Msaada: Nahitaji passport ya kusafiria

Kwa ninavojua na experience nliyona mwezi mmoja hauishi huwa ni siku14 tu ukifanya taratibu zote tena online unaenda tu wilayani wanakupitishia, mwisho mkoani kwa 150000, ila express mmhh
Shukran sana mkuu
 
Sasa kwa Zimbabwe si hata hutafuti visa ni passport tu ndani ya siku 14, ila unaanzia mwenyewe online unapata ile form unajaza watakuomba viambatisho utaeka, utaenda uhamiaji wilaya atakupitishia tena km hana shaka na uraia wako kama jamaa wa mipakani labda umpe ten ya shukrani then uende mkoani napo hapana mzunguko ni vimaswali kidogo tu, anapitisha anakupa control number unalipia unangojea siku 14 tu
Shukran mkuu🙏🙏
 
Habari wakuu nimepata mchongo wa kazi nje ya nchi, nimepewa taratibu za kupata passport na inachukua muda wa mwezi na week kutoka, naombeni msaada kama kuna njia naweza kutumia kuipata kwa siku 7. Kila kitu kinachohitajika ninacho.

Natanguliza shukran🙏
Nikuazime yangu?
 
Andaa nyaraka zako Zote zinazohusu uraia wako, sababu ya kuhitaji passport, taarifa za huyo mwenyeji wako huko uendako, kama ni biashara, muariko, shule nk,,, harafu Andaa kibunda maana kwa taratibu kabisaaaa mpaka kupata passport kwa mwez mmoja, 150000,,ila Kuna express 1,000,000 hiyo ndani ya siku moja mpk siku saba! Lkn utapata passport baada ya mamlaka kujiridhisha kama unastahili kupata, kwakuwa lazima wafanye nyatu nyatu. Kala la kheri mkuu huko ughaibun
Duh! Milioni? Mbona kubwa sana mm nimepata passport yangu ndani ya wiki na siku tatu kwa Tsh. 450,000/- tu
 
Kila kitu unacho kwenye simu msaada wa nini sasa jaza maombi fomu zipo kwenye simu yako kisha zitume hizo fomu kesho uende ofisi ya karibu nawe
 
450,000 ina maana ulitoa 300,000 ya ganji au vipi
Ndio mkuu maana hapo ni kama nlitoa 470,000/- malipo ya passport yalikuwa 150,000/- 130k ya passport 20k ya fomu jumla ndio hiyo 150k ila ilipidi nitoe 20k ya mwanasheria sjui kuna kuapa mahakamani (ila wanatoa hapo hapo hakuna kufika mahakamani) maanake kwenye hiyo 470k malipo halali ilikuwa 150k ambayo ndio ina risiti hiyo 320k haina risiti
Passport ilipofika yule askari alinicheki mwenyewe nikachukue
 
Back
Top Bottom