Mrejesho: Matokeo ya Usaili kwa kazi niliyotangaza humu

itakuwa hawakujua, lakini nasikitika kuwa hakuna anayejiyejitokeza kusema yeye ni miongoni mwa hao unaowazungumia wewe (yaani alitumiwa, akataka kurejesha ila hakupata namba). Tuseme hao unaowazungumzia wewe watakuwa wana bahati mbaya kama wale ambao wanaweza wasielewe interview itafanyikia ukumbi gani amma kwa uzembe au kwa bahati mbaya, hawa nao huwa wanakuwepo ndio, na kama anatafutwa mtu mmoja walioomba ni 2000, hiyo ni moja ya njia zinazotumika kupunguza watu (suala la kuwa ni nzuri au mbaya huo ni mjadala mwingine).
Ungetaka kutenda haki Kwa hao washiriki wote ingetumia namba yako ya Tigo kuwa rushia hela watu wa Mpesa kwani lingetokea namba ya simu
 
Wakuu nawasalimu.
Nilitangaza nafasi ya kazi humu ya usimamizi wa biashara ambapo kigezo cha kwanza nilichokuwa nimetoa ni uaminifu.
Nafasi ya kazi kwa mtu mwaminifu sana

Matokeo ni kama ifuatavyo:

(a) Watu 81 waliomba kazi hii.
(b) Watu 29 walijibu maswali niliyouliza ya kupima uaminifu na wakathibitisha kuwa uaminifu wao hauna shaka, hivyo kupita kwenye hatua ya kwanza ya usaili.
(c) Katika hatua ya pili ya usaili, nilichagua waombaji 15 kutoka kwenye 29, hapo juu, nikawatumia fedha kwa tigo/mpesa kwenye namba walizonipa (kutoka kwenye namba wasiyoijua bila maelekezo yoyote. Kiwango nilichotuma kwa kila mmoja ni kati ya ya 2000 - 10,000/=. Kati ya hao 15, 13 walipokea hela wakazilamba bila hata kuuliza mtumaji kama alikosea namba au alituma kwa makusudi na kama alituma kwa makusudi alituma za nini.(hatua hii imewafanya kushindwa usaili).Watu wawili waliuliza, nikawambia nimetuma kwa makosa, wakaonesha dhamira ya kunirudishia ndio nikawajulisha kuwa ilikuwa ni sehemu ya pili ya usaili wa kazi hii. (hao wawili wamefaulu usaili kwenye hatua hii) na kati yao mmoja atapewa kazi.

Nawatakia kila la heri.
mkuu hii imenikumbusha mbali, ilimkumba mtu mmoja kule geita, yy aliomba kazi ya udreva mgodini, na akapata

siku ya 1 anaingia kazini akapewa gari, mpya ila boss wake kampa kama laki 4 hiv kamwambia aende shell akalijaze mafuta, jamaa kaingia kwenye gari akaona mafuta yapo full , sasa akajiuliza mbona mafuta yapo full?

wakati anashangaa yule boss akamwambia afanye haraka maana wanasafari ya kwenda mwanza, jamaa akaondoa gari, alipofika mjin akazunguka zunguka kisha akarudi site, na list ya mafuta, jamaa akamuuliza umejaza mafuta? akajib ndiyoo, ok jamaa akamwambia weka mizigo kwenye gari,

baada ya dk kama 5, akaitwa ofcn akaambiwa na boss huna kazi maana umedanganya gari lilikuwa na mafuta, hyo pesa utatumia..... jamaa alikuwa amesain mkatab wa kulipwa m.1.5 alilia kama mtt. bt haikusaidia
 
Inaonekana kushukuru kwako ni tatizo, mwenye tigopesa amekosea kufanya transaction. Mtu kaacha shughuli zake na inawezekana katumia nauli ili amrudishie pesa halafu hata asante ikamshinda.Wewe bado unang'ang'ania kuwa ni haki yake. Kwa hiyo aliyerudisha pesa hana haki, na vipi kuhusu muda wake aliopoteza.
Tenda wema nenda zako! Unalilia shukrani ya nini? Ili ikusaidie nini? Kama kuna gahrama umetumia na ungependa kurejeshewa sema tu, siyo ukae unalialia kwenye mitandao!
 
