Wakuu habari zenu,mimi ni kijana mtanzania mwenzenu ambae nipo kwenye dimbwi kubwa la mawazo kutokana na mambo yaliyonitokea.Kiufupi wakuu nilishapoteza wazazi wangu wote hivyo wakaniacha nikiwa na wadogo zangu watatu wawili wapo shule ya msingi na mmoja yupo kidato cha kwanza.Wakuu tukiwa tunaishi kwenye nyumba waliyotuachia wazazi hawa wadogo zangu nimejitahidi kuwasomesha kwa shida sana kwani hatukuwa na ndugu wa kutusaidia..
Nikiwa muhitimu wa chuo ninayesubiri ajira ilinilazimu nifanye kazi kwenye library ya kukodisha CD na kuingiza nyimbo na nilipata pesa ndogondogo kwa ajili ya kupata mkate wa maisha wa kila siku hivyo kunisaidia mimi na wadogo zangu.Wakuu kilichosababisha niwe katika dimbwi kubwa la mawazo ni hivi juzijuzi nimefanikiwa kuajiriwa na serikali kama mwalimu but eneo nililopelekwa ni mbali sana na nyumbani walipo wadogo zangu mimi ni mwenyeji wa kusini mwa tanzania but nimepelekwa kaskazini kabisa ambapo ni mbali sana na hii familia ninayoilea.
Wakuu katika kipindi kigumu nilichowahi kupitia ni hiki kwani hawa wadogo zangu ni wadogo mno na wanahitaji malezi yangu but ndo hivyo imenilazimu niwaache wenyewe na mimi kuja kureport kazini.Wakuu nimefikiria sana na nipo kwenye njia panda kwani inatakiwa niwepo karibu nahiii familia na kusimamia mali kidogo tulizoachiwa na wazazi ili wadogo zangu waweze kupata elimu.Wakuu nimejaribu kuulizia taratibu za uhamisho kwa hii halmashauri niliyopo nimepewa maelezo kuwa ni ngumu sana kupata uhamisho kutoka huku sababu ya nature ya viongozi wakuu wahusika wa hii halmashauri niliyopo.Wakuu kutokana na hayo majibu niliyoyapata nimefikiria na kuona kama hamna uwo uwezekano wa kurudi karibu nahii familia niliyoachiwa ni bora niache tu hata hii kazi kwani wadogo zangu nimewaacha katika hali mbaya pasipo uangalizi wa karibu wa ndugu wala mlezi but nikifikiria nitaishi vipi kwa maisha ya kubangaiza niliyozoea najikuta katika wakati mgumu sana.
Wakuu nipo katika njia panda ya kukata tamaa na naombeni ushauri wenu nifanyaje, pia kama kuna mtu anaweza nisaidia mimi kuhama kutoka eneo hili nililopangiwa nirudi karibu na familia hii nayoilea or anaweza niunganisha na mtu anayeweza nisaidia nitashukuru sana.Sitakuwa na cha kumlipa but mimi na wadogo zangu tutamuombea mungu ambariki mana atakuwa kaiokoa sana hii familia na mungu atamlipa tu siku moja.
Kama kuna mtu anyeweza nisaidia nipo tayari kufanya kazi eneo lolote lile hata kama itakuwa kijijini vipi na mazingira ya kazi yawe magumu vipi ili mradi tu mi niwe karibu na hawa wadogo zangu ambao wananitegemea mimi kwa kila kitu.
Nitashukuru sana kama mtanipa ushauri mzuri wa kunisaidia na najua jamiiforum kuna watu wengi wa kila namna kama kuna mtu ataguswa nakuhitaji kunisaidia namna ya kurudi karibu nahii familia or kunisaidia kuniunganisha na mtu yoyote enayeweza kunisaidia unaweza kuja PM na mungu atakulipa..Nipo katika hali ya stress sana kwani nachofikiria sasa ni bora tu niachane na hii kazi ili nikawalee wadogo zangu mana mimi ndo baba,mama na ndugu yao pekee niliyebakia hapa duniani.
Nimejitahidi kuandika kwa ufupi kwani ni mengi sana yakusikitisha yaliyonyuma ya maisha yangu mi na wadogo zangu tangu wazazi wamefariki..ahsanteni sana