TANZIA Mratibu wa zamani wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga afariki Dunia

Inside10

JF-Expert Member
May 20, 2011
30,624
33,958


Mratibu wa zamani wa Miss Tanzania Hashim Lundega, amefariki dunia leo katika Hospitali ya Kitengule - Tegeta, Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mshirika wa karibu wa Marehemu Lundenga, Bosco Majaliwa, Lundenga ambaye amekuwa akiumwa kwa muda mrefu, alikimbizwa hospitalini hapo leo asubuhi baada ya kuzidiwa lakini muda mfupi baadaye akafariki.

Lundenga ambaye ameugua kwa muda mrefu itakumbukwa ndio aliyesimamia kwa mafanikio makubwa Mashindano ya Urembo Tanzania na kuyapa umaarufu mashindano hayo.

Lundenga pia aliwahi kuhudumu kwenye Kamati ndani ya Klabu ya Yanga.

Taratibu za mazishi zinaendelea nyumbani kwake Boko jijini Dar.
 
Washiriki wa miss Tanzania toka 1994 hadi 2021 kama sikosei hawawezi kumsahau mzee Lundenga.

Imagine nchi nzima watoto wa miaka 18 hadi 24 ndio Lundenga alikua akifanya nao kazi miaka yote hiyo😂.

Yaani hii season ikiwa inaelekea kuisha tayari ameanzisha pre season ama new season, muda wote ana new stock ya watoto wazuri under 25.

Mzee Lundenga, a life lived
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…