Msajili Mkuu wa Mahakama awataka mahakimu wazingatie haki ya dhamana

MP CHACHANDU

JF-Expert Member
Dec 4, 2016
875
616
Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Katrina Revocati amewataka mahakimu nchini kuzingatia sheria katika utendaji wao wa kazi hasa katika utoaji wa dhamana.

Kauli ya Msajili imekuja wakati kukiwa na malalamiko dhidi ya baadhi ya mahakimu kuwanyima dhamana washtakiwa ilhali mashtaka yao yanaruhusu.

Aidha, kauli ya msajili huyo mkuu imekuja wakati mawakili wa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wakipambana ili mteja wao apate dhamana baada ya kukwaa kisiki katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Mashtaka ambayo kwa mujibu wa sheria dhamana zake zimezuiwa ni ya mauaji ya kukusudia, uhaini, utakatishaji wa fedha, wizi wa kutumia silaha, usafirishaji binadamu na dawa za kulevya.

Hata hivyo, Mahakama inaweza kuzuia dhamana endapo kutakuwa na pingamizi la kisheria, na mara nyingi mapingamizi hayo yamekuwa yakiambatana na hati kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Msajili huyo alitoa maagizo hayo jana mjini Moshi alipokuwa akizungumza na mahakimu wa ngazi zote katika mahakama za mjini Moshi baada ya kumaliza ziara ya kikazi katika mkoa wa Kilimanjaro.

Taarifa iliyotolewa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Bernard Mpepo ilisema msajili huyo waliwataka mahakimu watunze maadili yao ili kujenga imani kwa jamii.

Msajili mkuu pia alitembelea Gereza Kuu la Karanga mjini Moshi na kufanya ukaguzi wa kawaida na kisha kuzungumza na wafungwa, mahabusi na wafanyakazi wa gereza.

Akiwa katika gereza hilo, msajili mkuu alisema mkakati wa Mahakama ni kuona wateja wanapata huduma bora na ya haraka na tayari mahakimu wamepewa malengo ya kumaliza kesi haraka.

Ili kuboresha huduma, alisema mwaka 2017 wamekubaliana katika mahakama ya mwanzo, shauri lolote lisikae zaidi ya miezi sita wakati mahakama ya wilaya na mkoa shauri lisikae zaidi ya miezi 12.

Pia mahakama imeingia mkataba na Shirika la Posta kusambaza nakala za hukumu kwa wateja na nakala ya hukumu itakuwa inamfikia mdau ndani ya siku 21.

Chini ya mkakati huo, nakala ya mwenendo wa shauri utamfikia mteja wa mahakama ndani ya siku 21.
 
Huo ndio ukweli bali upande ule wa pili hukumu ikiwa upande wao MAHAKAMA IMETENDA HAKI lkn ikiwa dhidi yao MAHAKAMA IMEFUATA MAAGIZO KUTOKA JUU.

Hii ni post ya kujishuku. Alichokizungumza huyo bwana kiko wazi na kinachoendekea kinaonekana. Wanaoitumia mahakama kwa madaraka yao wako wazi. Huoni kwanini ametamka neno anayepaswa kupewa dhamana apewe?
 
wafate sheria,ni sawa..watu wapate haki zao bla kuangalia maslah y watu binafsi.
 
Hii ni post ya kujishuku. Alichokizungumza huyo bwana kiko wazi na kinachoendekea kinaonekana. Wanaoitumia mahakama kwa madaraka yao wako wazi. Huoni kwanini ametamka neno anayepaswa kupewa dhamana apewe?
Nani kanyimwa dhamana kinyume cha sheria?
 
Nadharia ya mahakama kuwa huru ilikuwepo, ipo na itaendelea kuwepo. Tatizo katika utekelezaji linatokana na watendaji.
Sheria zipo, shida ni watu. Ustaarabu hupatikana kwa kuwashughulikia moja kwa moja watu wanaotumia nafasi zao vibaya, au kutimiza kiu zao za uovu kwa kujificha kwenye kivuli cha mfumo.
Ukishughulika na mtendaji asiyetoa haki moja kwa moja itakuwa fundisho kwake na kwa wengine, na mwisho wa siku kunakuwepo na fursa sawa kwa wote.
 
wanaojimilikisha hii nchi, na vyombo vyake km mahakama polisi n.k,cku zao zinahesabika, watalia na kusaga meno
 
Uteuzi wa msajili mkuu wa mahakama utatenguliwa wakati wowote kutokana kauli aliyoitoa Jana kuwataka mahakimu kutosikiliza matamko kutoka kwa wanasiasa mbali wafate sheria tetesi ambazo zipo ni kwamba uteuzi huu utatenguliwa mda wowote na SAA yoyote kwanzia sasa .

Msajili huyo alisema mahakama siyo chombo cha siasa hivyo aliumizwa na jambo la mbuge lema kunyima dhamana wakati kesi yake ipo kwenye kesi ambazo zinazaminika kwa wepesi tu .
 
akitoka afanye siasa za kistaarabu!
 
mahakama haitakuwa huru 100% kama mfumo wa uteuzi katika mhimili wa mahakama unafanywa na wanasiasa kamwe. pia bajeti ya mahakama ilipaswa kutoingiliwa na muhimili wa serikali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…