Msaada wa ushauri katika kipindi hiki kigumu nilichonacho na Mungu atakubariki

mkuu mali nilizokuwa na simamia sio mali nyingi ni mifugo tu mishache na mashamba kidogo ambayo ndo yalikuwa yanatusaidia tunapata chakula wazazi wangu hawakuwa na uwezo mkubwa walikuwa ni masikini tu...but ahsante sana mkuu kwa ushauri wako
Kwani huko kwenye ajira unaenda kujitolea au utakuwa unalipwa mshahara? Kama utalipwa mshahara si utakuwa unakusaidia ku cover hizo gharama za kula na kusongesha maisha? Hata huko unapoenda kuna mashamba. Mifugo hata ukitaka kuihamisha utaweza tu! Kila siku kuna maroli yanaleta ng'ombe kutoka usukumani mpaka Dar, kwani nini kinashindikana? Unaweza ukahama na mali zako.
 
walulimu wa siku hizi sijui wakoje, utaweza kuwafundisha watoto wetu stadi za maisha kama unalialia kwa hili.

anyway wengi wameshakupa ushauri
mkuu ahsante sana but ebu jaribu kuvaa viatu vyangu utaelewa magumu nayopitia ndugu
 
Kwani huko kwenye ajira unaenda kujitolea au utakuwa unalipwa mshahara? Kama utalipwa mshahara si utakuwa unakusaidia ku cover hizo gharama za kula na kusongesha maisha? Hata huko unapoenda kuna mashamba. Mifugo hata ukitaka kuihamisha utaweza tu! Kila siku kuna maroli yanaleta ng'ombe kutoka usukumani mpaka Dar, kwani nini kinashindikana? Unaweza ukahama na mali zako.
mkuu ahsante sana tatizo sio nitashindwa kusongesha maisha tatizo ni malezi ya wadogo zangu yatakuwaje nikiwa mbali nao
 
mkuu sio kwamba nataka kufanya kazi karibu na nyumbani ni matatizo ya kifamilia ndo yamesababisha yote haya..and mkuu ebu jaribu kuvaa viatu vyangu leo hii nianze kuzunguka na watoto kwenye nyumba za kupanga and hizi mali walizotuachia wazazi hata kama ni kidogo nani atazisimamia nikiwa mbali huku..imagine mkuu
Kwa utandawazi huu, pangisha nyumba au tafuta ndugu akae hapo, watu wenyewe ni wawili tu kweli unashindwa kuhama nao? acha ushamba fanyakazi huku kaskazini upate na akili nyingi za maisha, usimchoshe Mungu kama ulikuwa unamuomba kazi na amekupa alafu unataka kuiacha, watu wangapi wanaishi kwenye nyumba za kupanga? walimu huwa mnamatatizo sana.
 
Nami nakushauri yafuatayo:
1.Tafuta mtu wa kubadilishana nae kituo cha kazi, nina hakika utapata mtu.
2. Kama unahakika hakuna ndugu yeyote wa kusimamia mali za wazazi, hamisha wadogo zako, uza mali, pesa utakayopata nenda katafute eneo huko uliko, anzisha makazi, ikiwemo miradi kama vile ufugaji au kilimo au lolote, lakini mali hizo utakazonunua, hazitakuwa zako peke yako. Ni zako na wadogo zako.
Natambua thamani ya rasilimali hasa ardhi, hivyo ukipata pesa, please usifanye starehe, nunua viwanja haraka sana.
 
Kwa utandawazi huu, pangisha nyumba au tafuta ndugu akae hapo, watu wenyewe ni wawili tu kweli unashindwa kuhama nao? acha ushamba fanyakazi huku kaskazini upate na akili nyingi za maisha, usimchoshe Mungu kama ulikuwa unamuomba kazi na amekupa alafu unataka kuiacha, watu wangapi wanaishi kwenye nyumba za kupanga? walimu huwa mnamatatizo sana.
mkuu ahsante sana kwa ushauri wako wa kujenga na ubarikiwe na mungu
 
Wakuu habari zenu,

Mimi ni kijana mtanzania mwenzenu ambae nipo kwenye dimbwi kubwa la mawazo kutokana na mambo yaliyonitokea. Kiufupi wakuu nilishapoteza wazazi wangu wote hivyo wakaniacha nikiwa na wadogo zangu watatu wawili wapo shule ya msingi na mmoja yupo kidato cha kwanza. Wakuu tukiwa tunaishi kwenye nyumba waliyotuachia wazazi hawa wadogo zangu nimejitahidi kuwasomesha kwa shida sana kwani hatukuwa na ndugu wa kutusaidia.

