ndolelejiUduhe
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,360
- 2,682
Naunga mkono hoja,Serikali imeshindwa kuuendesha mradi wa mabasi ya haraka dar es salaam kwa ufanisi. Kwanini wasipewe watu mwenye uzoevu wa usafirishaji wa abiria wauendeshe?
Ili mradi huu uende sawa lazima uendeshwe kibiashara badala ya kisiasa. Mwendeshaji afanye upembuzi wa kujua gharama halisi (wafanyakazi, Kodi, vipuli, uchakavu na matengenezo) za uendeshaji kisha wachaji abiria kwa uhalisia.
Pale Ethiopia mabasi ya umma watu wote hata wanafunzi na askari wanalipa sawa. Kule ulaya na Marekani hivyohivyo ila wanafunzi Kuna namna wanavyolipiwa usafiri wao.
Wapewe tu 🙌👍