Diwani
JF-Expert Member
- Oct 25, 2014
- 2,677
- 2,770
Huenda sipo peke yangu hivyo labda maada hii inaweza kuwagusa na wengine watakaoamua kujifunza kutoka kwa wanachama wengine.
Mwaka 2017, rasmi nilikabidhiwa urithi wa marehemu baba yangu ambaye alikufa miaka mingi iliyopita, kitu pekee kuhusu nyumba yetu ni kuwa, hakukuwahi kuwa na migogoro mingi kama zilivyokuwa nyumba nyingi huko kwenye maeneo mengine.
Kiufupi si nyumba ya kifahari, ni ya kawaida sana kwa mazingira ya mjini. Kinachonisikitisha ni kuwa mara nyingi imekuwa nyumba ya kufanyiwa ukarabati ilhali hali yenyewe si nzuri kwa upande wangu.
Nimewaza kuuza, ila naona kama si vizuri, nimeweza kurekebisha lakini sijui pa kuanzia, marekebisho ni makubwa na hayaendani kabisa na kipato changu.
Nimeleta kwenu mada hii kuomba msaada wenu wa dhati ambao huenda ukanipa mwangaza wa kufanya maamuzi sahihi.
NB: Nyumba ipo Dar es Salaam.