Msaada mwenye uzoefu/utaalamu na biashara ya chakula(mama ntilie)

Ukijua unataka kwenda kuuza wapi ndipo itakuwa rahisi kupata mchanganuo wa gharama na bei ya kuuza chakula pia. Location ina matter.
Sawa. Nimekusoma mkuu, location ni mtaani naweza sema kwa kuwa sio centre kihivyo ingawa kuna biashara nyingine mchanganyiko
 
Siku ungepata wasaa, ungemtafuta mama Ntilie mmoja, unakula kwake mara 2 uku unaangalia vifaa vyake afu siku ya tatu unamuuliza changamoto zake.
Okay, hili la maana sana.
Ingawa nimefanya mara moja lakini nimehis kama hajafunguka vile nnavyotaka mimi
 
Okay. Mi ninavyoamini.

1. Vifaa vya kupikia
  • ASUBUHI: Kikaango cha chapati na vya kukandia, jiko la mkaa na la gesi dogo, sufuria za supu &maharage, flampeni la maandazi na vifaa vyake, kama utapika vitumbua utahitaji pia kaangio lake.
  • MCHANA: Sufuria za wali na ugali, sufuria za mboga mbalimbali.
  • JIONI (kama utakuepo): Itafanana na mchana.
2. Vifaa vya kupakulia
  • Sahani, Bakuli za mfupa na udongo na za bati, vijiko, mahotpot kadhaa na vyombo vya kuwekea maandazi, chapati na sambusa.
3. Fenicha za kukalia wateja na Meza
  • Utampata fundi selemala mzuri akutengenezee pahala pa kukaa wateja, pawe na kivuli na upepo mwanana, pasiwe jirani na vumbi wala harufu yoyote, aweke benchi simple na meza kadhaa.
USHAURI:
  • Biashara nyungi zina feli au kufahuru, ila mchawi ni vitu vitatu: Location, Eneo na Mahali. Hakikisha unaweka biashara yako mahala ambapo oana raia/wateja.
  • Kua unique, kama unajua kupika pika vitu kama sambusa, bagia, etc ambavyo ni adimu. Mtaani zimejaa chapati na maandazi mabaya sana.
  • Weka huduma safi na fanya delivery kwa watu wa madukani au ofisini.
  • Kuwepo na majinya kunywa ya bure kwa watu wa vipato vya kati.
  • Uza na juice ya bei ndogo kuanzia Tsh mia 5 na kuendelea kama utaweza.
 
Noted Mkuu.
Umetisha sana!
 
Noted Mkuu.
Umetisha sana!
Unataka umama ntilie wa aje kufungua mgahawa au kutembeza? Au plan ni kuuza uzaje.... Hii ya kutembeza naona ni nzuri zaidi

Ukianza na mahesabu ya hadi ununue ma viti mafriji hautoboi, labda kama huo mtaji upo.

Hii biashara mi nilifanyaga enzi hizo nikiwa naishi home, mtaji ni masufuria ya maza 😁. Kuna mdada alikua anauza juice pale mtaani ndo nilimuomba lift akipeleka juice ananipelekea na msosi.

Napika wali, maharage, nyama na mboga za majani tuu...PIKA CHAKULA KIZURI wateja hawaondoki. Na ujiboreshe nunua visahani vizuri hata kama ni cha mfupa ila kizuri sio ile misahani ya mabati

Jitahidi sana uwe msafi, ukishapika kimbia oga ndio uanze kuuza usizunguke zunguke na jasho lenye mixa ya nyanya na vitunguu

Hebu ingia field zungukia humo kwa hao kina mama angalia wanavofanya anza biashara na kidogo ulichonacho, usiombe ombe sana ushauri wa watu UTAKWAMA
 
Umetisha mkuu, nashukuru kwa maoni.
umenipa mwangaza kwa ukubwa
 
Watoto wa shule, wale ni viwavi....wanapenda vingi kachori ni kitu chao pendwa ila pia vyakula vya sukari sukari, ice cream

Nisikutoe kwenye wazo lako lakini la biashara ya msosi nayo ni nzuri pia
Okay, noted mkuu.
Nimehoji kwa kuwa naishi karibu na shule na hilo goli la chakula nililopanga kuanzisha lipo hapa hapa maeneo ya karibu na shule.
 
Aanze wapi? Wewe angalia hili jukwaa wote wanaoomba ushauri kama wanaenda kutekeleza.
Biashara sio kitu cha mchezo mchezo ni vita na ni wachache wanaweza ndo mana wanasema biashara nying hazitoboi miaka 5 watu wanakata tamaa..kuna mdada alifungua sehem anauza vinywaji hata mwezi 1 haukufika akaacha kisa changamoto za business haziwez
 
Siku ungepata wasaa, ungemtafuta mama Ntilie mmoja, unakula kwake mara 2 uku unaangalia vifaa vyake afu siku ya tatu unamuuliza changamoto zake.
Sio rahisi hivyo.

Hawezi kukumegea siri ya biashara ,labda kama ni mtu wako wa karibu.
 
Back
Top Bottom