Mrejesho wa kutafuta kazi

Kenjay

Member
Jun 26, 2024
82
251
Habari za siku kadhaa ndugu zangu.

Narudi tena kwenu wakuu. Week kadhaa zilizopita nilileta bandiko la kutafuta kazi hapa, sipendi nieleze tena mapito yangu ila nataka kusema tu bado kwa upande wangu giza ni kubwa sioni mwangaza

Nimejaribu haya kwa upande wangu

1. Nimejaribu viwandani, nilienda kiwanda cha rasta pale mbagala lakini nilishindwa sababu ya kwamba hawalipi kwa siku wao wanalipa katikati ya mwezi na mwisho wa mwezi, ambapo kwa upande wangu ni vigumu sababu mimi nahitaji hela ya mlo wa siku na familia. Sikuweza kwenda viwanda vya kubeba vitu vizito sababu nina shida ya mbavu

2. Nimejaribu kusema na ndugu zangu wa karibu japo wanikopeshe mtaji nifanye business, niliwaza kufanya biashara ya kuku wa kuchoma, phone accessories, vile visendo vya kina dada au nyingine yoyote mradi kipatikane kipato kwa siku lakini bahati mbaya ndugu nao wanasema hawana kitu

3. Nimejaribu kutafuta mteja ili niuze eneo langu lipo huko mkoa wa kusini nusu eka, nililinunua nilipokuwa huko maana nilipata kazi ya kusimamia mradi wa mtu kwa muda. Lengo ilikuwa niuze nipate mtaji maana sina jinsi, lakini nalo kwa bahati mbaya sijapata mteja mpaka sasa

4. Nimejaribu kadili ya uwezo wangu kutafuta channels sehemu tofauti tofauti lakini wapi! Bado naona giza

Naishi vipi sasahivi?

Kiukweli kwasasa wife ndio anapush jahazi hivyo hivyo mdogo mdogo. Ipo hivi, baada ya upande wangu kuona mambo magumu ikabidi nimwambie yeye ajaribu kutafuta hata hizi za mama lishe za 3000 kwa siku, Mungu ni mwema kweli kuna sehemu amepata ndio hapo anajishikiza, akipata hiyo 3k akitoa nauli 1000 inabaki 2000 ndo anarudi na chochote cha kula siku hiyo.

Kwanini nimerudi tena? Nataka nini?

Kiukweli ndugu zangu hii ishu anayofanya wife mpaka mwenyewe namuonea huruma, huwa ananieleza changamoto anazokutana nazo nadhani wenyewe mnajua wanayopitia mama lishe, mbali ya hizo changamoto ni kwamba ikitokea siku biashara imeenda vibaya basi ndo harudi na chochote. Kwa upande wangu nashindwa tena kutoka kuangaika sababu yeye akitoka asubuhi mimi nabaki na watoto kuwazingatia mpaka usiku anaporudi kwahiyo siku inaisha hivyo.

Sasa nimerudi tena kuwaomba ndugu zangu, sihitaji msaada wa pesa hapana ila nipe tu kazi kama unayo ambayo naweza kupata kuanzia 5000 kwa siku utakuwa umenisaidia sana ili tu huyu mama nimpumzishe nyumbani awalee watoto wake vizuri. Hiko ndicho ninachohitaji ndugu zangu hata kama kazi yako inatoa ujira kwa mwezi, me nilipe tu kwa siku ili family ipate kula basi! Vinginevyo naona kabisa mzigo unanielemea halafu wa kunitetea sina

Kuna muda napata mawazo mabaya ya kumkosea Mungu lakini kila nikifikiria naona hata! Huu mzigo ni wangu sina wa kumuachia! Labda ningekuwa mwenyewe pengine ningesema nikajaribu maisha nchi za watu hapa bongo pamenikataa.

Naomba mnishike mkono ndugu zangu. Asanteni, usiku mwema
 
Hilo eneo liko sehemu gani mkuu?
 
Kuna watu wanapitia mengi kuliko wewe ila trust me muda niwakati sahihi utakuja kubutua maisha utakaa uamini. Kwa sasa mungu yupo anampima mkeo na uvimilivu wake kupitia kwako. Ila usivyo kuwa na akili Mungu anaweza kukufungulia milango alafu ukajikuta umememuacha huyo muke wako.
 
Hapana mkuu siwezi kufanya hivyo Mungu anisaidie katika hilo. Pia asante kwa dua yako njema
 
Ndungu yangu sisi binadamu tuna mapungufu mengi muno. Usije kuchukulia matatizo yako kama vile mungu amekusahau. Kuna matatizo mengine Mungu anakupa challenge ili kukupima.Wakati mwingine Mungu anakupa mitiani ila ufahamu watu sahihi wakutembea nao wanaweza kuwa ndugu jamaa au malafiki. Ufanye huu wakati kuwa mwalimu wako.
 
Fika pale kituo cha nguvu kazi cha daladala. Kuna madereva wa bodaboda, waambie wakupeleke mabanda ya kuku. Huko utapata taratibu zote za kuingia kazini.
Sawa mkuu nimekupata, hii nitajaribu kesho kwenda sababu kesho wife anapumzika haendi kibaruani. Na je unaweza kunipa maelekezo haya machache kama unafahamu?

1. Wanalipa kwa siku? Maana ninachokitaka mimi ni mlo wa siku tu basi, ikizidi hapo ni mapenzi ya Mungu nitashukuru

2. Je naweza kwenda hata kwa mguu? Kwa boda sitoweza nauli. Kama inawezekana basi nielekeze tu nikifika hapo niulize kampuni gani hiyo au ni kwa mtu?
 
Ndungu yangu sisi binadamu tuna mapungufu mengi muno. Usije kuchukulia matatizo yako kama vile mungu amekusahau. Kuna matatizo mengine Mungu anakupa challenge ili kukupima.Wakati mwingine Mungu anakupa mitiani ila ufahamu watu sahihi wakutembea nao wanaweza kuwa ndugu jamaa au malafiki. Ufanye huu wakati kuwa mwalimu wako.
Asante mkuu nilizingatia hilo. Naamini Mungu ni mwema nitavuka ktk hili
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom