Msaada: Mifuko ya simenti mingapi hutumika katika matofali ya kulaza?

Standard ratio ya kujenga tofali ni 1:3 hiyo ni sawa na ndoo 6 za mchanga kwa mfuko mmoja [ujazo wa mfuko mmoja wa cement ni sawa na ndoo 2 za lita 20] mchanganyiko huo unaweza jenga tofali 50 za kulala na tofali 70 za kusimama kwa mfuko mmoja. Lakini hiyo inaweza kufikiwa ikiwa tu fundi ataweka uwiano sawa wa udongo wa inch 1 kati ya tofali moja na nyingine. Kwenye ujenzi wa msingi changamoto kubwa kwa fundi ni level hasa kama msingi utakua na steps, hivyo wakati mwingine anaweza tumia udongo mwingi zaidi ya inch 1 kutoka kozi moja ya tofali hadi nyingine ili kuweka level sawa hivyo kutumia udongo mwingi zaidi. Mifuko 20 kwa hizo tofali 950 zilizojenga ni reasonable kiufundi.
 
Back
Top Bottom