Inside10
JF-Expert Member
- May 20, 2011
- 30,625
- 33,960
Mratibu wa zamani wa Miss Tanzania Hashim Lundega, amefariki dunia leo katika Hospitali ya Kitengule - Tegeta, Jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa mshirika wa karibu wa Marehemu Lundenga, Bosco Majaliwa, Lundenga ambaye amekuwa akiumwa kwa muda mrefu, alikimbizwa hospitalini hapo leo asubuhi baada ya kuzidiwa lakini muda mfupi baadaye akafariki.
Lundenga ambaye ameugua kwa muda mrefu itakumbukwa ndio aliyesimamia kwa mafanikio makubwa Mashindano ya Urembo Tanzania na kuyapa umaarufu mashindano hayo.
Lundenga pia aliwahi kuhudumu kwenye Kamati ndani ya Klabu ya Yanga.
Taratibu za mazishi zinaendelea nyumbani kwake Boko jijini Dar.