Msaada: Bachelor of information technology 'IT'

Ulimwengu wa ICT ni mpana na upo supa

Unapenda yaliyomo katika kozi hiyo au bado hujasoma kabisa kufahamu?
 
Heshima yenu wakubwa

Nahitaji kujua endapo ukasoma information technology ajira zake zina base sana katika nini?

Yaan namaanisha unaweza kuajiliwa katika nyanja zipi?
Na je,ni marketable kama course za afya???

Nahitaji msaada katika kujua ili.
Ahsante
 
ajira za kuajiriwa upande wa IT ni chache sana na ngumu kupata, japokuwa ina fursa nyingi kama ukipekecha kichwa vizuri hela ya kula hukosi, kikubwa kama unasoma hiyo kozi malengo yako makubwa yabase kwenye kujiajiri kuliko kuajiriwa, ila kama unataka kuajiriwa kwa haraka basi soma kozi za afya, IT haifai.
 
Ahsante sana mkuu
 
Wakuu nina mdogo wangu kapata four ya 26 ana eng_c kiswahili_c geog D History D B/M_D bios_D na civics D je anaweza kasoma diploma ya IT? Na ni chuo gani hapa dar ni kizuri kwa IT anachoweza kupata kulingana na marks zake?
 
certificate, anaweza kusoma nadhani UCC kinafaa.
 
Kwa wale ambao ni walemavu wa kifikra kwamba ni lazima uajiriwe IT haifai. Ila kwa wale ambao wamefunguka bongo zao, It ndo kila kitu kwani unaweza kujiajiri au ukapata mafanikio makubwa sana.
Kwamfano ukajiajili unakuwa unajishugulisha na nn zaidi
Naomba nieleweshe apo
 
Kwamfano ukajiajili unakuwa unajishugulisha na nn zaidi
Naomba nieleweshe apo
IT inahusisha vitu vingi, baadhi ya hivyo ni.

Artificial intelligence

Computer Programming

Networking designing and Administration

web server management and website designing

Computer maintenance

System analysis and design

computer graphics,

Database implementation and management

na vingine vingi ambavyo chuo hamfundishwi kwa hiyo ni wewe kujiongeza, sasa kama ni kujiajili hapo ni akili yako na jinsi gani unaweza tumia hayo maarifa ku-earn pesa, mfano unaweza ukawa ni software ama website developer na hapa unahitaji kufanya kitu kinachoweza mvutia mtu kufanya kazi na wewe, matumizi ya simu sasa ni makubwa hapo inabidi ujifunze hata app developing na ku-repair simu na kompyuta, kiufupi mr ni kuumiza kichwa, hivyo ni vichache ambazo unaweza kujiajiri mwenyewe.
 
ajira za kuajiriwa upande wa IT ni chache sana na ngumu kupata, japokuwa ina fursa nyingi kama ukipekecha kichwa vizuri hela ya kula hukosi, kikubwa kama unasoma hiyo kozi malengo yako makubwa yabase kwenye kujiajiri kuliko kuajiriwa, ila kama unataka kuajiriwa kwa haraka basi soma kozi za afya, IT haifai.
Duh kwa hio id yako nahisi kuna mtu ujumbe ameupata
 
Back
Top Bottom