Mr Nice kawa dereva wa bodaboda?

Liwe fundisho kwa ambao hayajatufika! Tujaribu kuishi maisha ya kawaida hata kama umejaaliwa utajiri.
 
Mambo ya kudharau kazi ni ya kishamba sana, yani kuendesha bdbd unaanzisha uzi?
 
Wabongo bhana!,kweli kikulaachooo,wanaona geleee...mhhh maisha haya yanatana hisabati Sana,wapambe wote wamekimbia.
 
Ya NGOSWE MWACHIE NGOSWE MWENYEWE
unafahamu kuwa wewe pia ni Ngoswe mtarajiwa?usipojifunza chochote kwa ngoswe huyu wa sasa utaishia kuwa ngoswe wa ajabu when you get at the bridge!! You better wake up and live.
 
Msilaumu maisha kama amefilisika "kweli" basi lawama apewe yeye mwenyewe Mr. Nice. Watu tunakuwa wa ajabu sana kila kitu lazima tutafute pa kuangushia lawama. Mara "Maisha" mara "shetani" mara "wachawi" kila mtu ana anatafuta pa kuangushia lawama.

Maisha yako ni matokeo ya matendo yako, hakuna wa kulaumiwa zaidi yako mwenyewe. Na wale wanafiki wanaojifanya wanaouliza "cha ajabu kipi" kwa Mr. Nice kufilisika mpaka kufikia kuendesha "boda boda" lazima watakuwa na wanamatatizo kichwani au zaidi ya hapo.

Ni pa kujifunza ukipata pesa usiwekeze kwenye dhima "liabilities" wekeza kwenye mali "asset" zitakazokuletea pesa kukidhi mahitaji ya kila siku. Mkipata pesa ni baloon, mark x, gambe, pamba, wakina Lulu kwanini usije kuendesha boda boda baadae.
acha ujinga wewe unaweza kuwekeza kwenye mali na bado ukafilisika ukauza kila kitu...unaweza kufanya biashara ukapata hasara ikafa.....maisha hayana formula
 
Mhh! maisha yanapanda na kushuka mimi mwenyewe huwa nampaga lift mkuuwa wa matraffic mstaafu wa visiwani wa miaka ya nyuma huwa namkutaga akipiga mguu (sio mazoezi) cha kunote hapa kuwa ni kuishi kwa uzuri na watu, tena hasa hawa maaskari ndio wanatakiwa waishi vizuri na watu kwelikweli.
 
acha ujinga wewe unaweza kuwekeza kwenye mali na bado ukafilisika ukauza kila kitu...unaweza kufanya biashara ukapata hasara ikafa.....maisha hayana formula

Mdogo wangu "If you fail to plan, you are planning to fail" Nani kakufundisha kuwa maisha hayana formula?

Inaonyesha upeo wako ni mdogo sana na sidhani kama niliyotaka kukufundisha yatakujenga wacha nibaki nayo, inaonyesha una kiburi na hauko kwenye kujifunza sababu unajua kila kitu.

Fahamu njia za kujifunza kwa kuuliza, ili uongeze uelewa halafu upinge kwa hoja si kwa kuanza kukashifu nafsi za watu.

Endelea kulaumu maisha na dunia halafu wenzako wanaojilaumu huwa wanajiuliza wapi walikosea na pia si lazima ujifunze kupitia makosa yako, hata makosa kama haya ulitakiwa ujiulize Mr. Nice alikosea wapi ili na wewe usije kutumbukia kwenye hilo shimo.

Hizo sababu unazozieleza hapa ni mawazo ya kimasikini na ukishikilia msimamo huo hutaendelea kama kwenye maisha yako wala nafsi yako.

Maisha yana fomula ila kwakuwa upeo tunatofautiana sitapoteza muda wangu kukuelimisha sababu nimeeleza juu na zinajitosheleza
 
Back
Top Bottom