Mpenzi wangu anaomba ruhusa ya kutoka na marafiki zake leo usiku Valentines day

Salama JF.,
Ikiwa leo ni siku ya Valentine nimerudi kutoka job naona mwili umechoka sana kama nina dalili za malaria.
Mpenzi wangu toka mchana nimempa taarifa kwamba sipo vizuri kiafya. Ila cha ajabu jioni hii anaomba kutoka na rafiki zake kwa kuwa leo ni Valentine day. Kinachoniuma zaidi badala angenitake care ajue hali yangu inaendelea aje yeye ananang'ania kutoka tuu na rafiki zake wa kazini.
Ukizingatia tunaishi pamoja hapa mjini ila kila mtu ameajiriwa sehemu tofauti.
Naomba ushauri anapokwenda kuna usalama kweli kwa wale wajuzi wa mambo
Mkuu pole sana na kuumwa,""lakini kwanini usifikirie tofauti kwamba anatoka tu na rafiki zake,pasipo kujihusisha na vitu vingine..Kwanini ujihaminishe vitu tofauti,,je kwani ni kawaida yake kutoka hivyo,,,...
 
Back
Top Bottom