi watanzania kuwaungeni mkono ni bora muachane na siasa kuliko kuchochea ubaguzi utakaosababisha na kuchochea machafuko hapa nchini .
Punguza mihemko, Rais siyo Malaika, ana mapungufu yake pia, Rais pia kaajiriwa na wananchi hivyo pale ambapo hapako Sawa lazima aambiwe ukweli. Tulia
 
Huyu lini atachukuliwa hatua na chama chake kufungiwa?

20240429_211230.jpg
 
Chadema ni chama kikubwa sana na kimebeba matumaini mengi sana ya watanzania hasa wa hali ya chini ambao hawana ajira au wenye kipato kidogo hivyo kama serikalii ikijaribu kukifuta ni kutafuta mfarakano katika jamii cos italeta shida au mafuriko ya fujo kama Sudan au somalia watu watauwana sana.....

Serikali ipo na watu makini na washajua ilo kwamba ni hatari kuendelea kuwafanya watanzania wajinga cos ile kasumba ya watu waadilifu inaenda kupotea taratibu saivi kuna vijana hawana cha kupoteza na wengi wapo kwenye tumaini la chadema labda watapata nafuu endapo chama hicho kikishika inchi hivyoo Mkuu Lucas hilil jambo sio jepes kama unavyozani.......
 
Ndugu zangu Watanzania,

Nauliza kwa uchungu mkubwa sana kuwa ofisi ya msajili wa vyama vya siasa ipo wapi? Inafanya kazi gani? Imelala wapi huko usingizi wa pono mpaka inashindwa kuona hatari kubwa inayoletwa na CHADEMA hapa nchini?...
Kuwa mpole mkuu usiogope hakuna lolote roho ikitaka kuacha mwili lazima mtu atape tape Samia kafanya kosa kumuondoa makonda pale kaweka watu wachovu sababu ya kuwasikiliza nape na ndugu yake wa yamini!
 
Chadema ni chama kikubwa sana na kimebeba matumaini mengi sana ya watanzania hasa wa hali ya chini ambao hawana ajira au wenye kipato kidogo hivyo kama serikalii ikijaribu...
Hakuna mtanzania mwenye mapenzi mema na Taifa letu anayeunga mkono na kufurahia mbegu ya ubaguzi inayopandwa na kuhamasishwa na CHADEMA.kila mtu mitaani analaani sana kauli zinazotolewa na viongozi wa CHADEMA.
 
Hakuna mtanzania mwenye mapenzi mema na Taifa letu anayeunga mkono na kufurahia mbegu ya ubaguzi inayopandwa na kuhamasishwa na CHADEMA.kila mtu mitaani analaani sana kauli zinazotolewa na viongozi wa CHADEMA.
Ni kweli mkuu maneno ya kibaguz sio siasa safi ila hata wew upaswi kurudisha maneno ya kibaguzi kwa kuombea Chadema mabaya cos Chadema sio TL au Mbowe chadema ni watanzania wote kwa upande wa upinzani hivyo ulitakiwa kumkemea TL .....
 
Ni kweli mkuu maneno ya kibaguz sio siasa safi ila hata wew upaswi kurudisha maneno ya kibaguzi kwa kuombea Chadema mabaya cos Chadema sio TL au Mbowe chadema ni watanzania wote kwa upande wa upinzani hivyo ulitakiwa kumkemea TL .....
Ni lazima tupinge kwa nguvu zote na kukemea chuki na ubaguzi unaotaka kupandikizwa na CHADEMA kwenye Taifa letu.
 
Back
Top Bottom