Nikiwa muhitimu wa chuo ninayesubiri ajira ilinilazimu nifanye kazi kwenye library ya kukodisha CD na kuingiza nyimbo na nilipata pesa ndogondogo kwa ajili ya kupata mkate wa maisha wa kila siku hivyo kunisaidia mimi na wadogo zangu. Wakuu kilichosababisha niwe katika dimbwi kubwa la mawazo ni hivi juzijuzi nimefanikiwa kuajiriwa na serikali kama mwalimu but eneo nililopelekwa ni mbali sana na nyumbani walipo wadogo zangu mimi ni mwenyeji wa kusini mwa tanzania but nimepelekwa kaskazini kabisa ambapo ni mbali sana na hii familia ninayoilea.

Wakuu katika kipindi kigumu nilichowahi kupitia ni hiki kwani hawa wadogo zangu ni wadogo mno na wanahitaji malezi yangu but ndo hivyo imenilazimu niwaache wenyewe na mimi kuja kureport kazini. Wakuu nimefikiria sana na nipo kwenye njia panda kwani inatakiwa niwepo karibu nahiii familia na kusimamia mali kidogo tulizoachiwa na wazazi ili wadogo zangu waweze kupata elimu.

Wakuu nimejaribu kuulizia taratibu za uhamisho kwa hii halmashauri niliyopo nimepewa maelezo kuwa ni ngumu sana kupata uhamisho kutoka huku sababu ya nature ya viongozi wakuu wahusika wa hii halmashauri niliyopo. Wakuu kutokana na hayo majibu niliyoyapata nimefikiria na kuona kama hamna uwo uwezekano wa kurudi karibu nahii familia niliyoachiwa ni bora niache tu hata hii kazi kwani wadogo zangu nimewaacha katika hali mbaya pasipo uangalizi wa karibu wa ndugu wala mlezi but nikifikiria nitaishi vipi kwa maisha ya kubangaiza niliyozoea najikuta katika wakati mgumu sana.

Wakuu nipo katika njia panda ya kukata tamaa na naombeni ushauri wenu nifanyaje, pia kama kuna mtu anaweza nisaidia mimi kuhama kutoka eneo hili nililopangiwa nirudi karibu na familia hii nayoilea or anaweza niunganisha na mtu anayeweza nisaidia nitashukuru sana. Sitakuwa na cha kumlipa but mimi na wadogo zangu tutamuombea mungu ambariki mana atakuwa kaiokoa sana hii familia na mungu atamlipa tu siku moja.

Kama kuna mtu anyeweza nisaidia nipo tayari kufanya kazi eneo lolote lile hata kama itakuwa kijijini vipi na mazingira ya kazi yawe magumu vipi ili mradi tu mi niwe karibu na hawa wadogo zangu ambao wananitegemea mimi kwa kila kitu.

Nitashukuru sana kama mtanipa ushauri mzuri wa kunisaidia na najua jamiiforum kuna watu wengi wa kila namna kama kuna mtu ataguswa nakuhitaji kunisaidia namna ya kurudi karibu nahii familia or kunisaidia kuniunganisha na mtu yoyote enayeweza kunisaidia unaweza kuja PM na mungu atakulipa. Nipo katika hali ya stress sana kwani nachofikiria sasa ni bora tu niachane na hii kazi ili nikawalee wadogo zangu mana mimi ndo baba,mama na ndugu yao pekee niliyebakia hapa duniani.

Nimejitahidi kuandika kwa ufupi kwani ni mengi sana yakusikitisha yaliyonyuma ya maisha yangu mi na wadogo zangu tangu wazazi wamefariki.

