Mrejesho: MwanaJF aliyeomba mtaji

If you are serious ni pm, ukieleza uko wapi, unafanya nini, unapokwama ni wapi, kwa nini unakwama, ungependa usaidiwe nini, mchanganuo wa unachotaka kufanya n.k.

Lakini badala ya ku pm, unaweza pia kuchanganua hapa anaweza akajitokeza mdau akakuunga mkono.
nipo morogoro.
 
natamani kufanya hichi kibiashara lenfo kbwa ni kupandish mtaji.
kwa mtu atayekuwa tayari anisupport kupata hivi.
bench mbili ndefu, mbili fupi kiasi
meza moja ndefu futi nne na nusu na upana wake futi mbili.
kitivi kidogo kwa ajili ya wateja
mabirika manne. makubwa mawili na madogo mawili
kahawa na tangawizi
karanga mbichi na za kukaangwa
kashata
themosi nne zote mdogo
vikombe vidogo pic20
vikubwa pic 20
vikombe vya plastic saiz ya kati pic20.
asante sana
Mkuu samahani, hii nilikuwa sijaiona. Ushauri wangu kabla ya kuanza hiyo, anza kuuza ftari hapo morogoro mjini kuanzia wiki hii ramadhani inaanza, mpaka ramadhan inaisha, utakuwa tayari una mtaji wa kuanzisha biashara ya kahawa ambayo itakuwa kwenye kiwango cha juu na utatengeneza faida nzuri ndugu yangu.

Usiwe na aibu wala usijivunge kabisa, funguka, jitume, penda unachofanya na kuwa mwaminifu halafu utakuja kuniambia.

Ila pia wewe si unatumia smart phone hapo? Kwa nini usiiuze, ukanunua kasimu simple halafu ukapata mtaji wa kuanzia?
 
Hajafanya kitendo kizuri na nonawachukia sana watu wa aina hiyo
Amewaharibia na wengine watakaokuja wako serious wanahitaji msaada wote wataonekana ni matapeli sababu ya mjinga mmoja tu
 
Mkuu samahani, hii nilikuwa sijaiona. Ushauri wangu kabla ya kuanza hiyo, anza kuuza ftari hapo morogoro mjini kuanzia wiki hii ramadhani inaanza, mpaka ramadhan inaisha, utakuwa tayari una mtaji wa kuanzisha biashara ya kahawa ambayo itakuwa kwenye kiwango cha juu na utatengeneza faida nzuri ndugu yangu.

Usiwe na aibu wala usijivunge kabisa, funguka, jitume, penda unachofanya na kuwa mwaminifu halafu utakuja kuniambia.
asante kwa ushauri kaka.
 
Na hiyo itasababisha watu wenye shida wasisaidiwe, kumbe pengine wako serious. Sema tu sisi wengine tatizo letu tuna huruma saja jambo ambalo mara nyingi hutuponza.

mkuu uko right kabisa sometimes unakuwa na nia kabisa ya kutoa msaada ila watu wa namna iyo ndo wanakwamisha

usiache kutoa msaada toa kadri uwezavyo na kipato icho icho kidogo ulicho nacho Mungu yupo asipo kulipa hapa duniani ata kesho akhera atakulipa Inna Shaa ALLAH
 
Nyota ndogo aliwahi kusema: Kuna watu na viatu.

Pole mkuu kwa hilo. Ila usichoke kusaidia pale unapoguswa na ukawa na uwezo.

Uaminifu ni nguzo ktk maisha. HONESTY is always the best policy.

-Kaveli-
 
mkuu uko right kabisa sometimes unakuwa na nia kabisa ya kutoa msaada ila watu wa namna iyo ndo wanakwamisha

usiache kutoa msaada toa kadri uwezavyo na kipato icho icho kidogo ulicho nacho Mungu yupo asipo kulipa hapa duniani ata kesho akhera atakulipa Inna Shaa ALLAH
A amin!
 
