NYOTA YA JAAH
Senior Member
- Sep 14, 2022
- 142
- 220
Habari, Jamani naomba msaada wa aina yeyote ile, nimechanganyikiwa sana sana. Niende kwenye mada;
Mimi ni dada ambaye najishughulisha na biashara ya kuuza matunda, sasa basi nimepanga mahala naishi mwenyewe, nina tabia ya kuhifadhi pesa ndani, yaani ule mfumo wa kuweka kwenye kibubu. Yaani hizi ambazo naweka kwenye kibubu ni kwa ajili ya kulipa Kodi, kwahiyo ndio maana nahifadhi ndani.
Nimeanza kuweka pesa toka mwezi wa 5 mwaka huu, nahifadhi kwa ajili ya kulipa Kodi kwa ajili ya muhula unaofata, Kodi yangu yaisha mwezi wa 10.
Jana wakati nimepumzika nikajikuta natamani kujua hadi sasa nimefikisha sh. ngap ili nione kama naweza kulipa kabisa au niongeze ili itimie nilipe Kodi yangu ya mwezi unaofata, chumba nalipa elf 50 ambayo huwa nalipa kwa miezi 6 ili niwe huru kufanya mambo mengine.
Cha ajabu nilichokuta sijui hata niseme nini, yaani niliishia kulia na kucheka kwa pamoja! Nimekuta elf 30 tu wakati nilikuwa lazima ingekuwa hata laki 2 au zaidi.
Jamani jamni hali ilivyo ngumu halafu unapata janga kama hili kiukweli niliishiwa nguvu, tangu jana hadi leo sijatoka kwenda kokote, nahisi kama naumwa.
Jamani kwa anayefahamu haya mambo ya Chuma Ulete naweza rudisha pesa yangu na kama inawezakana je nifanyeje au ndio nishikuru tuu niongee na mwenye nyumba mapema anipe muda wa kujitafuta?
Yaani sijui hata la kufanya, please please naomba mnisaidie cha kufanya sielewi nifanye nini!