Ahsanteni sana.
Pole rafiki kwa changamoto ulizopitia na unazopitia.mi ushauri wangu kwako ni kwamba usikatishwe tamaa na maneno ya hao waliokwambia ni vigumu kupata uhamisho,pengine wao ishu zao hazikuwa nzito kama yakwako.Anyway,nenda hadi kwenye uongozi husika jieleze hali unayopitia usiwafiche mi naamini kama wana ubinadamu watakuelewa.pili usiache kazi maana huo ndo mpenyo wenyewe wa kufanikiwa.pia unaweza kutafuta mtu wa kukaa na wadogo zako kwa malipo ya kila mwezi japo kumpata inaweza kuwa ni changamoto pia.
 
Miaka 23 mkuu
Ndio maana... Ok, wewe tangulia, ukifika kule utapewa pesa za kujikimu. Then utawatumia wadogo zako kwenye simu kwa Mpesa n.k... Then kabla hujaondoka hakikisha umenunua simuya bei nafauu ili uweze kuwasiliana nao ukiwa mbali... Tafuta mtu mkubwa jirani ambaye utamkabidhi awe anawaangalia kwa kipindi ambacho uko mbali. Hakikisha ndani umewaachia chakula cha kutosha na hela kidogo. Nina uhakika ukifika huko utakuwa umepewa pesa za kujikimu na hivyo utaweza kupanga nyumba. Baada ya kama miezi miwili mitatu, watafutie uhamisho kama wanasoma shule waje huko ulipo. Mifugo kama huna mtu wa kumuachia iuze ukifika huko utanunua mingine. Mashamba yaache kama yalivyo... Usiyauze.
 
Tupo pamoja mkuu,changamoto za dunia zipo nyingi sana, lkn tutazikimbia??? Hapana lazima tupambane nazo tena kwa njia ya kupambana na kumtanguliza MUNGU mbele tutafanikiwa kuzivuka salama...
ndiyo mkuu haijalishi mtu unapitia katika kipindi gani kigumu but mwisho wa siku tutafanikiwa tu
 
Ndio maana... Ok, wewe tangulia, ukifika kule utapewa pesa za kujikimu. Then utawatumia wadogo zako kwenye simu kwa Mpesa n.k... Then kabla hujaondoka hakikisha umenunua simuya bei nafauu ili uweze kuwasiliana nao ukiwa mbali... Tafuta mtu mkubwa jirani ambaye utamkabidhi awe anawaangalia kwa kipindi ambacho uko mbali. Hakikisha ndani umewaachia chakula cha kutosha na hela kidogo. Nina uhakika ukifika huko utakuwa umepewa pesa za kujikimu na hivyo utaweza kupanga nyumba. Baada ya kama miezi miwili mitatu, watafutie uhamisho kama wanasoma shule waje huko ulipo. Mifugo kama huna mtu wa kumuachia iuze ukifika huko utanunua mingine. Mashamba yaache kama yalivyo... Usiyauze.
ok ahsante sana mkuu ingawa haya mambo yanakatisha tamaa ndo hivyo inabidi nipambane nayo tuu..nilishafika kureport ndugu tangu tarehe 25 but hati leo hiyo pesa ya kujikimu hakuna hata dalili
 
Pole rafiki kwa changamoto ulizopitia na unazopitia.mi ushauri wangu kwako ni kwamba usikatishwe tamaa na maneno ya hao waliokwambia ni vigumu kupata uhamisho,pengine wao ishu zao hazikuwa nzito kama yakwako.Anyway,nenda hadi kwenye uongozi husika jieleze hali unayopitia usiwafiche mi naamini kama wana ubinadamu watakuelewa.pili usiache kazi maana huo ndo mpenyo wenyewe wa kufanikiwa.pia unaweza kutafuta mtu wa kukaa na wadogo zako kwa malipo ya kila mwezi japo kumpata inaweza kuwa ni changamoto pia.
ahsante sana mkuu inabidi nimtafute mtu mkubwa nimuelekeze huenda akawa na roho ya huruma ya kunisaidia..nitashukuru sana kama nitafanikiwa
 
Back
Top Bottom