Mpenzi wangu kanicheat mara mbili na wanaume wawili tofauti, Inaniuma sana

Habari ya muda huu wakuu

Katika miezi kadhaa iliopita nilitokea kuumizwa na msichana niliempenda sana, alinicheat katika mazingira ambayo kila nikiyafikiria huwa yananiumiza sana maana sikuwahi kumkosea na hata nikimkosea tulikua tunaelezana na kusameheana na maisha kuendelea.

Sio siri kupenda ni uchizi asee maana alinicheat mara ya kwanza ilitokea nikafaham nikasamehe yakaisha but kibaya zaidi akaja kurudia kwa mara nyingine, tuligombana sana ila mwisho wa siku nilimsamehe tena.

Simtetei ila kwa sasa kiukweli amebadilika na kuwa mwenye mapenzi ya dhati.

Kinachoniumiza ni ile situation ya kunicheat mara 2 na wanaume wawili tofauti ndio imebaki katika kumbukumbu kichwani mwangu, kila nikikumbuka alivyokua akiniaga kwa kunidanganya kumbe anaenda kwa mwanaume mwingine huwa nachukia sana maana ukiangalia kwa upande wangu toka nimekuwa nae sijawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke mwingine.

Kumpenda nampenda ila nikikumbuka alichonifanyia huwa nachukia sana na kukosa raha. Natamani ningeweza kusahau lakini nashindwa kwakuwa nilimwamini sana sana..,
Hujitambui wewe!Haribu muda wako na mwishowe utaharibu afya yako,ukishapata ukimwi utatulia,Shauri yako Boya wewe!
 
Hivi wanaume mna matatizo gani? tuseme kipindi chote mlichokua hamuelewan ulikua hauruki ruki na wanawake wengine? kwanini mnapenda sana kujihesabia haki, yeye ndo unamuona mkosefu tu.Kama unampenda kweli utamsamehe na kusahau hata kama alichit mara sabini!
Huna haki ya kumuhukum mtoa post. Ameumia na hajawah kucheat... ww unaleta assumption za kutaka kumuweka kwenye kundi la wanao cheat wakat demu wake ndio ka cheat...
Acha kutetea dhambi.. dema ame cheat na itabaki kuwa hivyo..
 
Kaka nakushauri kama ulikuwa na mpango wa kuoa pls sitisha huo mpango.
Fisi hataacha kula mifupa hata kama ukimpa minofu mwaka mzima.

Huyo demu wako ni tabia yake.. hapo kaongeza mapenz ili kukufumba macho, lakin ukifika wakati ata cheat tena.
Mteme faster........
 
Yeye mwenyew ni shahidi juu ya uwezo wangu wa kupata gal mwingine co shida ila ilitokea nikamuheshimu sana
Sasa tatizo ni nini brother... why unaumia moyo kiasi hiki wakati uwezo unao..? piga chini my man.
Huyu ame cheat mara mbili na ata cheat tena na tena.. huwa hawaachi
 
Huna haki ya kumuhukum mtoa post. Ameumia na hajawah kucheat... ww unaleta assumption za kutaka kumuweka kwenye kundi la wanao cheat wakat demu wake ndio ka cheat...
Acha kutetea dhambi.. dema ame cheat na itabaki kuwa hivyo..
Mie sijamuhukumu..FYI kumuamini binadamu ni kitu kigumu sana!huu ni upande mmoja tu wa story what if huyo Dada naye alikua na sababu kedekede za kucheats zilizosababishwa na jamaa?
 
Kiongozi pole sana.....sio ametulia sema kabadilisha mbinu za kukucheat.

Swali.Je alivyokucheat ulimuliza kwa nini alikucheat au sababu zip zilipelekea akakucheat. kama ndio alikuambia UMEJIREKEBISHA au UMETEKELEZA maombi yake....kama hujamuliza sababu elewa anaendelea kufanya yake ila tu kabadilisha mbinu.....Huyo binti ni hatari kwa afya yako na uchumi wako
 
Oa kwanza kaka mdogo ili uje na mkeo. Paw kazeeka siku hizi ana wivu kama ananichumbia. Halafu ukija na mkeo namkabidhi jiko apike nimtesti
Najua tangu siku ile hadi leo urojo utakuwa umeisha,sasa unaweza kunikaribisha kingine aisee?

Hebu fanya fanya unikaribishe buanaa!!
 
Oa kwanza kaka mdogo ili uje na mkeo. Paw kazeeka siku hizi ana wivu kama ananichumbia. Halafu ukija na mkeo namkabidhi jiko apike nimtesti
Acha kuanza visingizio banaa....

Mara kka mdogo mara nioe kwanza yote ya nini hayo?

We nikaribishe bana....
 
Back
Top Bottom