Mkuu ulikosea sana kumpa mtu mtaji pungufu hakika hawezi anzishaalichopanga sababu ya pungufu.. trust me ulipompa pungufu kama mikosi maana kila atakalofanya litakuwa na mapungufu nina uzoefu huo wa aina yako kuna hadi ndugu na jamaa waliopewa kwa aina hiyo wote walifail na muhimu kumsaidia mtu 100% alichopanga na atafanikiwa tu hakika ila pungufu never... me nakulaumu wewe na utakuwa umepa forever stress katika maisha yake kwani hatoacha kujilaumu milele na hiyo itamuondolea confidence kuwa hawezi chochote.. ndio maana hata Mabank yanawanyang'anya wafanyabishara Mali sababu huwa hawatoi 100% so wafanyabiashara hufail tu maana kujazia lazima akakope pengine na alipe huko kwanza huku bank inamuwait mwishowe ni failure
 
Hahaha, mkuu sio kondooo. Ni nini kinachoweza kumtofautisha binadamu na wanyama wengine?
Basi wewe walii.

Huyo shweini katufungia mlango wengine kesho tukose pa kukopa kwako pedeshee, maana naona utakuwa huna imani nasi wabongo tena.
 
Daaah kafanya vbaya sana. Ndi maana wengne wanakua hawasaidiwi. Ila hzo hela hajafanyia la maana ndo maana akakuzungusha, kashaipga kbrti.
 
Mkuu hapa ni sehemu ya kupeana msaada wa mawazo, CASH katoe kwenye kituo cha watoto yatima.
 
Mkuu nimependa sana way ulivyo na uthubutu japo ilikuwa mbaya Kwa mlengwa ila huyo jamaa angejielewa asingejuta.
(Kweli penye miti mingi hakuna wajenzi)
 
Yaani sijui tunaenda wapi aisee.Ni shida, maana sasa kila mtu atakuwa anamuogopa mwenzake halafu hata mtu akiwa na shida serious, watu watadhani ni uhuni na hakuna atakayechukua hatua
Yeah halafu inaweza kukuharibia baadae huko mbeleni ukapata mikosi halafu ukaishia kusema wananiloga kumbe ni kujitakia
 
Na hiyo itasababisha watu wenye shida wasisaidiwe, kumbe pengine wako serious. Sema tu sisi wengine tatizo letu tuna huruma saja jambo ambalo mara nyingi hutuponza.
Kuna member humu alikuwa na matatizo akahitaji msaada, nilimsaidia, akawa anatoa mrejesho kwenye Mp mpaka akaweza fika kwangu ila mimi sikuwepo. Sasa hivi ana kazi na huwa anawasiliana na pale nyumbani hivyo kuna wengine matapeli lakini wengine ni watu wanaojitambua.
 
Kuna mwanafalsafa mmoja alitusisitiza wanadamu juu ya umuhimu wa kushuku kila kitu.Jamaa alikuwa akishuku hata uwepo wake mwenye. Ila ikafika hatua akahitimisha kuwa kwa kuwa anafikiri, basi atakuwa yupo, kwa hiyo angalau hilo ndilo jambo pekee ambalo ana uhakika nalo, lakini nalo tena baadae akaja kulishuku pale alipojiuliza kwamba hivi kwa kuwa mtu anapoota anadhani yuko kwenye ulimwengu halisia hadi atakapoamka, sasa je kama vile anavyodhani anafikiri yuko ndotoni tu?

Kwa hiyo sikushangai mkuu.Unafuata falsafa ya Descartes.
ungefuata ushauri wangu yasingekuwa hayo
 
Ndiyo sababu wengine humu tunafikiria mara mbili mbili kutoa msaada kwa kuhofia kutapeliwa.

Miezi michache iliyopita kuna mtu alikuja kuandika hapa kwamba amepungukiwa pesa ya ada shuleni. Kuna bi dada mmoja mwenye roho nzuri sana humu akawasiliana naye na kumsaidia pesa za ada na pia za matumizi.

Kwa mshangao wake zikawa zinaibuka IDs mpya na nyingi hata kabla ya kuandika humu wenye ID zile wakawa wanaandika moja kwa moja kwake kuomba msaada kwa matatizo mbali mbali ya kimaisha. Machale yakamcheza ndipo akaniomba ushauri afanye nini,

Mie nikamwambia uwezekano mkubwa ni mtu yule yule anataka kuchuma zaidi toka kwake.

Kuna watu wana shida za kweli kabisa lakini kabla ya kujitoa kusaidia ni lazima mtu/watu wajiridhishe kwa kina kwamba huyu anayehitaji msaada ni kweli anahitaji msaada au ni tapeli tu.
 
Back
Top Bottom