Msaada: SSD 1080 PRO NGFF M.2 4TB Haifanyi Kazi Kwenye Laptop Yangu

Jumanne Mwita

JF-Expert Member
Nov 18, 2014
517
1,364
Habari wanajamvi,

Nimenunua kifaa cha kuhifadhi data aina ya 1080 PRO NGFF M.2 SSD 4TB
View attachment 3004187Kwa ajili ya kuongeza uwezo wa laptop yangu. Hata hivyo, baada ya kukifunga kwenye laptop yangu, haisomi ingawa inaonyesha kuwaka kama kawaida.

1000015438.jpg

SSD iliyokuwepo awali ni ya 128GB M.2 NGFF ambayo niliinunulia kwenye laptop, laptop ni aina ya ProBook.

Ninapowasha laptop, inaleta ujumbe huu:

Aptio Setup Utility Copyright (C) 2023 American Megatrends, Inc.

Nikiwa ndani ya hiyo Aptio Setup Utility sielewi chochote. Naomba msaada wenu wanajamii, nini naweza kufanya ili SSD yangu mpya iweze kusomwa na kufanya kazi ipasavyo? Je, kuna hatua za ziada ninazopaswa kuchukua?

Asanteni sana kwa msaada wenu.

---
 
Attachments

  • 1000015439.jpg
    1000015439.jpg
    2.4 MB · Views: 4
Habari wanajamvi,

Nimenunua kifaa cha kuhifadhi data aina ya 1080 PRO NGFF M.2 SSD 4TB
View attachment 3004187Kwa ajili ya kuongeza uwezo wa laptop yangu. Hata hivyo, baada ya kukifunga kwenye laptop yangu, haisomi ingawa inaonyesha kuwaka kama kawaida.

View attachment 3004198
SSD iliyokuwepo awali ni ya 128GB M.2 NGFF ambayo niliinunulia kwenye laptop, laptop ni aina ya ProBook.

Ninapowasha laptop, inaleta ujumbe huu:

Aptio Setup Utility Copyright (C) 2023 American Megatrends, Inc.

Nikiwa ndani ya hiyo Aptio Setup Utility sielewi chochote. Naomba msaada wenu wanajamii, nini naweza kufanya ili SSD yangu mpya iweze kusomwa na kufanya kazi ipasavyo? Je, kuna hatua za ziada ninazopaswa kuchukua?

Asanteni sana kwa msaada wenu.

---
SSD baadhi sio plug and play mkuu, sometime zinataka drivers, huna manual yake?

Ideal hapo unakuwa na flash mbili, moja Ya windows na nyengine yenye driver, then unapiga windows itashindwa kudetect ssd itakuomba driver, Unatoa driver kwenye flash nyengine then unaweka windows.

Hio Aptio ni bios pengine unatumia Machine kama ya Asus.
 
HD yako ya zamani ni NGFF mpya ni NVME zote zinatumia slot ya M2 lakini ni tofauti so kuna uwezekano laptop yako haiwezi kutumia NVME [Niliona vibaya kwenye simu kumbe zote ni NGFF!]

Itafute machine model yako hapa Memory & SSD Upgrades | Crucial.com au soma manual yake. Kisha tazama compatible SSD. Kama inakubali SSD ya aina hiyo endelea kusoma chini, kama haikubali ndo mwisho.

Hiyo machine in HD hiyo moja tu? Kama ni hivyo maana yake umetoa windows umeweka HD ambayo haina kitu chochote, hakuna OS ya kufanya boot, so itabidi uweke windows upya. Pia laptop inapofanya boot jaribu kuingia BIOS uone kama HD inaonekana, kwa probook naamini inabidi urudie ESC wakati unaiwasha itatokea boot menu, kisha F10 kuingia bios.

Option nyingine ambayo ni complicated zaidi ni kufanya clone ya ile ya zamani kuja kwenye mpya ili ubebe windows na kila kitu uhamishe kwenye mpya, hii itahitaji PC yenye uwezo wa kuinstall HD zote mbili ili ufanye clone au uwe na external case ya M2.

Kama hiyo ni HD ya pili na ile ya windows bado ipo na PC inawaka hadi windows jaribu kufuata hatua hizi ndani ya Windows Initialize new disks
 
Back
Top Bottom