Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,669
- 119,294
Mkuu Baraghash, unamaanisha kazi nzuri na yakutukuka iliyofanywa na Okelo na ma comredi kwenye yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kuvirejeshea hishma visiwa vyetu vya Unguja na Pemba yaliyomtimua mvamizi ilikuwa ni kazi ya kishetani?!. Jee kauli ya "Naapa naahidi Mapinduzi nitakulinda mpaka kufa " na "Mapinduzi Daima" hazina maana kwenu?!. Ni vitu vidogo tuu kama hivi vinafanya "mnapata" lakini "hampewi" na kama hamta badilika, kamwe hamtapewa hivyo kuishia kulalamika kutwa kucha!. Kesho tunasherekea maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wetu Adhimu. Kwa vile Tanzania ni nchi moja ya JMT,na tutaulinda Muungano kwa gharama yoyote, yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya 1964 pia yatalindwa kwa gharama yoyote, hivyo dharau mengine yote lakini kamwe usiyadharau Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, na waasisi wa Mapinduzi, yale akiwemo John Okello.Kweli Nakumbuka umetoa hoja hiyo kitambo kwa vile, CUF kwako ni zaidi ya chama cha siasa. Una hamu na matamanio ya kukamilisha ndoto za kishetani alioteshwa Field Marshall John Okello na " mungu" dhidi ya watu wa Zanzibar wenye imani tofauti na yeye.
Paskali