Yes nilirudisha kwa sababu niliona haitanisaidia chochote...ningekula na mwisho wa siku ingeisha na thamani yake ingekuwa haipo tena. Kwangu utu wema ni wa thamani kuliko dhahabu..yani hakuna thamani yoyote inayozidi hapo.
Yes hela ilikuwa yake na ilikuwa wajibu wangu kumpelekea lakini neno asante ni la thamani sana. Ujue kwa jinsi alivyochukulia poa hadi nikahisi huenda mimi ndo nimechanganya mahesabu.Kwa kweli mtu asiyejua kusema asante mimi huwa ananishangaza sana aisee
Uaminifu hauna kiasi nduguyangu, 1bl inaweza kukusaidia chochote...unaweza kuiiba? Last two weeks jamaa watatu kutoka ethiopia wakiwa airport uchina walisahau sehem flani dola laki kadhaa, walijua ndiyo basi tena ishakula kwao, lakini aliyeziokota aliziwasilisha kwa askari, askari nao walifanya jitihada wenye oesa zao wakapatikana wakarejeshewa pesa zao zikiwa kamili. Ingekuwa Tanzania hapo zingepotelea hata mikononi mwa polisi!
 
Nimeshakwambia mimi uaminifu wangu hauna thamani ya fedha wala dhahabu. Hata ingekuwa billions nini 1 bilion?
 
Wakuu nawasalimu.
Nilitangaza nafasi ya kazi humu ya usimamizi wa biashara ambapo kigezo cha kwanza nilichokuwa nimetoa ni uaminifu.
Nafasi ya kazi kwa mtu mwaminifu sana

Matokeo ni kama ifuatavyo:

(a) Watu 81 waliomba kazi hii.
(b) Watu 29 walijibu maswali niliyouliza ya kupima uaminifu na wakathibitisha kuwa uaminifu wao hauna shaka, hivyo kupita kwenye hatua ya kwanza ya usaili.
(c) Katika hatua ya pili ya usaili, nilichagua waombaji 15 kutoka kwenye 29, hapo juu, nikawatumia fedha kwa tigo/mpesa kwenye namba walizonipa (kutoka kwenye namba wasiyoijua bila maelekezo yoyote. Kiwango nilichotuma kwa kila mmoja ni kati ya ya 2000 - 10,000/=. Kati ya hao 15, 13 walipokea hela wakazilamba bila hata kuuliza mtumaji kama alikosea namba au alituma kwa makusudi na kama alituma kwa makusudi alituma za nini.(hatua hii imewafanya kushindwa usaili).Watu wawili waliuliza, nikawambia nimetuma kwa makosa, wakaonesha dhamira ya kunirudishia ndio nikawajulisha kuwa ilikuwa ni sehemu ya pili ya usaili wa kazi hii. (hao wawili wamefaulu usaili kwenye hatua hii) na kati yao mmoja atapewa kazi.

Nawatakia kila la heri.
Mimi ulinitenga!
 
Kuna wakala mmoja nilimwachia 21,500 aniwekee nikaondoka zangu, Nahisi alikua na wateja wengi Nilkuja pata meseji amenitumia 215,000 badala ya elfu 21 nikamrudishia kesho yake kile kilchozidi, hakuna sababu ya kula kisicho chako
 
Hii nimeipenda.

Kama utafiti unaonesha 71% ya Watanzania ni wavivu, usitegemee mvivu apate kitu cha bure, halafu aanze kuhoji, kuwa ni kwanini kapewa. Wavivu wote wanapenda vitu vya dezo.
Mkuu sawa kabisa.
Kuna kampuni mmoja ya nje ilikuwa inaajiri wafanyakazi Dar.Kitu cha kwanza waneambiwa WaTanzania sio waaminifu Na wavivu.
Kwahiyo Mimi Na wamiliki ya kampuni tukaenda sokoni tukanunua vitu vya Tsh 75k.
Tulikuwa tunaajiri watu 6. Hatukuuliza CV zao Ila kila mmoja tulimpa Tsh100k kwenda sokoni kununu vitu Vilevile tulivyo nunua.
Matokeo watu 3 walinunua vizuri tu Lakini hawakurudisha chenji. 2 walinunua vitu chini ya viwango lakini walirudisha chenji. Na 1 Alifanya Kama alivyo agizwa. Na Huyo ndio aliyepata kazi.
Kwa hiyo UAMINIFU na UMAKINI ni utajiri mkubwa sana.
 
acha zingua wewe! tigo pesa ikileta pesa inaonesha namba au jina la aliyekupigia? na kama ni ivyo alikupigiaje bila kujua namba!?
 
Uaminifu hauna kiasi nduguyangu, 1bl inaweza kukusaidia chochote...unaweza kuiiba? Last two weeks jamaa watatu kutoka ethiopia wakiwa airport uchina walisahau sehem flani dola laki kadhaa, walijua ndiyo basi tena ishakula kwao, lakini aliyeziokota aliziwasilisha kwa askari, askari nao walifanya jitihada wenye oesa zao wakapatikana wakarejeshewa pesa zao zikiwa kamili. Ingekuwa Tanzania hapo zingepotelea hata mikononi mwa polisi!
Bongo nani wa kuzifikisha mikononi mwa Polisi?
 
Back
Top Bottom