Msaada: Nimetapeliwa milioni 1

Cha kumshauri sina manake mtu anakuja kuweka mil 2 kwenye m pesa na wewe unamkubalia kirahisi rahisi .
sasa mkuu akatae kwanini wakati pale yuko kwa ajili ya kuweka na kutoa pesa!..anachojali yeye hiyo pesa iko kwenye akaunti yake au la!
 
next tym mwambie boss wake abandike note fake hii ni njia ya kuwaonesha/kuwatisha na kuwa makini kuzifaninisha na zile but noti halal huwa zinakaharufu kake na huwa zinamng'ao wake ang'avu but noti fake lipolipo tu
Na ikiwezekana aweke mashine ya kubaini note fake
 
Hapo hakuna ujanja mwingine. Kilichobaki ni kulipa tu au bosi wake amsamehe ! Hakuna namna. Awe makini next time. Watu hawana huruma...isipokuwa wachache tu!!
 
Kama jamaa yako alikabidhiwa electronic device for notes counting and detection of genuinity, na pengine alifanya uzembe hakuzipitisha kwenye hiyo mashine au hakufuata maelekezo ya matumizi ya hiyo mashine(i.e denomination set-ups) basi yupo liable na he/she has to pay for the shortage.
Ila kama hapo ofsini hakuna hiyo device basi ana haki ya kutolipa hiyo shortage make sio kila fake notes zinaonekana kwa macho wala texture yake na wajibu wake sio detecting fake notes bali is all about serving customers by receiving and handing out cash money.
 
Kama jamaa yako alikabidhiwa electronic device for notes counting and detection of genuinity, na pengine alifanya uzembe hakuzipitisha kwenye hiyo mashine au hakufuata maelekezo ya matumizi ya hiyo mashine(i.e denomination set-ups) basi yupo liable na he/she has to pay for the shortage.
Ila kama hapo ofsini hakuna hiyo device basi ana haki ya kutolipa hiyo shortage make sio kila fake notes zinaonekana kwa macho wala texture yake na wajibu wake sio detecting fake notes bali is all about serving customers by receiving and handing out cash money.
 
Nenda polisi mkuu, atakamatwa kwa njia nyingine hats kama kabadili simu.

Unless huyo mtuhumiwa akutwe na pesa nyingine za bandia, itakuwa ngumu sana kumtia hatiani kwa kosa hili la jamaa kutapeliwa.. Kitakachogomba hapo ni ushahidi wa kuthibitisha kama huyo mtuhumiwa ndio alietoa hizo hizo noti bandia..

Umakini unatakiwa katika kuhakikisha uhalali na kiwango kamili cha malipo..
 
Pole sana,
Kwenye hizi huduma hizo pesa bandia zinazunguka sana.
Nilienda kutoa pesa kwa wakala dada akanipa pesa feki laki mbili, nilipoanza kuhesabu pesa ndio nikagundua kuwa pesa ni feki.
Huyu bado anaisaidia polisi. Kuweni makini hizo pesa ni nyingi mitaani, ukizubaa tu unapewa.
 
Huko polisi aende kukamilisha ratiba tu lkn asitegemee kupata msaada wa maana. Mimi niliibiwa katika account yangu ya Tigo pesa 1 m na nilifuatilia Tigo niakipata ile namba pesa iliyojitumia na nikapewa watu 10 anaowasiliana nao marakwamara na sehemu alipoenda kutolea kazi ilibaki kwa polisi tu kwenda Tigo waombe iwashwe GPS ili tujue jamaa yuko eneo gani wakamkamate. Niliambiwa nitoe laki tatu kwaajili ya mafuta na yakuwalipa watakaoenda ktk operation.
 
Majigo akaripoti polisi na kama ana namba ya yule mwizi basi mchezo ushaisha huo,andaeni hela ya kuwapa hao jamaa watawasiliana na mtandao wa simu kuomba call logs za huyo mshkaji,hata kama amezima simu watacheki lazima kuna namba moja ambayo anawasiliana nayo sana mfano mke wake au demu wake,basi akikamatwa mkewe au dem na jamaa mshamtia nyavuni. Ndio umuhimu wa kusajili line walisema tcra.
 
Wiki 1 iliyopita, rafiki yangu kapatwa na maswahibu ya kusikitisha mno.!
Yeye ni muajiriwa katika duka la kutoa na kuweka pesa kwenye mitandao ya simu!Kuna jamaa akaja kuweka pesa tsh milion 2 baada ya kumtumia zile hela na kuondoka.Akabaini mil 1 kati ya zile hela, toka kwa yule jamaa ni feki (hakuwa mzoefu kujua uharali wa fedha).

Amechanganyikiwa kwani namba ya yule mwizi, haipatikani hadi sasa na hatujui la kufanya! Bosi amemkaba alipe hela zilizopotea.

Jana kanipa taarifa hii na ameomba ushauri atazipata vipi hela zake kwani kwa sasa ana mzigo wa kulipa deni, kupitia mshahara wake.

Karibuni wakuu..Pia Samahani kwa kuwachosha!

Jigo
Badili kichwa cha habari, andika RAFIKI YANGU AMETAPELIWA MILLION 1
 
Back
Top Bottom