Msaada: Kutuma na kupokea pesa kutoka nje ya nchi

namanyele

JF-Expert Member
Oct 19, 2012
1,852
610
Habari wanajukwaa,naombeni kujuzwa kwa wanaofahamu jinsi ya kutumiwa na kupokea pesa toka bara la America na Ulaya,njia gani bora mtu anaweza kutumia ili aweze kutuma pesa kuja Tanzania? je,jinsi gani mtumiwaji anaweza kupokea hizo pesa?
Ahsanteni!

===============================================


Western Union or Money Gram.
Tumia njia hizi na pesa itamfikia mlengwa within 5mins after sending.
Money Gram nenda Exim Bank au Twiga bank na Western Union nenda bank ya poster, Amana bank,BOA etc.....
 
Huwa napokea pesa toka ulaya kupitia account yangu ya bank. Anachofanya mtumaji ni direct deposit kwenye account yangu toka huko aliko. Ila kubali kula hasara maana bank wanafanya conversion (hela ya kigeni-tanzania shillings) kwa exchange rate yao ya siku hiyo ambayo kwa uzoefu wangu huwa iko chini ukilinganisha na kwenye bureau de change. Kama una account ya pesa za kigeni utapokea kama zilivyotumwa ila utachagiwa withdrawal fees ambayo nayo si haba!!

Kwa mwenye msaada zaidi aongeza nyama...
 
Njia mbili rahisi kwanza pesa yawezatumwa moja kwa moja ktk account yako,gharama kwa mtumaji ni ndogo sana yaaani akikutumia $1000 sending charge itakuwa $17 tatizo ni Kuwa huweziipata mda huohuo inachukua siku moja Kama imetumwa siku ya kazi,njia ya pili japokuwa ni gharama kidogo ni western union mfano akikutumia $1000 gharama ya utumaji itakuwa Kama $80 lakini utapata ndani ya sekunde chache,+971504374387 Dubai
 

mkuu lucky sabasaba

ninahitaji msaada wa ushauri wako kwa exposure yako ya huko.. nita ku-pm
 
Last edited by a moderator:
Through bank account by way of swift code, ama acc no,through money gram,western union etc
 
Nilikua nataka kutuma application fee ya chuo fulani nje kidogo ya Tz ila ni Africa hapahapa,

Chakushangaza nimeenda benki ya standard chartered jibu nlilopewa nusu nizimie;

Eti gharama za kutuma kiasi chochote ni $90 wakati mimi nataka kutuma kama $60 hiv.

Sasa wakuu naombeni ushauri, hivi kuna njia gani nyingine naweza kutumia ili nitume hizo pesa au kuna benki Tanzania ina gharama za chini kidogo. Naomba pia kama kuna mtu aliwahi kuomba nafasi za kusoma nje ya nchi anipe uzoefu wake njia aliyotumia kulipia application fee au nikituma pesa ndani ya bahasha kutakua na shida.

Maana hizo $90 mmmmmhhh ni utata (TSH:145,000). Anyhow, I can take risks of that $90 but i need your advice first.

Asanteni kwa msaada




"The secret of health for both mind and body is not to mourn for the past, not to worry about the future, or not to anticipate troubles, but to live in the present moment wisely and earnestly."
 
hz bank zetu ni full ubepari, mimi mwenzio nilitaka kutuma APPL FEES kwa ajili ya Msc Univ of Cape Town, R 20 tu, CRDB wakanambia gharama za kutuma hiyo R 20, ni USD 50, nilichoka hoi! nikamuomba jamaa yng wa CAPE TOWN akanilipie, nikamaliza mchezo!
 
lipia kadi yako ya benk kama una visa au master eg crdb tembo card, fungua hio application form online then lipia kwa online kama chuo kimesimama lazima hizo option tha online payment zitakuwepo na watakukata onlt $10 - $15, umemaliza
 
lipia kadi yako ya benk kama una visa au master eg crdb tembo card, fungua hio application form online then lipia kwa online kama chuo kimesimama lazima hizo option tha online payment zitakuwepo na watakukata onlt $10 - $15, umemaliza

Huu ushauri mzuri, akishindwa atumie Western Union, mimi huwa nacheza na hii.
 

Bank money wire transfer ni gahli po pote duniani, hii ni kutokana na gharama zinazotokana na zinakopelekwa pesa namna ya kuzifidia gharama zake huwa juu. Bora tu kutumia western union. Usifikiri ni Tanzania tu, hiyo ni po pote uwe Asia, Ulaya, Marekani au Australia, utakumbana na hiyo hiyo hata kama unatuma shilingi moja utalipia hizo zote.
 
hz bank zetu ni full ubepari, mimi mwenzio nilitaka kutuma APPL FEES kwa ajili ya Msc Univ of Cape Town, R 20 tu, CRDB wakanambia gharama za kutuma hiyo R 20, ni USD 50, nilichoka hoi! nikamuomba jamaa yng wa CAPE TOWN akanilipie, nikamaliza mchezo!
Daah mimi nataka nitume botswana halafu deadline ni tar 28 mwezi huu.. sina jinsi itabidi nitoboke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…